Serikali inunue korosho yote kama tangazo la Mkuu lilivyotoka kisha kwa yule atakaeshindwa kuonesha shamba lake Serikali ikusanye ushuru

Liuumi

Senior Member
Jun 17, 2015
164
164
Kwanza kabisa natanguliza shukrani zangu za dhati kwa Muumba wa Mbingu na Ardhi, kwa kutuamsha salama siku nyingine tena,

Jana nilimsikia Mkuu wa Nchi akisema kuwa wapo mawaziri na wafanya biashara walikuwa wananunua korosho kwa wakulima kwa bei ya chini kabisa kwa kauli yake anasema “wapo watu wananunua korosho wakati iko maua Shambani kwa bei ya shilling 200@ 1kg” kama ni kweli walikuwa hawa watu hawa watendei haki wakulima

Lakini pia Mkuu alisema wale ambao wanazo korosho na hawana mikorosho “hawa hakuna kulipwa alisema taifisheni korosho zao” hapa akimaanisha kama umenunua korosho ziko shambani au baada ya mkulima kumletea CHOMA CHOMA ili tu hajikimu wakati anasubiri wafike wanunuzi wakubwa apeleke ghalani kwa bei kubwa kuliko ya CHOMA CHOMA, wakati huo CHOMA CHOMA ni mfanya biashara sio mkulima

Neno la Mkuu wa nchi akitamka huwa amri Sawa lakini ingekuwaje kama angewaangalia hawa wafanya Biashara wadogo au CHOMA CHOMA kwa umaarufu wao katika mtazamo wa BIASHARA kwa maana baada ya kuchukua korosho bila kuwalipa kwa nini SERIKALI usiwalipe hawa kisha ukiwatoza USHURU (TAX) kuliko ili la kuwanyang’anya KOROSHO zao ambazo zilinunuliwa na Pesa ambayo ilikuwa MITAJI Yao serikali haioni inazidisha Maisha kuwa magumu kwa wananchi wake

Wazo langu kwa serikali inunue korosho zote kama tangazo la Mkuu lilivyotoka kisha kila yule atakae shindwa kuonyesha shamba lake la MIKOROSHO serikali Ikusanye USHURU(KODI) kutoka kwao
 
Back
Top Bottom