Dazzle 2
Senior Member
- Oct 9, 2015
- 125
- 71
Kuna namna nyingi za kuonyesha kuguswa na misiba mikubwa inapotokea. Moja ya njia hizo ni kuwa na siku ya maombolezo kitaifa. Hii haina maana kuwa tupumzike tusiende kazini la hasha bali bendera zote kupepea nusu mlingoti kuashiria taifa liko kwenye kipindi cha kuomboleza. Kuondokewa na vijana zaidi ya 32 kwa wakati mmoja sio jambo dogo. Ni msiba mkubwa sio tu kwa wanafamilia bali kwa taifa zima. Serikali inapotangaza kuwa tuko kwenye maombolezo kitaifa inaleta uzito fulani tofauti na ilivyo sasa. Haya ni mawazo yangu tu.