Myahudi Jr II
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 6,703
- 8,481
Naandika haya nikiwa na huzuni kubwa sana Moyoni huku nikiona kabisa hakuna “future” yoyote kwa makampuni ya wazawa na ma engineer wetu(civili) wanaozalishwa kila siku kwenye vyuo vyetu vya ndani.
Ndugu zangu nikiwa kama mdau wa sector ya Ujenzi based kwenye majengo (Building Constructions) napenda niseme neno moja tu walau SERIKALI ilisikie isaidie wahandisi wazawa na kampuni zetu za ndani za Ujenzi ili nazo zikue.Kwanza kabisa napenda nipongeze wote wenye kampuni Class 1-3 maana si lele mama kumiliki hizo class inaonyesha kuna kazi ya ziada imefanyika sana, hongereni.
Ndani ya nchi yetu sasa kuna utitiri wa kampuni za wageni hasa wachina, wamekuja kuua soko kabisa la kampuni zetu za ndani, nachosema WAMEUA KABISA KAMPUNI ZETU, ni mjinga tu atakaesifia ujio wa utitiri wa kampuni hizo bila kuelewa chochote, nawaomba CRB itoshe basi kampuni za Kichina zilizopo nchini, zimetosha, zimetosha zimetosha. Tunaua makampuni yetu ya wazawa bila kujua, tunaua mainjinia wtu bila kujua, tunapeleka wapi hili taifa la engineers wenye vyeti wasio na ujuzi??
Makampuni ya kichina ukienda nayo kwenye Tendering, usijidanganye kushinda, narudia tena usijidanganye kushida mradi wowote, wale ni vunja bei (atatoke mtu hapa atasema mlizoea wizi na Magufuli anawakomesha, Usamehewe in advance), sitaki kusema sanaaa maana wanajua wanachofanya kufidia hasara ya hiyo vunja bei, ndio maana ukifanya kazi na mchina 24/7 unatakiwa uwe nae mgongoni ukilala kidogo tu UMEUMIA.
Hizi kampuni za Kichina nyingii sana ni za serikali yao yaan 70% ya serikali huku 30% ya mtu binafsi kwa hiyo wao hawalipi mishahara bali serikali yao ndio inalipa wafanyakazi, equipments zoote ni serikali ndio ina facilitate, pia huwezi kukuta mchina hana equipments wanaazimana maana ni mali ya serikali yaani yeye haangaiki chochote.
Pili hawa jamaa unaweza ukakuta wamebid hata kampuni 3 mradi mmoja usidhani ni wajinga wale, yaani hapo ni mmoja ila kampuni tofauti tu na lazima mmoja apate huku wazawa wanapigwa chini, INAUMIZA SANA.
Naiomba serikali isaidie wazawa hata miradi ya 2.5billions kushuka chini iwe inafanya wazawa tu tuinue kampuni zetu na watoto wetu wapate ajira humo nasema hivo kwa kua mradi wa 2billions mchina atakuta amebid kwa 1.3b wakati lowest bidder wa kibongo ana 1.6b, jamani huyu analipa mishahara, ofisi, mitambo, etc etc akishuka zaidi ni majanga sana, hawezi shindana na mtu aambae anasaidiwa na serikali yake
Naweza nikawa nisiwe mzuri kuwasilisha hoja zangu ila naomba niwasilishe hivo hivo