Serikali iruhusu kuanzishwa mifuko binafsi ya Pension kwa ajili ya watu wasio na kipato cha kila mwezi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Serikali iruhusu kuanzishwa mifuko binafsi ya Pension kwa ajili ya watu wasio na kipato cha kila mwezi kama Contractors, consultants, wakulima, wachimbaji wa madini ,freelancer jounalists nk wenye vipato vya msimu.

Serikali iruhusu uanzishaji wa private pension funds wataoshughulikia na pension za watu hao.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,270
2,000
Serikali iruhusu kuanzishwa mifuko binafsi ya Pension kwa ajili ya watu wasio na kipato cha kila mwezi kama Contractors, consultants,wakulima, wachimbaji wa madini nk wenye vipato vya msimu

Serikali iruhusu uanzishaji wa private pension funds wataoshughulikia na pension za watu hao
Kabisa ni wazo zuri natumai litafanyiwa kazi
Informal sector ipo nenda nssf ujaze fomu ujiunge
Toka nimekufahamu leo ndiyo umeongea point kwa mara ya kwanza
Kwanza Serikali irudishe imani ya wachangiaji kwenye hiyo mifuko.

Kwasababu unachokisema hapa siyo kitu kipya. Kumeshawahi kuwa na mafao hao huko nyuma, hata NSSF bado kuna hiyo program.

Kwa lugha rahisi hiyo mifuko haikatai pesa ukipeleka. Ila ukiitaka pesa yako hapo ndipo pataleta utata.

Tulikuwa na mifuko takribani minne ya hifadhi ya jamii

  • NSSF
  • PPF
  • GEPF
  • LAPF

Na baadhi ya mifuko ilikuwa na mafao ya aina hiyo.

Mfano: Kuna mafundi wa mtaani walishawishiwa wawe wanaweka pesa zao GEPF ( Uliokuwa mfuko wa wastaafu ) lakini cha kushangaza huo mfuko umekufa.

Pesa zimehamishiwa PSSSF na nyingine NSSF na namna ya kuzipata imekuwa ngumu.

Imagine pesa ambazo mwenyewe umeshawishiwa kuziweka kwa hiari, leo masharti ya kuzipata yanakuwa magumu na uwezekano wa kuzipoteza ni mkubwa sana.

Kwa hali hiyo utamshawishi nani mwenye akili zake timamu akaweke pesa zake kwenye hiyo mifuko kwa hiari??
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,061
2,000
Kwanza Serikali irudishe imani ya wachangiaji kwenye hiyo mifuko.

Kwasababu unachokisema hapa siyo kitu kipya. Tulishawahi kuwa huko.

Tulikuwa na mifuko takribani minne ya hifadhibya jamii

  • NSSF
  • PPF
  • GEPF
  • LAPF

Na baadhibya mifuko ilikuwa na mafao ya aina hiyo.

Mfano: Kuna mafundi wa mtaani walishawishiwa wawe wanaweka pesa zao GEPF ( Uliokuwa mfuko wa wastaafu ) lakini cha kushangaza huo mfuko umekufa.

Pesa zimehamishiwa PSSSF na nyingine NSSF na namna ya kuzipata imekuwa ngumu.

Imagine pesa ambazo mwenyewe umeshawishiwa kuziweka kwa hiari, leo masharti ya kuzipata yanakuwa magumu na uwezekano wa kuzipoteza ni mkubwa sana.

Kwa hali hiyo utamshawishi akaweke pesa zake kwenye hiyo mifuko kwa hiari??
Well said mkuu
 

mlimilwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,415
2,000
mkumbuke ilipunguzwa baada ya kuonekana mingi.
mimi naona kitu muhimu warudishe ile sheria ya kujitoa, maana nilichokiona kwenye awamu ile sizani kama ilifanya vizuri.maana ilizuia watu kujitoa kumbe walikua nalengo la kutumia hela zao kwenye mambo yao. nahii ndio iliyosababisha watu wengi binafsi kushindwa kwenda kuweka tena hela huko.

hebu jiulize,kama walizuia watu kujitoa kwa madhumuni ya kua ni akiba ya uzeeni ,kwanini wameruhusu kukopesha kwa waajiliwa wa serkali!!
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Huo ndo wizi. Hiyo serikali yenyewe imekula hela ya wastaafu sembuse mtu binafsi
Nchi nyingi zinao fund managers private wanao manage pension fund za watu wa aina hiyo wao kazi yao kumanage na kuwekeza vizuri hizo pension za watu kwenye maeneo yenye interest kubwa au faida kubwa na wao huwa hawalipwi mishahara kama pension fund zetu ili wasile mtaji .Wao hulipwa small commission kwa sehemu ya faida wanayozalisha kama management fee

Mfano umeweka pesa zako mfuko wa pension private milioni moja wao wataizalisha na kuizungusha ikipatikana faida mfano laki tano wao wanachukua 20 percent ya faida ambayo ni laki moja kama management fee yao laki nne wanaziweka kwako unakuwa na milioni moja na laki nne wanaendelea kuzungusha ukisema siku mimi basi wanakupa pesa zako zote hizo mnaagana kwa heri ya kuonana.Anytime ukitaka kuondoka unaondoka.

Ofisi zao huwa na wafanyakazi wachache tu waweza wasifike hata 10 lakini wenye uwezo wa ku manage hata mabilioni ya pension za watu

Na zinakuwa regulated na kusimamiwa na mamlaka ya usimamizi wa mifuko ya pension
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
mkumbuke ilipunguzwa baada ya kuonekana mingi.
mimi naona kitu muhimu warudishe ile sheria ya kujitoa,

hebu jiulize,kama walizuia watu kujitoa kwa madhumuni ya kua ni akiba ya uzeeni ,kwanini wameruhusu kukopesha kwa waajiliwa wa serkali!!
Yote ilikuwa ya Serikali

Mifuko ya pension ya private ndio huwa na kigezo cha kujitoa anytime na unalipwa chako sababu wao hu act kama investment managers wa pesa yako ya pension
 

Mzigua90

JF-Expert Member
Sep 23, 2014
36,175
2,000
NSSF nadhani wana huduma ya namna hiyo kwa watu wanaochangia kwa hiyari ambao hawapo kwenye mfumo rasmi wa ajira.
 

malang0

JF-Expert Member
Apr 7, 2021
442
1,000
Unaelewa logic ya hii mifuko elewa sasa maaa yake tunakuhifadhia fedha zako maana wewe hujui kuweka akiba, je wewe hujui kuweka akiba kila hela unaingiza kwenye matumizi?sekta binafsi hatutaki hilo jambo ni kufanya watu hawana akili
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Unaelewa logic ya hii mifuko elewa sasa maaa yake tunakuhifadhia fedha zako maana wewe hujui kuweka akiba, je wewe hujui kuweka akiba kila hela unaingiza kwenye matumizi?sekta binafsi hatutaki hilo jambo ni kufanya watu hawana akili
Kifupi una expossure ndogo

Bima mfano unakata sababu una uwezo mdogo wa kukwepa ajali?

uwezo wako hata uwe nani utafikia mwisho hutaweza kufanya kile unachofanya sasa hata uwe unamiliki kiwanda ,mabasi,malori nk biashara hu change kwa ushindani ,na kuwa obsolete nk ndio maana huweko hiyo mifuko private hata ukifilisika maisha yanaendelea .Waswahili wengi unamkuta ana mabasi mia akifilisika utamuonea huruma.

Au mwanamuziki anajaza miukumbi siku ikifika kachuja unamkuta yuko hoi bin taabani kimaisha mfano mzuri tuna bi kidude.Hakuna mtanzania alizunguka dunia nzima nchi 104 kuimba alipata chake lakini alipoishiwa muziki na kuzeeka aliishi maisha magumu na watu wakawa wanalaumu serikali kuwa ohh alibeba nembo ya taifa!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom