Serikali isilaumiwe kwa hali ngumu ya maisha-JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali isilaumiwe kwa hali ngumu ya maisha-JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 13, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,784
  Likes Received: 83,143
  Trophy Points: 280
  Serikali isilaumiwe kwa hali ngumu ya maisha-JK

  2008-10-13 10:24:10
  Na Thobias Mwanakatwe, Kyela

  Rais Jakaya Kikwete amesema kushuka kwa uchumi wa dunia hivi sasa ni lazima kutaathiri uchumi wa taifa, na hivyo hakuna sababu kwa wananchi kulaumu kwamba serikali inawatesa kutokana na hali ngumu ya maisha.

  Akiwahutubia wananchi wa mji wa Kyela juzi, alisema hivi sasa uchumi wa dunia umekumbwa na msukosuko mkubwa kuliko yote katika historia toka mwaka 1930 ambapo hali hiyo haijawahi kujitokeza.

  Alisema pamoja na kuwepo kwa msukosuko huo wa uchumi wa dunia, hata hivyo serikali bado haijaanza kujipanga kukabiliana na hali hiyo lakini baada ya miezi michache ijayo athari zitaanza kujitokeza.

  Hata hivyo, Rais Kikwete alisema serikali inaendelea kutafakari ni jinsi gani itaikabili hali hiyo ili kusijitokeze athari zaidi katika uchumi.

  Alisema hivi sasa kutokana na msukosuko wa uchumi, serikali ya Marekani imetenga Dola 700 bilioni kujaribu kuokoa mabenki yanayofilisika, mkakati ambao pia unafanywa na Uingereza,Ujerumani, Japan pamoja na nchi nyingine.

  ``Wenzetu wanao uwezo mkubwa wa kiuchumi sijui yakitufika sisi itakuwaje, tunaendelea kutafakari ili na sisi yatakapotukuta tufanye nini lakini siyo kazi rahisi,`` alisema Rais Kikwete.

  Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo hakuna sababu kwa wananchi kulalamika kuwa serikali inatutesa kwa sababu kushuka kwa uchumi wa dunia athari zake zinazikumba nchi maskini ikiwemo Tanzania.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,784
  Likes Received: 83,143
  Trophy Points: 280
  This guy is talking on both side of his mouth. Hapa anasifia ongezeko la mapato ya TRA.
  President Jakaya Kikwete has announced that Tanzania Revenue Authority (TRA) last month broke its monthly revenue collection record after collecting 427bn/-. Kama uchumi wetu una matatizo inakuwaje mapato ya kodi yanaongezeka kwa kiasi kikubwa kama hiki!?

  Na wakati huo huo anataka kuficha uwezo wake mdogo katika kuiongoza Tanzania kwenye matatizo ya uchumi wa dunia. JK, tungekuwa tunapata angalau 40% ya mapato ya machimbo ya dhahabu yetu badala ya 3% basi tungeweza kufanya mambo mengi sana kuinua viwango vya maisha vya Watanzania wengi. Ungeweza kupunguza ukubwa wa serikali yako na kupunguza gharama kubwa za uendeshaji ya serikali zikiwamo za safari zako za nje ya nchi, savings ya hapo ingeweza kuhamishiwa katika nyanja nyingine muhimu na kuleta ahueni kubwa katika nyanja hizo. Matatizo mengi ya uchumi wa Tanzania hayasababishwi na matatizo ya uchumi wa dunia.

  Kwa miaka mingi iliyopita uchumi wa Dunia ulikuwa unafanya vizuri sana, lakini Watanzania wengi hawakuona ahueni yoyote, kwa hiyo basi matatizo ya sasa ya uchumi wa Dunia yasitumike kuficha uwezo wako mdogo wa kutatua matatizo ya Watanzania. Wengi tunaamini Tanzania ina uwezo kabisa wa kutatua matatizo yetu mengi ya kiuchumi hata kama uchumi wa Dunia si mzuri.
   
 3. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Great BaK, watanzania kila siku uchumi wao ni mbaya hata kama wa dunia mzuri. Naamini tuna rais mwenye kichwa cha nazi! Tatizo anaongea kama anasema na wajinga. Watanzania si wajinga tena. Sawa uchumi wa dunia mbaya, yeye amefanya nini kusaidia? Yeye si aliomba kura kwa ajili ya kutupatia Maisha bora kwa Kila Mtanzania? Au amesahau? Grrrrrrrrrrrrrrrr!
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Oct 13, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  AACHE Upuuzi bwana

  Alisema "SITEMBEI NA FUKO LA HELA"

  KISHA "VUMILIENI MAISHA MAGUMU"

  KISHA "NIMEWAPA MAWZIRI WAWILI WAANDAMIZI CHOKO CHOKO ZA NINI TENA?"

  KISHA "KELELE ZA MLANGO HAZIMZUII MWENYE NYUMBA KULALA"

  KISHA "SIASA BASI,TUKISOMESHA WANASHERIA TUTAISHIA KUFUNGANA TU"

  KISHA "SHURUBATI"

  THEN "NAWAPA MUDA WEZI WA EPA WARUDISHE"
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,784
  Likes Received: 83,143
  Trophy Points: 280
  Date::10/13/2008
  Mrema ahoji wapi maisha bora kwa kila Mtanzania
  Na Hemed Kivuyo, Arusha
  Mwananchi

  MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, juzi alikuwa akihutubia wananchi wa kata ya Sombetini jijini Arusha, gazeti la Mwananchi na kuwataka Watanzania wamuulize Rais Jakaya Kikwete ahadi zake za maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Mrema alipanda jukwani kumnadi mgombea udiwani kupitia chama hicho, Emmanuel Lobulu na kabla ya kuongea na wananchi alishika gazeti la Mwananchi toleo la Jumamosi (Oktoba 11) na kusoma kichwa kikubwa cha habari na baadaye kusoma habari hiyo kwa kutumia kipaza sauti, akiwanukuu wananchi wa mkoani Mbeya wakimtaka Rais Kikwete awafikishe mafisadi mahakamani na kuhoji ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Mrema aliwataka wananchi wa kata hiyo kusoma gazeti hilo kwa kina, hasa habari hiyo na kudai kuwa, Mkoa wa Mbeya umeonyesha mfano wa kuigwa na hivyo kata ya Sombetini iwaige kwa kumuuliza Rais Kikwete maisha bora aliyowaahidi.

  Mrema, ambaye amewahi kuwa mbunge wa majimbo mawili tofauti kwa nyakati tofauti akiwa vyama tofauti, aliwataka wakazi hao wasimpe kura mgombea wa CCM na hata Rais Kikwete katika chaguzi zijazo.

  "Someni gazeti la Mwananchi la leo (juzi), mwuone wananchi wa Mbeya walivyombana Kikwete... wamemuuliza yako wapo maisha bora uliyotuahidi? Sasa nataka kuwaeleza msipe kura mtu yeyote wa CCM hata huyo Kikwete kwa kuwa amewadanganya," alisema Mrema huku akiwa ameshika gazeti hilo.

  Pia Mrema aliutupia shutuma uongozi wa Rais Kikwete na wasaidizi wake kwa madai kuwa, umeshindwa kuongoza na badala yake nchi imeshamiri kwa ufisadi na kushindwa kuwafikisha mahakamani walioiba fedha za wananchi.

  "Serikali ya Kikwete imeshindwa kazi yeye pamoja na wasaidizi wake... nchi sasa imejaa mafisadi wanaoiba fedha za wananchi na hawafikishwi mahakamani. Msimpe kura mgombea wa CCM kwa kuwa mtoto wa fisi ni wa fisi tu," alisisitiza Mrema.


  Katika hatua nyingine, diwani wa kata ya Sokoni One, kupitia TLP, Michael Kivuyo alidai kuwa wananchi wa kata ya Sombetini wamefanyiwa hujuma na CCM kwa kumhadaa aliyekuwa diwani wa kata hiyo na kuhamia chama hicho tawala.

  "CCM wamewahadaa wananchi wa kata hii, wamemchukua diwani wenu na sasa amekuja kugombea kwa kofia ya CCM. Huu ni usaliti na mchezo mchafu. Ninyi sio watoto wa kudanganywa... msimpe kura zenu," alisema Kivuyo.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Cha ajabu zaidi ni kwamba hali ngumu ya maisha Tanzania haikuanza jana! Kisha ni wananchi wangapi Tanzania wenye kuwekesha fedha zao, wanaopewa mikopo kuendesha shughuli zao za kila siku bila kuweka rehani nyumba na mashamba yao. Asilimia 80 ya Wadanganyika fedha zao zipo chini ya mito yao, kila mtu hubeba mzigo wake ndio strategy ya uchumi inayoendeshwa na serikali, mkopo wa nyumba ni lazima serikali iwe na share (NHC -NSSF) - thamani ya nyumba zimepanda kwa asilimia 100 within 5 yrs, iweje leo matatizo ya Ulaya na US yabebe hotuba ya JK kama vile uchumi wetu unaendeshwa sawa na wao..
  Hizo credit card zenyewe ni lazima uweke fedha zako kwanza kabla hujaitumia ina maana credit card Tanzania haina tofauti kabisa na Debit card sema tu tofauti ni kwamba credit card Unaweza kuitumia kwa malipo nchi za nje!..
   
 7. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #7
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mtizamo wa JK na serikali yake ni kuwa wananchi wa Tanzania wanaweza kunyamazishwa na kudanganywa kupitia ziara za mikoani.Mkakati huu ulibuniwa makusudi eti kwa madai ya kuenzi harakati za hayati mwalimu Nyerere ambaye alikuwa kiongozi anayewatembelea wananchi vijijini na kufahamu maisha yao ya kila siku.

  Anachojidanganya nacho Kikwete ni kuwa anaendeleza kazi na mvuto uleule aliokuwa nao Mwalimu ili hali siyo kweli.Watanzania wa vijijini hawahitaji soko la mitaji la WALL STREET au FRANKFURT ili wajipatie mahitaji yao ya kila siku.Hali duni za wakulima na wafugaji wa vijijini zinahitaji sera nzuri ambazo zitatilia maanani uwepo wa rasilimali watu,rasilimali ardhi na maliasili zilizopo kusudi kila mwananchi afaidi uwepo wake.

  Leo hii watu wa mbeya hawahitaji dola bilioni 700 za bush Kusudi waweze kuendeleza kilimo cha chain a mchele.Hawahitaji kujua Bush anafanya nini ili wananchi wa Kahama,Shinyanga, Tarime na kwingineko waweze kufaidi kutokana na madini yapatikanayo kwa wingi na Tanzania kwa ujumla ijipatie faida stahili kutokana na uwekezaji wa aina yoyote.

  Watanzania wanaona na wanasikia kuliko wakati mwingine wowote tangu waanze kuishi.Wanatambua kuwa wanaibiwa na bahati mbaya sana wezi wa mali zao na uhuru wao hawaji usiku na wala hawavunji mlango, wanakaribishwa na watawala wao na kutembezwa wajionee milki yote na kujichagulia pa kumiliki.

  Watanzania siyo mabwege tena na wala hawatanyamaza kimya.Wameshaazimia kupambana vita vitakatifu kurejesha mali zao na uhuru wao.Vita yao imeanzia Tarime na itasambaa kila kona ya nchi.Ukitaka kujua serikali ina wakati mgumu waulize wananchi walioko hukohuko anakotembelea Rais.
  Leo wananchi wa Mbeya walitoa malalamiko yao kupitia radio clouds kuwa wandishi wanaoandamana na Rais huko Mbeya hawatoi taarifa sahihi juu ya kila kinachotokea.Wanashangazwa inakuwaje pale Rais anapokutana na upinzani wa wazi kutoka kwa wananchi waliokwisha kuchoshwa na ahadi hewa za sisiemuu waandishi hawa awaziripoti taarifa hizo.

  Rais wetu anaweza kuwa anao mvuto kwa raia wengi lakini ukweli ni kuwa imani ya wananchi asilimia 80 waliomwingiza ikulu mwaka 2005 imeshuka kwa kasi kama anguko la uchumi huko kwa rafikiye kipenzi,George Bush.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee wa gumzo,
  Haya maneno mazito sana labda kwa kifupi niseme hivi kwa Mtanzania haiwezekani kabisa picha iliyochorwa ukutani ikawa na thamani kuliko magunia 10,000 ya mchele...kwa hao wazungu na wall street ndio biashara na maisha yao. Mpira wa baseball unaweza kuuzwa kwa mabillioni kwa sababu tu ulipigwa homerun na celebrity, michoro ya rangi ya msanii fulani ikauzwa ghali kuliko hata thamani ya pato la taifa letu kwa mwaka...

  Haya maswala ya kuwahutubia wananchi maswala ya Wall street ni kuzidi kuwavuruga wananchi akili zao..Ni sawa na kujaribu kuwaambia wananchi kuhusu matumizi mazuri ya maji wakati maisha yao yote wameishi Jangwani...
  Huu ni Ulimbukeni..
   
 9. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii inaonyesha kwa kiasi gani raisi wetu ni mpuuzi na anafikiria waTZ wote ni wajinga. Hivi anafikiria Wadanganyika wa leo hawajui nani anayewaletea umasikini zaidi ya rushwa na matumizi mabaya ya mapato yetu? Uchumi wa TZ hivi sasa unatakiwa uwe unanawiri katika huu msukosuko wa mabenki ya magharibi.

  Dhahabu bei na demand yake imepanda, mafuta bei imeshuka, bei za pamba na kahawa ni nzuri, misaada toka nje tuliyoahidiwa haijakoma, sasa ni kwa nini JK atangaze hali ya hatari?

  Inaelekea kazi imemshinda na sasa anajaribu kutafuta sababu ya kujikingia. CCM wanatakiwa wasikubali kwenda chini pamoja na JK kwa upuuzi wake. Inabidi waanze kupiga kelele za kutokuwa na imani na uongozi wake otherwise, yaliyotokea Mwanjelwa alipozomewa yatageuka kura za kukataliwa CCM wakati wa uchaguzi.
   
 10. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2008
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani polepole, Jk kwa kweli asipewe lawama zozote. Nimeconclude leo kuwa huyu mtu haelewi kabisa uchumi wa Tanzania na uchumi wa dunia kwa ujumla.

  Yeye haoni kuwa serikali hizo za US, UK zinafanya kila namna kuokoa wananchi wao wasiwe na matatizo kwa sababu ofcouse serikali hizo zinapewa na zitapewa lawama sababu ndio kazi yao kumake sure wananchi wanafanya vizuri.

  Serikali ya Tanzania inapaswa kuangalia matatizo ya wananchi na kuyasolve. Sasa huyu JK anasema serikali isilaumiwe vipi wakati serikali ni chombo tu cha wananchi cha kusaidia maisha ya wananchi?? kwani serikali ni nini??

  JK tanzania bank hazikopeshi masikini kwa hiyo hizo liquidity problems bank zetu wala hazina na wala sio issue.

  Wewe angalia namna wakulima wanavyoweza kupewa mikopo ya matractor, mbolea kwa guarantee za serikali. Serikali mkipunguza matumizi yenu yasio na msingi hamuwezi kukosa Bilioni 500 kuweka kwenye sekta ya kilimo. Ok JK acha kuangalia CNN na BBC, matatizo hayo huwezi kuelewa kabisa, sababu unadai eti hizo nchi zina hela?? Nani kakwambia US wanabailout na hela zao?? Kutoka wapi?? wanachukua mkopo wewe JK kwa kuuza treasury bills.

  Kwa hiyo na wewe siku ukiwa na uchungu na wananchi wetu, unaweza kabisa kuuza T Bills ili mradi useme tu zitapelekwa Mikoani kwa kusaidia Kilimo (80% ya wananchi wetu wako huko). Kwa hiyo Mr. presida usitofautishe serikali na wananchi kama viongozi wetu wanavyofanya, Serikali ni chombo kinachowekwa na wananchi kwa manufaa ya wananchi oops sorry sio kwetu
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sasa tumlaumu nani? Kwani serikali haikuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa inatupitisha salama kwenye uchumi huo mbaya wa dunia? Jamani, inaonekana wanakwepa majukumu
   
 12. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  "wanaoeneza maneno haya wameshiba ugali na maharage"

  "liwa ule "
   
 13. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ni kweli tusilaumu serikali bali mafisadi waandamizi ndani ya ccm, nadhani it sounds good bcoz ccm is not part and parcel to this government
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Oct 13, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ...sijui kikwete ni mjinga??

