Serikali ipige marufuku dua na maombi kwenye mikutano ya kisiasa!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,502
2,046
Pamoja na kwamba mimi ni mwamini Mungu lakini naona huu utaratibu ni kama unatuvuruga tu wananchi, kwani unaondoa dhana ya kutenganisha siasa na dini.

Isitoshe mambo mengi ya siasa yamejaa uongo uzushi jazba na visasi mambo ambayo ni kinyume kabisa na maombi/dua/sala za viongozi wa dini.
 
kweli kabisa, maombi ya jumla hufanyika misikitini na makanisani na yale ya ziada hufanyika nyumbani na sirini,
tukija kwenye majukwa ni political activities acha zifanyike siasa tu, dua, sala, maombi vinakosa maana, kwa kuwa maombi hugeuka kampeni.

wanasiasa wenyewe waongo, wanafki , kuwaombea ni kulitaja tu bure jina la muumba

Back
Top Bottom