Serikali irudishe hoteli ya Mikumi ijiendeshe kama awali

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
11,590
2,000
Mbuga ya hifadhi ya Mikumi na mbuga maarufu sana katika mkoa wa Morogoro na ipo masaa machache kutoka mjini Morogoro.

Kwa miaka mingi mbuga hiyo imeruhusu hoteli na kambi ndogondogo ambazo hazikidhi mahitaji halisi ya wananchi likiwemo suala la ajira.

Fedha inayotozwa kama ada ya malazi na chakula katika hoteli na kambi hizo inashia mifukoni mwa wamiliki wa hoteli hizo na nchi yetu kukosa pato halisi la taifa kupitia sekta ya utalii.

Ifuatayo ni orodha ya hoteli na kambi mbalimbali zilizomo ndani ya mbuga ya Mikumi:

Vuma Hills Tented Camp

Mahala ilipo: Vuma Hills

Uwezo/ Vyumba: 36

Mwaka iliyoanzishwa: 1999

Mmiliki: Galiano (mmiliki wa awali) - Fox Treks Company (Mmiliki wa sasa)

Foxes Tented Camp

Uwezo/ Vyumba: 24

Mwaka iliyoanzishwa: 2001

Mmiliki: Fox Trek Ltd

Mikumi (Kikoboga) Wildlife Camp

Eneo ilipo: Kikoboga

Uwezo/ vyumba beds

Mwaka iliyoanzishwa: 1967

Mmiliki: Oysterbay Hotels

Mikumi Wildlife Lodge

Mwaka iliyojengwa: 1970

Mmiliki: TTC ( Iliyokuwa Shirika la Utalii Tanzania)

Hali yake kwa sasa: Imefungwa

Rest house

Mahali ilipo mbugani: Kikoboga

Uwezo/ Vyumba: 8

Mmiliki: TANAPA

Hostel
Mahali ilipo mbugani: Kikoboga

Uwezo/ Vyumba: 60

Mmiliki: TANAPA

Lyambangali - Guest House

Eneo ilipo: Kikoboga

Uwezo/ Vyumba: 12

Mmiliki: TANAPA

Public Campsites

Uwezo/ Vyumba: 5

Campsites (No 1, 2, 3, 4 & Kitangawizi)

Mmiliki: TANAPA

Special Campsites

Uwezo/ Vyumba: 2

Campsite (Chogawale & Korongo la Muzimu)

Mmiliki: TANAPA

TANAPA ina wajibu wa kuhakikisha inaifufua hoteli ya Mikumi Wildlife Lodge ambayo itakuwa ni hoteli kubwa kati ya hizi hoteli zote zilizomo ndani ya mbuga hii.

Katika kulinda hadhi ya mbuga na sekta ya utalii katika nchi yetu hatuwezi kuona watu wachache wanahodhi baadhi ya sekta ambazo zinaweza kabisa kupanua wigo wa ajira na maendeleo ya watu wake.

TANAPA wanawajibika kuifufua Mikumi Wildlife Lodge na kuirudsha katika hadhi yake ya kimataifa ilokuwa nayo mwishoni mwa miaka ya 80.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom