Serikali iondoe vibanda vilivyo Mbele ya Biashara nyingine Kariakoo, hali mbaya

Hao watu ni wengi, na tayari maisha yao yapo hapo.
Inatakiwa kabla ya kuwaondoa watafutiwe eneo ambalo watapata wateja kama ilivyo maeneo waliyopo sasa. Kusema huruma haihitajiki kisa ni maendeleo ya nchi tutakuwa tunajaribu kufufua ukatili ambao tunajitahidi kuuzika.
Hao wana familia, kuwaondoa hapo ni sawa na kuanza kuwalaza njaa.
Hebu jaribu wewe ulale njaa kabla haujapendekeza mwenzako alale njaa. Tuache ukatili.
Walakini hayo maduka hayajazibwa na hivyo vibanda kiviile,, mtu akitaka kuingia dukani mbona anaingia tu??
 
Hii nchi sijui ushamba tutaacha lini. Machinga wanalelewa Sana na zaidi ya kuharibu biashara za watu, wanachafua taswira ya mji.

Serikali waache uoga!
Ni binadamu wenzako wale ndugu yangu. Nao wanahangaika kutafuta chochote ili familia zao zipate chakula. Wana vitoto vinasoma.
Au haujali chochote zaidi ya taswira?
 
Wenzako wanafunga maduka mzigo wanagawa kwa wamachinga kadhaa kila siku jioni wanaleta hesabu. Unaokoka kulipa kodi za pango huku mzigo unauzika kama kawa.
 
Hakuna wakuthubutu kuwatoa hao,
Tabia hujenga mazoea na mazoea hujenga sheria,
Huku wamachinga, huku bodaboda huku bajajai, utapitia wapi?
 
Naona kwa hali hii baada ya miaka 20 kariakoo itakuwa ya machinga peke yao
Wafanyabiashara wengine watakimbia na kwenda maeneo mengine
 
Sasa tukiendelea hivi miaka mitano itakuwaje?..yaani ni bora watu wastopishwe kwa sasa,hili la kufanya biashara hadi barabarani sio sawa kabisa kwa jamii iliyostaarabika.
mkuuu hata ulaya kuna machinga na watu wanafanya biashara pembeni mwa barabara ustarabu unaoutaka ni upi
 
Machinga ni Bomu linalotengenezwa kinachosubiriwa ni kulipuka. Ni heri serikali iamue sasa kuliko kuendelea kusubiri. Kwa kweli hali ni mbaya. Barabara za mitaa kwa sasa ni kama hazipo Karakoo.
 
Waliokuwa mbele ya kituo Cha mabasi mbezi Luis wameondoka wenyewe ...saiv kumekuwa kweupe na kupendeza...miturubai na mimbaombao kwao kweli inaharibu taswira..bado na mlimani City ....ubungo mataa saiv Safi...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hili kundi lilitumika kama mtaji wa siasa, limekuwa ni kero baada ya kuaribu swala zima la mipango miji. Watu wamehamia mijini kwani sehemu yoyote waweka biashara, hakuna maegesho. Turudi kwenye taratibu.
 
Hao watu ni wengi, na tayari maisha yao yapo hapo.
Inatakiwa kabla ya kuwaondoa watafutiwe eneo ambalo watapata wateja kama ilivyo maeneo waliyopo sasa. Kusema huruma haihitajiki kisa ni maendeleo ya nchi tutakuwa tunajaribu kufufua ukatili ambao tunajitahidi kuuzika.
Hao wana familia, kuwaondoa hapo ni sawa na kuanza kuwalaza njaa.
Hebu jaribu wewe ulale njaa kabla haujapendekeza mwenzako alale njaa. Tuache ukatili.
Walakini hayo maduka hayajazibwa na hivyo vibanda kiviile,, mtu akitaka kuingia dukani mbona anaingia tu??
Pathetic fool
 
Waza pia vibaka, majambazi, makahaba, majangili, mafisadi, wahamiaji haramu, wauza gongo, walima bangi, wauza madawa ya kulevya, walima mirungi na matapeli, wote hao ni wengi, wana ndugu wanaowategemea, hivyo nao waachwe kama wamachinga?

Nchi iliyokosa utaratibu ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom