Serikali ipige marufuku uagizaji magari kwa miaka mitano tu, tuone kama havianzishwi viwanda

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,052
40,715
Kuna wakati huwa nawaza, hivi inakuwaje demand ipo ya kutosha lakini bado tunaagiza bidhaa nje. Mfano demand ya sukari ipo kubwa, ardhi kwa ajili ya mashamba ya miwa ipo unlimited na watu wenye uhitaji wa ajira za hicho kilimo wapo, ni kiasi cha kulima tu; ila utasikia sukari haitoshi tunaagiza nje, sasa huu ni uchawi wa wapi huu?

Hivi kwa mfano serikali kwa hasira ikapiga marufuku uagizaji wa magari toka nje kwa miaka mitano au 20 kabisa, hatutapata wawekezaji wa kuzalisha au walau ku-assemble tu magari hapa nchini?

Hebu tufumbe macho na tujaribu tuone itakuwaje, ila kitafutwe chanzo mbadala cha kodi maana haya magari ndio yanategemewa kubamizwa kodi kubwa bandarini.
=============================
Hii ndio Benz ya kwanza iliyotengenezwa mwaka 1886.
vintage-and-prestige.1497259025.47047.jpg

Na sasa wako hapa..
images.jpeg.jpg

===============================
Ghana kuna mchungaji anaitwa Kantanka, anabuni na kutengeneza engine, chassis na body za magari na kuziunganisha yeye mwenyewe kwenye workshop zake hapo Ghana, na serikali inamuunga mkono kwa kununua magari yake aina ya Kantanka V8, lione mwenyewe..
Kantanka-suv-made-in-Ghana.png

________________________________
IG: @marble_na_granite
 
Kwa kweli nami pia huwa najiuliza sana hili la sukari
Kama wazungu walikuwa wanategemea sana miwa kwa ajili ya sukari na kwa kuwa miwa haivumilii ardhi yao
Wakaja na mbadala wa kulima Sugar beet ambayo sijui kwa kinyumbani
Lakini wamefanikisha na wanalima sana kwa sasa

Yupo Mganda mmoja ambaye amekuwa inspired na walimaji wa Anglia na anataka kuanza kulima Uganda
Uzuri wa hili zao unaweza vuna mara mbili kwa mwaka na inatengeneza sukari nzuri sana na kwa wingi zaidi
Sijui tunashindwa nini kufuatilia na kuleta hilo zao kwetu
IMG_0824.JPG
 
Juzi mmepewa FOTON car za msaada, mara wachina nao hao magari, oooh sorry nyumbu nao hao...

Kagera sugar.
Mtibwa Sugar.
TPC Sugar.

Njoo kwa Mo sugar from Brazil.
>>Wewe unadhani wapi tunaweza kuwin kwa haraka..?
 
..Kuzuiliwa kwa uagizaji wa magari kuna uhusiano upi na kujenga viwanda. Badili title yako maana magari umenganisha ma matatizo ya sukari wapi na wapi?
 
Watanzania tunathamini vya nje kuliko vya nyumbani. Tunaamini vya nje ni bora kuliko vyetu. Wawekezaji wanakosa soko la uhakika. TUBADILIKE VYAKWETU KWANZA.
 
... ndugu purchasing power ya mtanzania unaijua? Ni watanzania wangapi wana uwezo wa kununua brand new cars? Ni watanzania wepi hao wenye uwezo wa kununua magari mapya kwa USD 25,000 kabla ya kodi na kuya-dump after not more than 5 yrs?

Hivyo vimtumba vya USD 650 to USD 2500 vilivyojaa barabarani watanzania wanavyoagiza Japan tena kwa mikopo ya hadi 7yrs kutokana na mfumo mbovu wa public transport kwenye miji yetu ndivyo vinakutia kiburi kudhani viwanda vya magari vinaweza kujengwa nchini?

Hakuna mwekezaji wa viwanda vya magari atakayewekeza kwenye soko maskini namna hii potelea mbali other factors including siasa zisizotabirika, kodi za hovyo, n.k.
 
Demand is the mother of all inventions, watu wakihitaji magari halafu uagizaji umezuiwa, unadhani nn kitatokea? Si tutanunua hata basi toka nyumbu
 
... ndugu purchasing power ya mtanzania unaijua? Ni watanzania wangapi wana uwezo wa kununua brand new cars? Ni watanzania wepi hao wenye uwezo wa kununua magari mapya kwa USD 25,000 kabla ya kodi na kuya-dump after not more than 5 yrs?

Hivyo vimtumba vya USD 650 to USD 2500 vilivyojaa barabarani watanzania wanavyoagiza Japan tena kwa mikopo ya hadi 7yrs kutokana na mfumo mbovu wa public transport kwenye miji yetu ndivyo vinakutia kiburi kudhani viwanda vya magari vinaweza kujengwa nchini?

Hakuna mwekezaji wa viwanda vya magari atakayewekeza kwenye soko maskini namna hii potelea mbali other factors including siasa zisizotabirika, kodi za hovyo, n.k.
Ghana kuna mchungaji mzalendo wa kule kaanzisha Kantaka motors
 
Watanzania tunathamini vya nje kuliko vya nyumbani. Tunaamini vya nje ni bora kuliko vyetu. Wawekezaji wanakosa soko la uhakika. TUBADILIKE VYAKWETU KWANZA.
Guilty as charged! Mm kwa TBS ya macho yangu naona hivyo. Nilimnunulia nwanangu viatu vya shule vilivyotengenezwa nyumbani, alivyorudi nyumbani siku ya kwanza tu socks zote kwa chini zimekuwa za bluu ambayo ni rangi iliyopo kwenye carpet ya hivyo viatu, haitoki hata kwa jik. Niliowanunulia viatu vya fitkidz( imported) hakuna shida.
 
Sio kila kitu cha kujaribu, hayo ya kujaribu jaribu ndio yametufikisha hapa
Kuna wakati huwa nawaza, hivi inakuwaje demand ipo ya kutosha lakini bado tunaagiza bidhaa nje. Mfano demand ya sukari ipo kubwa, ardhi kwa ajili ya mashamba ya miwa ipo unlimited na watu wenye uhitaji wa ajira za hicho kilimo wapo, ni kiasi cha kulima tu; ila utasikia sukari haitoshi tunaagiza nje, sasa huu ni uchawi wa wapi huu?

Hivi kwa mfano serikali kwa hasira ikapiga marufuku uagizaji wa magari toka nje kwa miaka mitano au 20 kabisa, hatutapata wawekezaji wa kuzalisha au walau ku-assemble tu magari hapa nchini?

Hebu tufumbe macho na tujaribu tuone itakuwaje, ila kitafutwe chanzo mbadala cha kodi maana haya magari ndio yanategemewa kubamizwa kodi kubwa bandarini.
 
Kuna wakati huwa nawaza, hivi inakuwaje demand ipo ya kutosha lakini bado tunaagiza bidhaa nje. Mfano demand ya sukari ipo kubwa, ardhi kwa ajili ya mashamba ya miwa ipo unlimited na watu wenye uhitaji wa ajira za hicho kilimo wapo, ni kiasi cha kulima tu; ila utasikia sukari haitoshi tunaagiza nje, sasa huu ni uchawi wa wapi huu?

Hivi kwa mfano serikali kwa hasira ikapiga marufuku uagizaji wa magari toka nje kwa miaka mitano au 20 kabisa, hatutapata wawekezaji wa kuzalisha au walau ku-assemble tu magari hapa nchini?

Hebu tufumbe macho na tujaribu tuone itakuwaje, ila kitafutwe chanzo mbadala cha kodi maana haya magari ndio yanategemewa kubamizwa kodi kubwa bandarini.

Haya ya kununua milion 6 kutoka japan yenye miaka zaidi ya kumi yanakushinda utaweza zero kilomiter.
 
Hebu ngojeni kidogo nami niagize kamkoko ndo mfunge mipaka, kwanza mtuambie SUTI za mheshimiwa zinatoka nchi gani.... sisi zetu ni malighafi tu.
 
Haya ya kununua milion 6 kutoka japan yenye miaka zaidi ya kumi yanakushinda utaweza zero kilomiter.
Hata ikibidi tununue yale makopo toka DIT au ile mikangafu toka nyumbu, potelea mbali, lazima tuanze chini ndio twende juu.., otherwise tunazidi kujidumaza wenyewe kiteknolojia,hata wao ukiangalia gari za mwanzo walizokuwa wanatengeneza zilikuwa kama baiskeli tu za miguu minne..
 
Ghana nao wanatengeneza magari yao wenyewe.., tutabaki sisi tu hapa duniani ndio hatujielewi kwenye masuala ya teknolojia..
Kantanka-suv-made-in-Ghana.png
 
Back
Top Bottom