Serikali inayofanyakazi kwa matukio ni rahisi kujua ilipo

mambomoto

JF-Expert Member
May 10, 2011
326
195
Katika kile kinachoaminika kuwa serikali inapofanyakazi kwa matukio lazima utajua ilipo. Kwa bahati mbaya sana serikali yetu imekuwa ikifanya kazi kwa matukio basi unaweza kutabiri serikali yetu kwa wakati fulani ipo sehemu fulani. Hii imekuwa kuanzia ngazi za juu kabisa za uongozi wa nchi yetu. Mfano panapotokea tukio fulani unakuta mkuu wa nchi hadi wenyeviti wa vijiji ndo wanakurupuka kama vile ndo wanatoka usingizini na baada ya hapo wanarudi kutulia kusubiri tukio lingine huu ni utendaji wenye kasoro. Serikali yeyote ambayo iko makini haihitaji kufanya kazi kwa matukio kwani mfumo wake unajitosheleza pale pale ulipo na hata kama ni msaada wa serikali unatakiwa kuwa kama mvua inayonyesha sehemu zote. Leo hii likitokea tukio morogoro utajua tu serikali yote itakuwa huko, then likitokea mwanza utajua serikali sasa inaelekea mwanza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom