Serikali isipo onyesha ujasiri kwenye rushwa Tanzania itakuwa Somalia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali isipo onyesha ujasiri kwenye rushwa Tanzania itakuwa Somalia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Jan 27, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Serikali ya Tanzania isikoonyesha ukakamavu wa kupambana na rushwa nchi yetu itakuwa kama somalia. Wananchi wa Tanzania wamefikia wakati wa kuchoshwa na hali ya juu ya rushwa ambayo kila mtu anakubali kuwa italeta michafuko mikubwa nchini. Matatizo kama migomo, umeme, elimu, polisi na afya ni kutokana na kutokuwa na pesa kwa serikali. Pesa nyingi zimetumika kwenye kampeni na rushwa hivyo ni watu wachache sana wanao control pesa za Tanzania. Hata biashara hazina ushindani ukitaka kuleta dawa za matibabu unaambiwa kuna kampuni fulani zimechaguliwa, ukitaka kuleta mitumba unaambiwa kuna kampuni zimechaguliwa, ukitaka kuleta bidhaa za mafuta/nishati unaambiwa kuna kampuni zimechaguliwa. Serikali inadiriki kununua gari moja lenye thamani ya zaidi ya milioni mia wakati polisi hawana magari, wanafunzi hawana madawati, na hospitali hazina vitanda. Nchi yetu kama serikali isipokuwa makini itakuwa kama Somalia.
   
Loading...