Serikali ipige marufuku Mahindi kuuzwa nje

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,536
2,000
Ni ukweli usio na shaka kuwa mwaka huu kunaweza kukawa na baa la njaa hapa kwetu Tanzania.

Mvua hakuzinyesha za kutosha na maeneo mengi nchini mavuno ya nafaka yatakuwa kidogo sana. Mikoa yote ya kanda ya ziwa hali ni mbaya, hasa hasa Mara na Mwanza.
Mfano Geita kwa sasa debe moja la mahindi ni Tsh 15000-20000.

Mchele pia bei yake imepaa sana, imefikia hadi 80000 kwa gunia la mpunga moja, hapa ni kwa Geita.

Serikali ifanye utafiti wa hali ya chakula nchini, ikibidi izuie kuuzwa kwa mazao ya chakula nje ya nchi hadi hapo itakapo ona hali ya mavuno iko vema.

Hayo ni maoni yangu na ka Elimu uchwara kangu, wasomi na wenye dhamani walitizame kisomi, waache Civics katika hili.
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,255
2,000
Huna hoja ww, mtu alime shamba kwa gharama zake bila msaada wa serekali ikifika saa ya kuuza utupangie bei. Mbona hao wakulima wakiingia hasara hamuwafidii? Nendeni na nyie mkalime sio kukaa ofisini njaa ikiingia muanze kupangia waliohenyeka shambani mahali pa kuuza.
Hapo sasa.
Kulima alime mwengine kutumia watolee macho.

Wakati nyanya zilipooza hakuna alofidia hasara
 
Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,307
2,000
Huna hoja ww, mtu alime shamba kwa gharama zake bila msaada wa serekali ikifika saa ya kuuza utupangie bei. Mbona hao wakulima wakiingia hasara hamuwafidii? Nendeni na nyie mkalime sio kukaa ofisini njaa ikiingia muanze kupangia waliohenyeka shambani mahali pa kuuza.
wewe uko nchi gani serikali ilishapiga marufuku tangu mwezi wa saba
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,650
2,000
Ni ukweli usio na shaka kuwa mwaka huu kunaweza kukawa na baa la njaa hapa kwetu Tanzania.

Mvua hakuzinyesha za kutosha na maeneo mengi nchini mavuno ya nafaka yatakuwa kidogo sana. Mikoa yote ya kanda ya ziwa hali ni mbaya, hasa hasa Mara na Mwanza.
Mfano Geita kwa sasa debe moja la mahindi ni Tsh 15000-20000.

Mchele pia bei yake imepaa sana, imefikia hadi 80000 kwa gunia la mpunga moja, hapa ni kwa Geita.

Serikali ifanye utafiti wa hali ya chakula nchini, ikibidi izuie kuuzwa kwa mazao ya chakula nje ya nchi hadi hapo itakapo ona hali ya mavuno iko vema.

Hayo ni maoni yangu na ka Elimu uchwara kangu, wasomi na wenye dhamani walitizame kisomi, waache Civics katika hili.
Mkuu, usisahau mkulima wa mahindi na mpunga naye anahitaji hela kama yule wa korosho wa msimu huu.
Labda useme serikali inunue bei kubwa kuliko walanguzi kitu ambacho si rahisi
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
10,876
2,000
Huyu ni mfanyabiashara wa nafaka Geita, anataka bei ipungue kwa wakulima yeye aendelee kufaidi. Unajua gharama za kilimo mpaka uishauri serikali izuie watu kuuza mazao yao kuliko na bei yenye faida?
 
kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,595
2,000
mbona wafugaji hawaambiwi wasiuze nje? na hawana limit afuge wangapi? kwanini mkulima anaonewa? na anaambiwa asiuze bidhaa yake nje, kama ni hivyo bhas na korosho pia zisiuzwe nje hadi ng'ombe, samaki na vinginevyo.., tuone kama nchi itakua ya viwanda
 
Idofi

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
2,012
2,000
hao wakulima mliwasaidia kwa chochote mpaka mnataka kupiga marufuku? pembejeo bei juu, mkulima hapewi ruzuku anatumia nguvu na rasirimali zake akivuna mnampangia masharti
 
Entim

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
3,926
2,000
Ni ukweli usio na shaka kuwa mwaka huu kunaweza kukawa na baa la njaa hapa kwetu Tanzania.

Mvua hakuzinyesha za kutosha na maeneo mengi nchini mavuno ya nafaka yatakuwa kidogo sana. Mikoa yote ya kanda ya ziwa hali ni mbaya, hasa hasa Mara na Mwanza.
Mfano Geita kwa sasa debe moja la mahindi ni Tsh 15000-20000.

Mchele pia bei yake imepaa sana, imefikia hadi 80000 kwa gunia la mpunga moja, hapa ni kwa Geita.

Serikali ifanye utafiti wa hali ya chakula nchini, ikibidi izuie kuuzwa kwa mazao ya chakula nje ya nchi hadi hapo itakapo ona hali ya mavuno iko vema.

Hayo ni maoni yangu na ka Elimu uchwara kangu, wasomi na wenye dhamani walitizame kisomi, waache Civics katika hili.
Ahaa. Baba alichukua mkopo bank akazazalisha mpunga gunia 900 huko Nyehunge Sengelema na mahindi gunia 450 ameweka store kwa lengo la kuuza Uganda na Kenya early January 2017.
Leo hii umzuie asiuze nje, kisa kuna njaa nchini. Alizalisha kwa ajili ya kulisha watu? Haya ndo mapinduzi ya kilimo na viwanda? Utamsaidia baba kurejesha mkopo? Mwakani atakopesheka tena? CRDB wakimnyima mkopo msimu ujao utawalaumu?
Tukihitimisha kwa kusema ukimbizwe milembe utakataa?
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
12,053
2,000
kuzuia kuuza mazao ya chakula nje kila serikali inapojisikia ndiyo kunaleta njaa. watu wenye mitaji hawapendi ujinga, wanaenda kulima vitunguu, vitunguu saumu, nanasi, tikiti, tangawizi, bamia, nyanya chungu, viazi mviringo, pilipili mbuzi, pilipili hoho, miti, wanajenga nyumba za kupangisha na zinazobaki wanakunywa balimi. wazee ndiyo wamebaki kulima mahindi.
 
Pierreeppah

JF-Expert Member
Feb 2, 2014
1,543
2,000
Wasiolima ni wengi na ndio wanapiga kelele ili waendelee kumlangua mkulima miaka na miaka..... Ukiangalia kazi ya kulima mpunga ilivongumu hata gunia lake ilitakiwa iwe sh laki na nusu hivi
 
MR MAJANGA

JF-Expert Member
Oct 4, 2014
2,328
2,000
Ni ukweli usio na shaka kuwa mwaka huu kunaweza kukawa na baa la njaa hapa kwetu Tanzania.

Mvua hakuzinyesha za kutosha na maeneo mengi nchini mavuno ya nafaka yatakuwa kidogo sana. Mikoa yote ya kanda ya ziwa hali ni mbaya, hasa hasa Mara na Mwanza.
Mfano Geita kwa sasa debe moja la mahindi ni Tsh 15000-20000.

Mchele pia bei yake imepaa sana, imefikia hadi 80000 kwa gunia la mpunga moja, hapa ni kwa Geita.

Serikali ifanye utafiti wa hali ya chakula nchini, ikibidi izuie kuuzwa kwa mazao ya chakula nje ya nchi hadi hapo itakapo ona hali ya mavuno iko vema.

Hayo ni maoni yangu na ka Elimu uchwara kangu, wasomi na wenye dhamani walitizame kisomi, waache Civics katika hili.

Mkuu kwani hayo mazao lini yameruhusiwa kuuzwa nje ya nchi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom