Serikali irudishe na itambue mahakama za kimila/jadi sambamba na mahakama ya kadhi

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,940
0
Wanajamvi

Hii mahakama ya kadhi ikirudi itabidi tuwaombe wazee wetu wapiganie kurudiswa kwa mahakama za kimila/Kijadi amabzo kwa kweli zilikuwa ni msaada mkubwa sana .

Kule vijijini ambako mkono wa serrikali haufiki kirahisi hizi mahakama za kimila zilikuwa zina njia ya kuwaadhibu na kwashughulikia watu kama wachawi, watoto wa tukutu kwa kutoa adhabu kama kulima barabara, etc

Sasa serikali ilivuruga mahakama za kimila ndio maana siku hizi wazee wanauwa ovyo wakati kulikuwa na njia wananzego( wanavijiji) kudeal na mambo yao na kuyatua bila watu kupteza maisha

Mfano matatizo ya walenchari na walenchoka kule Mara, matatizo ya wazee shinyanga kuuwawa ovyo ni sababu vaccum iliyopo baada ya mfumo wa kimila kuvurugwa. na kutotambulika.

Kwa hiyo sambamba na mahakama ya kadhi tunaomba wzeee waanze kudai mahakama za mila jadi zao zitambuliwe.

Nawasilisha kwa mjadala wa umuhimu na madhara ya hizi mahakama za kijadi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom