Serikali isifanye ubaguzi, iwe tayari kuwasapoti akina 'Babu' wengine wanaojitokeza

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Wadau - natoa hoja hii:

Kwa kuwa serikali ya JK imeamua kumsapoti babu wa loliondo -- Mchungaji Mwasapila -- kwa tiba yake na kuamua kumpa msaada mbali mbali pamoja na kumtangaza nchi za nje kama ni kivutio cha utalii -

Jee pia serikali hii iko tayari kutofanya ubaguzi na kuwa tayari kuwasapoti waganga wengine wa aina hii ambao tayari wamejitokeza, au watakaojitokeza siku za mbele? Kwa kuwa serikali imejiingiza kwa huyu, basi na iwe tayari kujiingiza kwa wengine pia, na tayari wamesha anza kujitokeza.

Jibu la swali hili ni muhimu kwa sababu hadi sasa serikali haijafanya utafiti wowote kuhusu tiba ya Babu na kutoa tamko kwa wananchi wake kwamba tiba ni salama na inatibu maradhi yanayokusudiwa kutibu.

Tamko hili ni muhimu kwa sababu hapo baadaye watu wakija dhurika, basi serikali iwe tayari kubeba lawama.

 
nafikiri serikali haina makosa.

nionavyo mimi ilmepeleka kule askari, ambulence, wauguzi, huduma za vyoo, mahema nk ili kuepusha janga la kibinadamu ambalo lingeweza kutokea kufuatia maelfu ya watu na magari waliorundikamna huko bila huduma stahiki za kibinadamu kuwepo. pia iliamua kuchukua hatua hizo kuepuka uwezekano wa kuibuka njaa, upungufu wa maji salama na magonjwa kwa watu uambulizana hasa ikizingatiwa kuwa wengine walikuwa wanatolwa mahospitalini.

zingatia pia wengine waliripotiwa kufia keneo hilo la samunge-loliondo kabla na baada ya kupata kikombe walichokifuata, hivyo serikali inayojua wajibu wake haiwezi kukaa kumya wakati kuna habari za watu kupoteza maisha.

kwa maoni yangu, serikali ilichukua nafasi yake kama serikali ya kuhakikisha ulinzi na usalama na kuhudumia kwa kile kinachoangukia kwenye dhamana yake. kwa msingi huu sioni kama kuna tatizo endapo siku za usoni wataibuka "mababu" wengine na serikali kuendelea kuwajibika kwa jinsi ilivyowajibika kwa babu wa kijiji cha samunge.

naamini tuko pamoja

Glory to God
 
Back
Top Bottom