Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,035
- 6,904
Mwendazake Sikuwahi kumkubali ila kwenye kusimamia maamuzi aliyoamini alikuwa poa.Kwamba itakuwa nchi ya kila kitu kitajijua? Bonge la swali.
Nchi ina watu milioni 60, walipa kodi rasmi idadi yao haifiki hata milioni 10 (na walio wengi kati ya hao ni wafanyakazi wanaokatwa over 30% ya mshahara wao kila mwezi kwa kodi tu PAYE).
Then kodi ya miamala ingewagusa walau hao wengine ambao kiukweli ndio walio wengi, but hawajulikani katika vitabu vya kodi vya serikali lakini wanawajibika pia katika kuijenga nchi yao.
Tusitake kuitana majina yasiyo na sababu za msingi, eti watanzania wa chini. Hakuna cha mtanzania wa chini au wa juu wote ni watanzania na hii nchi tuliambiwa ni nchi ya kijamaa.
Hapa kinachokosekana ni kiongozi wa kujenga hoja za ushawishi na kusisimua ili hii kodi ionekane ya kawaida, ya lazima na ya kuleta mabadiliko.
Sasa tumekosa kiongozi shupavu haiingii akilini unashindwa kusimamia maamuzi,udhaifu mkubwa huu.