Serikali ipo katika mpango wa kupitia utaratibu wa malipo kwa wanufaika wa mikopo ya Elimu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,744
2,000
Serikali imesema ipo katika mpango wa kupitia utaratibu wa malipo kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ili wapunguziwe mzigo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Machi 31, 2021 bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu Omari Kipanga alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum, Halima Mdee.

Mdee amehoji ni lini Serikali itapeleka bungeni mapendekezo ya sheria ili kuwaondolea mzigo mzito wanaobeba wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwani mpango huo umekuwa biashara.

Kwa mujibu wa Mdee Serikali inasema kuwa inawasaidia watoto wa masikini wakati inawaumiza kwa mlolongo wa madeni.

Naibu Waziri amesema tozo zilizotajwa na mbunge huyo hazina uhalisia kwani upo utaratibu mzuri wa namna ya ulipaji mikopo.

Swali la msingi liliulizwa na Atupele Mwakibete na likiibua mjadala mrefu bungeni ambapo wabunge wengi walitaka kuuliza maswali.

Chanzo: Mwananchi
 
samilakadunda

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
1,777
1,500
Na wapitie kweli hii imekuwa kero kwa vijana walio nufaika na mkopo huo, sasa imekuwa adhabu na mateso makali.
 
F M mbadange

Member
Feb 6, 2021
65
125
6% irudishwe.... 15% n ukandamizaji jamani........ Mtumishi hageuki.... Kakabwa vibaya... Nahayo manyongeza... Et kila mwez deni linakua kwa 1% na kila mwaka deni linakua kwa 6%.

hayo mateso baaaaa
😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Faru Tobbi

Member
Oct 29, 2018
62
125
Yani imekua biashara na chanzo cha mapato cha serikali haiwezekani iseme inasaidia watoto wa wanyonge kwa kuwasomesha elimu ya juu afu wanaacha kuwapa ajira baada ya mwaka wanapiga penati + ongezeko la thamani ya deni sasa kama sio kuumiza watoto wa masikini ni nini?
 
Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
1,301

Siku zote aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa
 
Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
1,301
2,000
Serikali imesema ipo katika mpango wa kupitia utaratibu wa malipo kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ili wapunguziwe mzigo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Machi 31, 2021 bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu Omari Kipanga alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum, Halima Mdee.

Mdee amehoji ni lini Serikali itapeleka bungeni mapendekezo ya sheria ili kuwaondolea mzigo mzito wanaobeba wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwani mpango huo umekuwa biashara.

Kwa mujibu wa Mdee Serikali inasema kuwa inawasaidia watoto wa masikini wakati inawaumiza kwa mlolongo wa madeni.

Naibu Waziri amesema tozo zilizotajwa na mbunge huyo hazina uhalisia kwani upo utaratibu mzuri wa namna ya ulipaji mikopo.

Swali la msingi liliulizwa na Atupele Mwakibete na likiibua mjadala mrefu bungeni ambapo wabunge wengi walitaka kuuliza maswali.

Chanzo: Mwananchi
" Ipo katika mpango wa kupitia"
Majibu ya kisiasa siku zote. Hii inamaana hata hawajaanza kupitia
 
Faru Tobbi

Member
Oct 29, 2018
62
125
Yaani ni hadi waulizwe, ina maana wao kama wizara hawajaona umuhimu wowote??
Ajabu kweli ndo maana mwanahistoria mmoja Denis Mpagaze ashawahi kutoa maoni kuwa ifike sehemu kama taifa tuwe na hitikadi na sera ya taifa ambapo vyama vya siasa ndo vitakua vinajinadi kwa kusema wataTUFIKISHAJE TUNAPOTAKA na sio kila chama kuwa na ilani yake kila awamu mambo yanabadilika badilika TU ajabu kweli.
 
Jostamas

Member
Jan 15, 2013
17
20
6% irudishwe.... 15% n ukandamizaji jamani........ Mtumishi hageuki.... Kakabwa vibaya... Nahayo manyongeza... Et kila mwez deni linakua kwa 1% na kila mwaka deni linakua kwa 6%.

hayo mateso baaaaa
😭😭😭😭😭😭😭😭
Dah! Wafanyakazi wa uma! Kila akigeuka ni kibano! Nadhan sab wanaopitisha sheria bungeni( wabunge), wao hua hawakatwi ktk malipo yao, ndio maana hata kikokotoo kinapitishwa tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom