Serikali iondoe ulazima kwenye bima za magari, itilie mkazo bima inayojali afya ya mtu

Mzalendo39

JF-Expert Member
Apr 17, 2015
695
1,000
Ni mwaka wangu wa tano nimekuwa nikikata bima kwa ajili ya gari yangu na kwa kipindi chote hicho sijawahi kupata ajali ya aina yoyote, Zaidi ya kuyanufaisha makampuni ya bima. Bima yenyewe haitumiki hata kughalimia service ya gari.

Kinachonishangaza ni kwanini Serikali iweke ulazima wa bima kwenye magari na vifaa vya moto, maana vifaa hivyo vikisababisha ajali bima inaangalia kifaa na si afya binadamu aliyasababishwa ajali, majeruhi na hata kuhudumia mazishi yanayotoakana na vifo.

Nashauri Serikali ipitie upya sheria inayolazima matumizi ya bima kwenye vyombo vya moto na iweke ulazima katika bima ya afya ya inayohudumia afya na uhai wa mtu.

Maisha ya binadamu ni muhimu kuliko chombo cha moto.

IMG-20210309-WA0021.jpg
IMG-20210111-WA0012.jpg

IMG-20210309-WA0028.jpg
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,951
2,000
Kwa jinsi tulivyo, subiri kuambiwa "hata ulaya hawafanyi hivyo"
 
legend Babushka

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
522
1,000
Naunga mkono hoja.

Inakuwa vigumu kueleweka kuwa chombo kilichopo barabarani kina ulazima wa bima ila anayekiendesha hana bima.
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
45,539
2,000
Bima ya lazima kwenye gari ni third party ambayo inamlinda yule utakaemsababishia madhara kwenye ajali.
Hayo ya fidia yote yapo kwenye bima shida ni jinsi tunavyoendesha mambo yetu,ila bima kama bima na sheria zake ziko vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Munambefu

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
1,822
2,000
Kwa hiyo Mkuu bima ikiondolewa ukimgonga mtu ukamsababishia ulemavu wa kudumu utaweza kumlipa?

Wewe ungesema bima ya Afya itiliwe mkazo Kama bima ya vyombo vya moto lakini kusema iondolewe sio fikra pana
 
Mzalendo39

JF-Expert Member
Apr 17, 2015
695
1,000
Kwa hiyo Mkuu bima ikiondolewa ukimgonga mtu ukamsababishia ulemavu wa kudumu utaweza kumlipa?

Wewe ungesema bima ya Afya itiliwe mkazo Kama bima ya vyombo vya moto lakini kusema iondolewe sio fikra pana
Sijasehema iondolewa napendekeza Serikali iiondolee ulazima' makampuni ya bima wanaonufaika tu fedha zetu
 
MissM4C

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,568
2,000
Kaka usiseme hivyo, mbona hata bima za afya za kawaoda watu hukata miaka bila matibabu(kuumwa) nao wanaibiwa?
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,578
2,000
Bima ya gari yako si lazima. Ukitaka unaweza kukatia gari lako na pia bima ya maisha kwako mwenyewe.

Bima ya lazima kwa magari ni third party ambayo inasaidia kulipa fidia endapo gari yako itasababisha damages kwa watu au magari mengine. Ukishaelewa dhana ya bima, sio vigumu kuona umuhimu wake. Unalipa 118,000 kwa mwaka, lakini unaweza sababisha hasara ya mamilioni.....
 
Coaster2015

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
2,528

Tujitahidi kuwa tunajenga hoja ambazo kimsiingi zaweza kutusaidia wenyewe, nianavyo mimi mleta mada ana hoja ya msingi kutokana na ukweli kwamba bima tunazolipa za magari tunafaidisha makampuni ya bima, hawa mbwa weupe wanaokaa barabarani wangeacha kuwa wanatusumbua kwamba ikiisha tu ukate hapohapo, wangeweza kuwa tu wanawakumbusha watu kwamba nenda ukakate bima yako imeisha sio ukiwakuta tu wanakupiga faini huo ni ushenzi, kwani kuwa nayo na kutokuwa nayo hakuwezi kusaidia kwa lolote kuzuia ajarii barabarani
 
Hana. Ni sawa tu na bima ya afya. Unaweza kuwa nayo lakini usiitumie au usiumwe mwaka mzima. Nakumbuka kuna vyuo na shule na hata kazi ni sharti kuwa na bima ya afya. Lakini wewe usipoumwa, ujue kuna wenzio wameumwa na kulipiwa gharama za matibabu mara 100 zaidi ya premium waliyolipa. Maana yake nini? Wewe na mimi ambao tulikata bima ya matibabu lakini hutujaumwa mwaka mzima, kimsingi tumewasaidia/tumewachangia hao walioumwa na kulipiwa gharama kubwa na bima. Huo ndio msingi wa bima....kukusanya pamoja fedha za wengi na kusaidia wachache na kinachobakia ni faida ya kampuni ya bima.

Magari ni vivyo hivyo. Wewe, mimi na wengine 8 tumekata bima (say jumla 1,180,000 TP) kwa mwaka huu. Wewe ndani ya mwaka huu kwa bahati mbaya umemgonga jamaa (kati ya hao 8) ana range rover lake....kulitengeza inahitajika 1,500,000. Sisi wengine wote 9 hatujamsababishia hasara mtu yoyote mwaka mzima. Bima inalipia mategenezo ya range rover lakini kimsingi ni sisi 9 ambao hatujasababisha ajali yoyote ndio tumekuchangia na bima hapo italazimika kujazia hiyo diff (1.5 less 1.18) na kama wateja wake ni sisi 10 tu, maana yake kapata hasara. Kusingekuwa na bima, wewe ungelazimika kutoa 1.5m kutengeneza range la watu ....lakini kwa kuwepo bima ni kama umelip 118,000 tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom