Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Baada ya kuwa na mvutano kuhusu nauli za mabasi ya DART huku wananchi wakisema ni kubwa sana na hawawezi kumudu na upande wa Kampuni wakidai ni ngumu kuendesha huwo mradi kwa nauli ya shilingi 500 jambo ambalo mimi binafsi nakubaliana nawo kwamba haingilii akilini utoe basi lenye uwezo wa kubeba abiria 150 ktk Kimara mpaka Kivukoni huu ni umbali ya zaidi ya kilometa 10 kwa shilingi 500, hii nauli hailipi kabisa na haiwezi kuifanya hii Kampuni ipate faida ili ilipe wafanyakzi vizuri, itengeneze miundo mbinu ya basi pindi iharibikapo, kununua mabasi mengine pindi haya yatakapochakaa na vile vile kuweza kulipa kodi Serikalini
Hivyo basi kwa kuwa pande zote mbili wana hoja ya maana nashauri wananchi walipe nauli wanayoitaka halafu Serikali ifidie pengo lililiobakia kufikia kiwango wanachopendekeza Kampuni na Serikali iongeze asilimia fulani kwenye bei ya mafuta (petroli/diesel) na fedha inayopatikana ndiyo itumike kufidia hilo pengo!
Kinyume na hapo kama Serikali ikitaka kulamizisha hiyo nauli ya 400 au 500 huu mradi utakufa baada ya miaka 2, utakuwa kama mradi wa Raisi Mwinyi wa mabasi ya Wanafunzi kwani hawataweza kujiendesha kwa nauli hiyo!

Last edited: