Serikali irekebishe mifumo ya Kodi

The seer

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
407
690
Kwa mda mrefu baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa hawalipi kodi stahiki au wanapewa misamaha isiyotahili jambo ambalo limekuwa likikwamisha ustawi na maendeleo ya nchi.

Lakini kwa bahati nzuri serikali mpya imekuja na mikakati ya kukusanya kodi na kuzibiti ukwepaji kodi hili jambo jema lakini ni vema pia serikali iboreshe mazingira ya wafanyabiashara na kutatua changamoto za wafanyabiashara ili kuwaongezea uwezo wa kulipa kodi(taxable capacity) kwa sababu mifumo ya kodi ikiwa mibovu inasababisha tax evasion na tax avoidance.

Kwa mfano muundo wa kodi unatumika sana Tanzania ni masikini analipa zaidi kodi kuliko tajiri (regressive tax system) ndio maana gap kati ya masikini na matajiri linazidi kuongezeka.

Pia mfumo huu unasababisha unfair competition kwenye soko.

Kwa sasa inabidi tutumie progressive tax structure. Kipato kikiongezeka na kodi iongezeke.

Mifumo ya kodi inabidi iendane na mazingira yetu.

SERIKALI IBADILI MFUMO WA KODI KWA KUFUATA KANUNI ZIFUATAZO

1.RESTRICTED EXCEPTION - Misamaha ya kodi iwe maalum na kipindi Fulani tu kwa manufaa ya taifa. Kwa Tanzania misamaha mingi ya kodi haina tija kwa taifa.

2.CERTAIN - Kodi inatakiwa iwe wazi ni kiasi gani unalipa lini unalipa na wapi unalipa.Kodi nyingi Tanzania ziko complex kwa walipaji wengi ambayo hawana elimu mfano ukiuliza wafanyabiashara wengi wanalipa VAT lakini hawajui namna inacalculatiwa.

Kitengo cha elimu kwa mlipa kodi kitoe elimu ya kutosha kuhusu kodi mbalimbali na faida ya kulipa.

3. Understandable - Kodi lazima ieleweke kwa walipaji.Kodi nyingi za Tanzania hazieleweki ndio maana wafanyabiashara wanakwepa na zinaleta usumbufu.

4.EQUITABLE - Kodi zinapopangwa lazima zizingatie uwezo wa watu kulipa rushwa imetawala kiasi kwamba usipokuwa tayari kutoa rushwa unapangiwa kodi kubwa kuliko uwezo wako.

5.Broad basing - kodi lazima iwe wale wote wanaingiza vipato katika sekta mbalimbali za Uchumi walipe kodi.Kodi isiegemee upande mmoja na kundi Fulani tu.Kuna baadhi ya watumishi wa serikali wana misamaha ya kodi wengine hawana hii ni unfair.

Hizo ni baadhi tu KANUNI za KUFUATA wakati wa kupanga mifumo ya kodi. Tanzania misahama ya kodi ni tatizo kubwa sana.

Mfano makampuni ya mawasiliano yanalipa kodi kidogo ukilinganisha na faida wanayoyapata. Pia makamupni ya kuchimba madini, mahoteli makubwa ya kitalii kwenye mbuga za wanyama.

N.B PIA SERIKALI IANZISHE KODI KWA WAPANGISHAJI NYUMBA NA FREMU ZA BIASHARA.WAMEKUWA WAKIONGEZA KODI YA PANGO KIHORELA NA HAWALIPI KODI tofauli na ile kodi ya majengo.
 
Back
Top Bottom