Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,110
- 2,736
Wanajukwaa, nadhani serikali yetu inabidi iangalie kwa umakini mkubwa haya mambo ya ukatili ndani ya hii nchi. Kuna mambo ya ajabu mno.
Mara kwa mara naenda Mikocheni kumtembelea mchumba wangu anayeishi Mikocheni Baraka Plaza Apartments, na mara nyingi nawakuta vijana wale wale waigwa lindoni. ILa leo ilikuwa tofauti kidogo maana mmoja alikuwa akibubujika machozi. Nililazimika kuingiza gari na kurudi kutaka kujua kulikoni, ndipo nikagundua kwamba, Huyu aliyekuwa akilia alifukuzwa kazi.
Sababu ya kufukuzwa kazi, ni kwa sababu aliomba mshahara wake. Huu ni wezi wa saba tarehe 20, lakini hadi leo hawajalipwa mishahara yao toka mwezi wa sita ya 150,000 (Laki na Nusu) kwa mwezi. Hawa vijana wanakosa hadi nauli wanalizimika kutuembea toka Kimara hadi Mikocheni, wengine wanatokea tegeta, kwa maana hiyo lazima waamke saa 9 usiku kuanza kuttembea ili waripoti kazını saa 1. Hapo hakuna chakula cha mchana wala kifungua kinywa. Wanaokesha nao ni njaa . Pamoja na tabu zote hizo, kosa ni kuomba Mashahara. Wasiongee chochote....!
Kwa pamoja hawa vijana walikaa, wakakubaliana kwamba kiongozi wao atume SMS kwa uongozi kwamba wana hali mbaya na wangeshindwa kuendelea kufanya kazi. Kosa ni hiyo SMS.
Hii kampuni ya ulinzi inaitwa HOSHI Security. Hawa vijana wanalipwa laki na nusu, ila inafika Tarehe 20 hawajalipwa..... Wanakuja kuomba stahiki yao, wanafukuzwa. Nimekuja kuongea na mmoja wa waimiliki wa nyumba, nao wanashangaa, na wamedhamiria kuifikisha hili swala kwa mamlaka.
Mamlaka Tanzania, angalieni huu UKATILI. Kwa nini Watanzania wanyanyaswe kiasi hiki?