Serikali inunue magari katika majimbo kwa ajili ya wabunge

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Hili suala la kuwapa wabunge mamilioni ya fedha kwa ajili ya wabunge lifutwe kabisa.

Miaka ya utawala wa awamu ya kwanza na pili serikali ilikuwa inatoa gari kwa kila jimbo kwa matumizi ya mbunge na kipindi ubunge unapoisha gari linabaki kwenye jimbo kwa matumizi ya mbunge anayefuata.
 
Ndugu yangu Bowie mawazo uliyonayo leo ni ya Dunia iliyopita (Socialism). Yalikuwa ni mawazo mazuri kwa kipindi hicho ambacho kweli Wabunge walikuwa ni watumishi wa umma.

Na wala kazi ya Ubunge haikushindaniwa kama leo, na wananchi walichagua viongozi kwa kuangalia taaluma, uadilifu na uwezo wa kiuongozi ( Leaders were elected on merit).

Leo mtu yeyote kuanzia mganga wa kienyeji ,kahaba na yeyote umdhaniae anaweza kutaka na kuchaguliwa na wapiga kura kuwa Mbunge ilimradi tu anaweza kuwanunua wapiga kura hao!

Sasa Ndugu Bowie mtu kama huyo anatumia milioni 300 kuupata Ubunge utamwambia atembelee Mandolin (Land Rover 109) au Mahindra?

Tuko kwenye Dunia ambayo kila kitu ni fursa ikiwemo na Ubunge huo. Ndani ya Dunia ya leo (Globalized world economy) kila mtu anataka kumiliki kitu.

Hivyo ndugu yangu you better refine your thoughts!
 
Ndugu yangu Bowie mawazo uliyonayo leo ni ya Dunia iliyopita ( Socialism). Yalikuwa ni mawazo mazuri kwa kipindi hicho ambacho kweli Wabunge walikuwa ni watumishi wa umma...
Mkuu nakushangaa sana kwa kukusikia mtu anatumia million 300 kuupata ubunge. Nitaafurahi sana kuona huyo mbunge akitumia mshahara wake kununua hilo gari badala ya kutupa mzigo walipa kodi
 
Achana na Ushauri wako. Wapewe Hera yao maana ni utaratibu uliopo/ Wamepambana sana Kupata Nafasi hhizo.
Kwamba wamepambana sana kupata nafasi hiyo isiwe sababu ya kupewa fedha ili kupunguza hayo makali ya upambanaji. Walipokuwa wakituomba kula walisema waziwazi kwamba wao watakuwa watumishi wetu.

Sasa mtumishi gani huyo anayemtaka bosi wake ajinyime ili yeye anufaike zaidi? Utaratibu utamtumikia tu pale bosi atakapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kwa sasa nguvu zetu zote tunazielekeza kwenye miradi ya JNHEP na SGR.
 
Mkuu nakushangaa sana kwa kukusikia mtu anatumia million 300 kuupata ubunge. Nitaafurahi sana kuona huyo mbunge akitumia mshahara wake kununua hilo gari badala ya kutupa mzigo walipa kodi
Hizo fedha wanazotumia kununua magari ni mikopo kutokana na mapato yao kwa kazi ya Ubunge hivyo si sahihi kusema huo ni mzigo kwa Serikali.

Nadhani hujapata taarifa za kutosha kuhusu hilo suala la magari kwa Wabunge,ebu jaribu kulifuatilia vizuri.

Ndio sababu si Wabunge wote uchukua mikopo kwa ajili ya magari kwa maana wengine tayari wanayo magari hayo.
 
Acheni uchawi, cha msingi kila mtu akabidhiwe hio 90M akatafute chombo chake 😝😝😝
 
Mkuu nakushangaa sana kwa kukusikia mtu anatumia million 300 kuupata ubunge. Nitaafurahi sana kuona huyo mbunge akitumia mshahara wake kununua hilo gari badala ya kutupa mzigo walipa kodi
Kwani wabunge wanatumia hela ya nani kununua magari?
 
Ndugu yangu Bowie mawazo uliyonayo leo ni ya Dunia iliyopita (Socialism). Yalikuwa ni mawazo mazuri kwa kipindi hicho ambacho kweli Wabunge walikuwa ni watumishi wa umma....
Duh! Kumbe ndiyo maana mnakimbizana kwa waganga huko? Ukishaona hali ipo hivyo, bado unashabikia tu.
 
Moja ya sababu kuu ya uamuzi wa kuwakopesha pesa badala ya kuwapa magari ya kutumia ilikuwa ni kukabiliana na gharama kubwa za matengenezo na matumizi mabaya ya magari hayo. Kwa wenye uzoefu na utunzaji wa magari ya umma/serikali, wanajua gharama "za kifisadi" zinazotumika katika huduma (service) na matengenezo ya magari hayo. Aidha, uwajibikaji katika matumizi ndio hakuna kabisa.

Si ajabu gharama (service na repair) ya gari la Mbunge kwa miaka mitano zikazidi hata TShs milioni 200 na gari kuhitaji kubadilishwa. Bora apewe hizo milioni 90 akawe muangalifu na matumizi yake. Kwanza si wanakopeshwa? Halafu milioni 90 (nasikia 50 hivi sasa) ni hela ya kawaida sana kwa gari la kikazi (field vehicle). Linganisha na kuwanunulia Toyota LC GX/VX mpya (TShs >100 mil tax free).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom