Serikali Isipotekeleza Maazimio 23 ya Bunge Kwa Usahihi, Bunge Litafanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali Isipotekeleza Maazimio 23 ya Bunge Kwa Usahihi, Bunge Litafanyaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Nov 14, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wapendwa wanaJF, katika Mkutano wa 16, Kikao cha 44 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania cha tarehe 1 Agosti, 2009, Spika wa Bunge hilo, Mh Samweli Sitt aliiomba Serikali ihakikishe kwamba suala la Richmond Development Company LLC liwe limefikia mwisho kabla ya kumalizika kwa mwaka huu. "Waheshimiwa Wabunge, sasa imefika hatua Kamati ya Uongozi iliamua kwambasuala hili la RICHMOND tulimalize mwaka huu lisiwe linaendelea kama mengine. Kwahiyo, nilimwandikia Mheshimiwa Waziri Mkuu nikiweka wazi kwamba tunahitaji kwa faida ya Taifa letu jambo hili tuliweke mwisho. Serikali ilete maelezo kwamba mmefikia wapi sasa na hayo mnayotujibu yaturidhishe kwamba ndiyo utekelezaji wa yale tuliyoazimia." Alisema Spika Sita.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Nov 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  (Contd...)

  Spika Sita alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba: "Hatima yake sisi tutaamua na baadhi ya maamuzi yanaweza kuwa ni magumu sana hatuna ukomo wa kitu cha kuamua hapa, tukiendelea kuridhika kwamba Serikali tuhaitaki kufanya yanayoazimiwa na Bunge ambayo mtu yeyote mwenye busara analionani jambo la haki kutendeka, tunaweza tukafika mbali zaidi. Waheshimiwa Wabunge, nadhani mnanielewa, kwa sababu Serikali inawajibika kwa Bunge kupitia kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu hilo siyo tatizo kubwa sana, sidhani kama tutafika huko. Waheshimiwa Wabunge, nadhani sasa mmeelewa."
  Kwa kauli hizo za Spika Sita nilizozinukuu hapo juu nina maoni yafuatayo:
  1. Suala la Richmond haliwezi kuisha mwaka huu kwa sababu hakuna kikao kingine cha Bunge kwa mwaka 2009, kwa hiyo Serikali haitapeleka utekelezaji wake kwa Bunge kwa mwaka huu.
  2. Tayari Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda ametoa kauli kwamba malumbano miongoni mwa vyombo vya Serikali hayana tija yoyote kwa hiyo hayataruhusiwa kuendelea.
  3. Kuna kila dalili kuonyesha kwamba suala la Richmond halitajadiliwa tena, kwa hiyo mapendekezo ya Bunge yatakuwa yametiwa kapuni.
  4. Kama mapendekezo ya Bunge hayatakuwa yametekelezwa na Serikali, Bunge litakuwa limedhalilika mno.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Nov 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  (Contd...)

  Ili Bunge lisidhalilike, Je, litachukua hatua gani kuficha fedheha hiyo au litakaa kimya? Spika Sita alidai kwamba Bunge linaweza kufika mbali zaidi, japokuwa hakufafanua kuwa litachukua hatua gani. Nionavyo mimi Bunge lina baadhi ya meno yafuatayo dhidi ya Serikali:
  1. Kama Bunge litaamua kumwondoa Rais madarakani, Kanuni ya 121 ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007, (pia Ibara ya 46A ya Katiba) inaeleza kwamba Bunge linaweza kumwondoa madarakani Rais kwa makosa matatu: (a) kama ametenda vitendo ambavyo kwa ujumla vinavunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (b) kama ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa Vyama vya Siasa yaliyotajwa katika Ibara ya 20(2) ya Katiba; na (c) kama amekuwa na mwenendo unaodhalilisha Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano. Isipokuwa kwamba, hoja ya namna hiyo haitatolewa, ndani ya miezi kumi na miwili tangu ilipotolewa na kukataliwa na Bunge.
  2. Kama Bunge litaamua kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa Kanuni ya 133 ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007 na Ibara ya 53A ya Katiba.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Nov 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  (Mwisho...)

  Maswali ya kujiuliza ni kwamba,
  1. Je, Spika Sita alipodai kwamba Bunge linaweza kufika mbali zaidi alimaanisha kwamba Bunge hilo litatumia meno yake niliyoyataja hapo juu kuing'ata Serikali na hatimaye kuiporomosha?
  2. Kwa nchi kama Tanzania, ambako kuoneana haya ni kama Sheria na viongozi wetu huwa wanaonekana wakali na wanachukua hatua pale ambapo kuna maslahi yao binafsi na sio ya nchi, inawezekana Bunge likaazimia kweli kuiporomosha Serikali ya Kikwete ili hali wabunge wenyewe hawajui kama watarudi tena madarakani baada ya kuitishwa uchaguzi mpya?
  3. Kama ni hapana Spika Sita anapodai kwamba Bunge litakwenda mbali zaidi anamaanisha nini?
  Kazi kwenu wanaJF kwa ajili ya mjadala!
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Nov 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  WanaJF karibuni kwa ajili ya comments kama zipo!
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Spika ni ndumilakuwili ndiyo tatizo..hapa ndipo alipotakiwa kuonyesha speed and standards zake, serikali ilitakiwa ibanwe kisawasa itoe majibu..badala yake amewafanya wabunge na watanzania "matoy"
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Nov 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure, this is the golden chance for the Speaker of Speed and Standards to go beyond the red line!
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  spika siyo ndumila kuwili issue ni kwamba kwa CCM ilivyo oza kila kona mzee sitta akiamua kuegemea kwenye ukweli kama alivyo jaribu atauawa na walio muua kolimba kwa sababu hiyo ndo silaha ya mwisho ya CCM.

  Kumbuka Mkapa alivyo muua Gen. Imrani Kombe.
   
 9. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Basi muongezee na sifa nyingine baada undumilakuwili...nayo MWOGA..anaogopa kufa kuliko kusema ukweli..he is just aniother disapointment in our leaders...
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Spika Sitta na CCM yake wote ni mafisadi hiyo ni kesi ya nyani...unategemea nini hapo...changa la macho hilo...mnazubaishwa.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Nov 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Haka kasuala kamekaa vibaya sana! Ni sawa na ile issue ya watu waliochomewa nyumba zao na Serikali kwa maelezo kwamba walikuwa wamevamia eneo la hifadhi, kijiji cha Nyamuma, Wilayani Serengeti. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, chini ya Jaji Robert Kissanga, ilamua walipwe mamilioni ya fedha kama fidia, lakini Serikali haikuwalipa (Waziri mhusika alitamka maneno machache tu-"hili halitekelezeki" and that was the end of the story)! Katika hatua kama hiyo Serikali inalazimishwaje kutekeleza maamuzi au mapendekezo yaliyotolewa na chombo kingine?
   
 12. T

  Teroburu Member

  #12
  Nov 14, 2009
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jibu lipo katika madaraka ya Bunge yaliyoaainishwa na Ibara ya 63 ya Katiba. Ibara hii inatuambia wazi kuwa Rais ni sehemu moja ya Bunge. Si busara kwa demokrasia kwa sehemu ya pili ya bunge kudai jibu linalolikubali. Sio lazima Bunge liridhike na majibu yote yaliyotolewa. Ushauri wangu ni kuwa sehemu ya pili ya Bunge ingeendelea na shughuli nyingine muhimu kwa kwa taifa letu. Shughuli kama kuangalia uwezekano wa nguvu umeme wa nuklea [kwa matumizi ya amani]. Wananchi wanapenda kupata nishati na sio malumbano kuhusu maamuzi yaliyopita na pengine kukosewa.

  Je sehemu ya pili ya Bunge inaweza kuchukua hatua gani ? Ibara ya 63 inatoa upeo wa hatua zinaoweza kuchukuliwa :
  63-(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
  (3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza–
  (a) kumuuliza Waziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;
  (b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
  (c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;
  (d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;
  (e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Serikali Isipotekeleza Maazimio 23 ya Bunge Kwa Usahihi, Bunge Litafanyaje?

  Jibu ni Rahisi sana Mkuu

  HALITANYA KITU

  Lilkuwa na Nafasi ya Kufanya KITU lakini halikufanya KITU so Halitafanya KITU
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mmmhhhh....Mkapa aliingia Urais rasmi Tar 23 November 1995.............Gen Kombe aliuawa tar 30 June 1996..........im just trying to comprehend this.........

  Tar 21 May 1996 Maafa MV Bukoba

  Tar 30 June 1996 Gen Kombe auawa

  Tar 13 February 1998 mauaji mwembechai

  Tar 21 January/February (correct me please) 2001 mauaji Zanzibar

  Tar 24 June 2002 Ajali mbaya ya Treni nje kidogo ya mji wa Dodoma

  UFISADI

  mengine ongezeeni

  Matukio ya Moto.....duuhh
   
 15. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #15
  Nov 15, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kumbe Spika 6 alikuwa anatingisha kiberiti kwa kudai eti Bunge linaweza kuchukua maamuzi magumu? Kama kulikuwa na wakati wa "wapambanaji" kuonyesha makeke yao, wakati muafaka ndio huu ambapo kuna kila dalili ya Bunge kulambwa chenga ya mwili na Sirikali! Wametishiwa kuhusu kupokea posho mbili kwa kazi moja "upambanaji" umeishia wapi? Kaaazi kweli kweli!
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Nov 15, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kuisimamia na kuishauri serikali? Sasa Spika 6 anaposema Bunge litachukua maamuzi magumu, naona hapo amevuka mpaka wa kuisimamia na kuishauri Serikali, nisahihishwe kama nimekosea!
   
 17. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #17
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaposimamia kitu inabidi kitekelezwe kadri ya matakwa yako
   
 18. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #18
  Nov 15, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Unataka kuniambia yale maazimio 23 ya Bunge yalikuwa ni maagizo na sio mapendekezo, kama ni lazima yatekelezwe?
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,603
  Likes Received: 18,639
  Trophy Points: 280
  Asante Buchnan, Spika 6 ni oportunity kama walivyo wengine, huku ataka na kule ataka, anauwezo wa kuisimamia serikali, serikali isipotekeleza maazimio ya bunge, inatakiwa iwe voted out, anachoogopa 6 ni kuwa akiongoza vote out process, na yeye atakosa ulaji kwani rais kama sehemu ya bunge, atalivunjilia mbali hilo bunge na wabunge wote kulazimika kuja kupiga magoti kwa CCM kuomba kuteuliwa hivyo 6 would loose.

  Nilisema kama 6 ameruhusu bunge liahirishwe mpaka feb, 2010 na viporo hivyo, huu ni uthibitisho jamaa amedhibitiwa na mafisadi and has bowed down to pressure. Njaa jamani ni ugonjwa mbaya sana!.
   
 20. T

  Teroburu Member

  #20
  Nov 15, 2009
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujakosea. Baada ya kuishauri serikali, serikali itafanya kazi zake kwa mujibu wa Sheria. Serikali haiwezi kushinikizwa kufanya jambo ambalo ikilifanya itakuwa imevunja sheria na taratibu zilizotungwa na bunge hilo hilo. Bunge inaweza kutumia nguvu zake za kisiasa kwa mfano VOTE OF NO CONFIDENCE na uchaguzi kufanyika. Pengine hoja itolewe ya kuondolewa kwa hoja hiyo na kura za wabunge zipigwe.

  Zaidi ya hapo madaraka ya bunge ni-63-(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza–
  (a) kumuuliza Waziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;

  (b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
  (c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;

   
Loading...