Serikali isilaumiwe mno mafuriko, waathirika wamechangia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali isilaumiwe mno mafuriko, waathirika wamechangia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Dec 23, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Kwa mtazamo wangu naona hoja dhaifu kuilaumu serikali 100% kwa yaliyojilia katika mafuriko Dar na athari zake. Ya miundo mbinu ni haki serikali kulaumiwa, ya kuchelewesha huduma za uokoaji ni lalamiko sahihi, na hili la watu kuishi mabondeni si haki lawama zote kuelekeza serikalini wakati waliojenga mabondeni wanaakili timamu. Nasema lawama hizi ni nadharia za mtindo wa maisha ya kufikiria tatizo lijapo serikali ndiye mhusika, hapa kuna udhaifu mkubwa na upeo finyu.

  Nadharia kwa maana kwamba wanaoishi huko mabondeni si kwa kujitakia ila mazingira na uwezo wao haukukwepeka, ndio maana walichagua kuwa tayari kutaabika kwa yahayojilia kuliko kubaki kuwa homeless kutokana na nafasi, uwezo kutowawezesha. Na wengine ambao uwezo ungeweza kuwaruhusu kujenga maeno stahili walizembea wenyewe kujitosa kujenga maeneo hatari.


  Zamani nilifikiri Watanzania tu ndio tuko wajinga hivyo, lakini nilishika tama siku moja nilipokuwa nchini Marekani mafuriko yalivyotokea katika mmojawapo ya mji ambao ni makao Makuu ya serikali ya state. Kando ya mto majengo makubwa na mahoteli yamejengwa kando yake umbali usiozidi meter 500, hali kadhalika stadium, ofisi za serikali, makampuni, makazi ya watu nk.

  Cha kushangaza madaraja yamejengwa juu sana na hayakumbwi na adha ya mafuriko, lakini majengo, ofisi na mahoteli hayakuchukuliwa maanani kujengwa mbali na mto ili kuepusha kama mafuriko yakitokea. Na mbaya zaidi sehemu kubwa ilipojengwa ninayoongelea ni tambalare hali ambayo ni kiashirio cha mafuriko yakitokea hapakwepeki.

  Mafuriko yaliyotokea hapo na kushuhudiwa na mimi mwenyewe ni historia ambayo haitasahaulika, kwani number one shopping center ambayo ilikuwa inaiingizia serikali mapato makubwa na resort zake ilifungwa kwa miaka 2-3 hadi kuirejesha katika hali yake ya kawaida baada ya kutumia mabilioni kuikarabati. Stadium ilikuwa ni lake-pond, vituo vya mafuta ndani ya maji, ofisi za serikali kufungwa, makazi ya watu kujaa maji, miundo mbinu kuharika nk. Sikutegemea kama watarudia huko tena bali kuhamisha.

  Nilichoshangaa wamerudi tena huko na kuendelea na shughuli kama kawaida ingawa mazingira yale kwa mtazamo wangu hayaruhusu. Nilikuwa naongea na mzungu mmoja kwamba hali kama hii ingetokea Africa ninyi wazungu mngetudharau na kuona licha ya umaskini tunashindwa kufikiri vizuri na kuona mbali, lakini nini kinatokea na bado mnarudia kosa juu yakosa? Aliniangalia tena kwa mara nyingine kwa nusu dakika, kisha akainamisha kichwa na kunivuta mkono, kisha akaniambia; "binadamu kiumbe cha ajabu na hivyo ubinadamu na mazingira ya kiuchumi yanapewa kipaumbele zaidi kuliko mafuriko yanayopita kwa siku moja ukilinganisha watu ambao maisha yao ndio majengo, viwanda, ofisi na mengineyo katika maeneo haya."

  Naweza kusema binadamu kiumbe cha ajabu, ni rahisi kuweka utaratibu na sheria ambayo kwa akili ya kawaida unaona itatekelezeka na huyo huyo kesho atafanya kinyume cha alichoamini kuwa sivyo. Pengine fikra za kibinadamu na utu huchukua nafasi zaidi, na pengine kutanguliza busara kuliko kutoa tamko la jumla bila kufikiria mazingira ya mwadhirika. Mambo haya rahisi kwangu kumnyooshea kidole fulani wakati mazingira ya ninayemnyooshea kidole sijakumbwa nayo. Na mwadhirika hatakoma kumlalamikia mwingine hata kama mwenyewe alikuwa na nafasi ya kutengeneza mazingira ya kutoathirika hapo awali. Nadharia bila vitendo ni hekaya za kufikirika.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wamiliki wa nyumba wanapewa viwanja bure, je hawa wapangaji ambao ni waathirika pia ambao hutegemea nyumba hizo kuishi watafanyeje wakati walishalipia nyumba hizo kwa miezi 6 au mwaka mmoja?
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ulitaka wakaishi milimani wakati uwezo huo hawana?
   
 4. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Du! Mitaro iliziba na taka za mifuko ya rambo usipime, mabwawa ya maji taka vingunguti yametakata, mvua kubwa tokea 1954 taarifa hizi watu wanazijua na wamezikalia.
  Watu wamekuwa mabondeni na wengine wana hati, mmepeleka umeme na maji sasa bado wanachi wanabebeshwa debe la pumba, ofisi za un nao wamejenga bondeni? Mvua kubwa zimewafikia hata wasio bondeni. Njaa inatokea somalia wanafiki nyie mtasema mabadiliko ya tabia nchi, ikitokea kwenu mtasema uzembe wa wanachi kushindwa kulima mazao yanayoimili ukame.
  Wasaidiwe kibinadam kwanza, hao watu wamepoteza watu, mali na maisha nyie mkipeleka mikate 10 na kundi la waandishi na camera ili mtokee ktk media.
   
Loading...