  ..hakosagi sababu..?....na hao waaandishi walioenda naye huko wanaandika kwa kumpemdelea mnasikia anapewa vibomu kweli lakini haviripotiwi.......wanasifia tu....hata watu wa mbeya leo walipiga simu redioni wakilalamikia magazeti kwa kutoripoti hali halisi ya ziara....shame!
   
 15. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tanzania itajengwa na wenye moyo.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,784
  Likes Received: 83,143
  Trophy Points: 280
  ...Na kuliwa na wenye meno alias Mafisadi
   
 17. A

  August JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Inabidi raisi aelewe kwamba Hiyo financial crisis si lazima ikumbe tanzania, na sana sana inaweza kuisaidia tanzania kwasababu export yetu ni raw material ambayo inahitaji viwandani, na nyingine ni chakula ambacho watu lazima wakile, tatu bei ya petrol inashuka, kutokana na kushuka kwa matumizi yasiyo ya lazima, na labda viwanda vikubwa vitapunguza production kama Genaral motors na magari ya ya 4 litre engine. etc
  Nne anatakiwa au anaelewa lakini anajifanya aelewi kwamba kinacho iangusha tanzania ni Ufisadi. Kitu cha Shillingi moja wao watakinunua kwa Shs 1000/ sasa uchumi utakuwa vipi au hiyo credit crunch ya nchi zilizoendelea zitadhuru vipi uchumi wetu?
  Ndio hayo hayo ya kuvuja kwa mitihani
   
 18. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #18
  Oct 13, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Na wakati huo huo anataka kuficha uwezo wake mdogo katika kuiongoza Tanzania kwenye matatizo ya uchumi wa dunia. JK, tungekuwa tunapata angalau 40% ya mapato ya machimbo ya dhahabu yetu badala ya 3% basi tungeweza kufanya mambo mengi sana kuinua viwango vya maisha vya Watanzania wengi. Ungeweza kupunguza ukubwa wa serikali yako na kupunguza gharama kubwa za uendeshaji ya serikali zikiwamo za safari zako za nje ya nchi, savings ya hapo ingeweza kuhamishiwa katika nyanja nyingine muhimu na kuleta ahueni kubwa katika nyanja hizo. Matatizo mengi ya uchumi wa Tanzania hayasababishwi na matatizo ya uchumi wa dunia.

  Nchi haitozi kodi kwa sasa kutokana na uchimbaji wa madini! Kinachofanyika ni kodi ya Mrahaba (Royality tax) ambayo hutegemeana na aina ya madidi na kama yamesafishwa (Processed) au hapana! Kwa dhahabu Mrahaba ni 3% ya NPV duniani kote! Imeandikwa kuwa kodi itakuwa 30% ya NPV lakini haijaanza kutolewa. Hii ni kwa mujibu wa Mining act 1977/ 1998 ambayo ndo inatumika!
  Kwa sasa wako kweny tax relief mpaka payback period itakapofika. Sasa hapo inategemea!
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,784
  Likes Received: 83,143
  Trophy Points: 280
  Mrahaba unaweza kuongezwa na kufikia 10% au 15% ya mapato ya dhahabu na 25% mpaka 30% ikawa ni kodi toka kwa mauzo halisi ya dhahabu yetu. Sikuandika faida (profit) kwa sababu hawa 'wachukuaji' wanaweza kabisa wakacheza na vitabu vya mahesabu na kuonyesha wamepata hasara kubwa lakini ukweli wa mambo wamepata faida kubwa sana.
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bwana wee wanajua mkwere anapenda sifa sana hata pasipostahili....poor Tanzania hajawahi kuwa na raisi kilaza kama huyu JK...hajui watanzania waliosasa wanauwezo wa kuchambua mchele na pumba, maisha bora kwa kila Mtz yako wapi?
   
Loading...