Nanyaro Ephata
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 1,221
- 1,788
Kodi ya SALIO
Hapa serikali ilipaswa kufanya utafiti ingegundua kuwa watu wengi wanaweka salio kupitia nipige tafu,songesha, na nyingine za kukopa kupitia makampuni ya simu..yaani wananchi hawana uwezo wa kununua hata vocha hasa baada ya sekta binafsi kugandamizwa na awamu ya tano! Watu kushindwa kuwasiliana ni aina nyingine ya ubaguzi!
Kamwe mawasiliano hayawezi kuwa anasa
Kama mapendekezo ya serikali yakipitishwa na bunge dhaifu,basi simu itawekwa salio kwa wiki mara moja tena salio la jero! Itakuwa mwendo wa tafadhali nipigie!
Hawa jamaa wanaturudisha enzi zile vocha zinauzwa kwa dhamani ya dola...hadi leo vocha zinaitwa dola
Hebu fikiria VOCHA ikitengenezwa kampuni inalipia kodi,ikipelekwa kwa mteja inalipiwa kodi, ukiweka kwenye simu unalipia kodi.Mwendo wa kodi juu ya kodi sasa vocha ya jero itakuwa na dakika nne au pungufu ili kulipia kodi,yaani mwendo wa kodi juu ya kodi na juu ya kodi.
Wizara ya fedha na mipango inapaswa kuibua vyanzo vyenye tija kwa TAIFA na maslahi kwa umma na sio kukamua kile kidogo cha mvuja jasho.Mfano wangeweka tozo/kodi kwenye posho za waheshimiwa Wabunge,au wangepunguza kwa 50% posho na marupurupu ya wabunge na viongozi wa serikali
Waziri wa fedha aliwahi kujitamba kuwa yeye ni mchumi wa daraja la kwanza,zile tambo zote zilikuwa kwa ajili hii ya kutoza airtime kodi?
Mawasiliano na MIAMALA sio ANASA kwa Ulimwengu wa sasa,tena eneo hili ilitakiwa kodi iwe affordable zaidi ili kuchochea matumizi ya uwekaji na utoaji fedha kwa kufanya MANUNUZI na malipo kwa njia ya miamala sio Taslimu,hii ingepunguza kabisa black money kwenye mzunguko na hivo kukuza uchumi
Kwa hizi kodi zinazopendekezwa watu watarudi kwenye mfumo wa malipo Cash jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa uchumi
Bahati mbaya sana Dodoma kuna praise team hakuna bunge la kuishauri au kuisimamia serikali, pale ni kikao cha kijani ambacho kazi yake ni kugonga meza tu!