Serikali inaweweseka kwa ujumbe wa Kikosi cha watu 2,858 cha ukombozi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inaweweseka kwa ujumbe wa Kikosi cha watu 2,858 cha ukombozi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtego wa Noti, Nov 20, 2011.

 1. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,168
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  [h=2]Viongozi wakuu wa serikali watishwa[/h]


  Na Mwandishi wetu



  20th November 2011




  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha




  Viongozi wakuu wa Serikalini wametishwa kupitia waraka uliosambazwa kwenye mitandao ya simu za mikononi na kompyuta ukiwataka kuondoka madarakani ndani ya siku 100.
  Waraka huo ambao pia umesambazwa Jeshi la polisi, unaodaiwa kutumwa na kiongozi wa Kikosi cha watu 2,858 ambacho kimedai kuwa ni muungano wa askari waajiriwa kutoka majeshi mawili nchini.
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha alikiri kuzifahamu taarifa za waraka huo alipopigiwa simu na NIPASHE Jumapili na kusema Jeshi la Polisi nchini limeanza kuzifanyia uchunguzi na kuwataka raia wema kuzipuuza na kuwa watulivu wakati zinafuatiliwa.
  Aliongeza kwa kuwataka wale wote watakaopata taarifa kuhusu wanaosambaza waraka huo, watoe taarifa za siri kwa Jeshi la Polisi ili hatua zichukuliwe mara moja.
  Alisema wizara yake imeendelea kupokea taarifa kutoka kwa watu mbalimbali juu ya kusambazwa kwa ujumbe huo kwa njia ya simu za mkononi zinazowatishia viongozi wa kitaifa kuondoka madarakani ndani ya siku 100.
  Nahodha alisema, pia watu hao wanawashawishi wananchi kushiriki kwa njia ya simu za mkononi na kompyuta katika vitendo vya kuvunja amani nchini.
  “Jeshi la Polisi limeanza kufanya uchunguzi kubaini watu hao na wakipatikana tuanze kuwahoji ili hatua zichukuliwe dhidi yao,” alisema.
  Waziri Nahodha alisema Jeshi la Polisi limeanza kufuatilia ujumbe huo umeanzia wapi kutoka kwa mamlaka husika ili kubaini chanzo chake.
  Aliongeza kuwa wizara yake inawaonya na kuwaomba watu hao kujirudi na wasipofanya hivyo hatua zitachukuliwa.
  Alisema kwa kuanzia sasa Jeshi la Polisi limeanza kufuatilia wanaotumia simu na mitandao ya kompyuta kusambaza habari hizo.
  Taarifa hiyo ya Waziri Nahodha, inafuatia waraka huo wa wazi kwa viongozi wa kitaifa unaowataka kuondoka madarakani kwa madai ya kushindwa kuiongoza nchi na nakala kutumwa kwa Jeshi la Polisi Tanzania, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Idara ya Usalama wa Taifa Makao Makuu, Wizara ya Mambo ya Nje, Ofisi ya Waziri Mkuu, Benki kuu ya Tanzania (BoT) na Ubalozi wa Marekani Tanzania.
  Nyingine kwa Ubalozi wa Uingereza Tanzania, Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU)
  Kamanda Mkuu Al-Shabaab, baadhi ya Mashirika yasiyo ya kiserikali ya nje na ndani ya Tanzania na Vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania.
  Baadhi ya madai ya Waraka huo unaodaiwa kutumwa na kiongozi wa Kikosi cha watu 2,858 ambacho kimedai kuwa ni muungano wa askari waajiriwa wa kutoka majeshi mawili nchini.
  Kikosi hicho kimedai kuwa “Tupo sehemu mbali mbali ya Tanzania (kwenye vituo vya kazi) ambapo baadhi yetu tupo kwenye safu ya Ulinzi na Usalama wa Taifa. Tumeamua kuungana kwa pamoja kutekeleza kwa VITENDO dhana ya kulilinda na kulifia Taifa letu ambalo kwa sasa limekuwa kama pango la mafisadi, wezi na wafujaji wa HAKI za Watanzania.”
  source Nipashe Jumapili, 20 nov 2011.
  Mytek.
  Kumbe madaraka matamu, sasa kwa nini hawafanyi kama walivoagizwa na wananchi ili wasitolewe? naamini Kikosi cha watu 2,858 hawatanii na watafanya kweli.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,280
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  maneno hayauwi..cha msingi kuepukana na vyanzo vya malalamiko
   
 3. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,168
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ngoja tusubiri siku 100 tujimwage pale magogoni kama jamaa wa kule libya walivyoimwaga tripoli.
   
 4. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 16,777
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Maneno hayaui kivipi??
  Hujawahi kusikia mtu akihukumiwa kwa kutishia kuua?
  Jogoo hunena, "masihara masihara mwisho hua kweli"
   
 5. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,168
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  mi nakwambia utasikia mweyewe. subiri uone tu. unajua wakijifanya wan-take easy ndio mwanya wa jamaa kufanya kweli, na kwa kuwa wako kwenye system ya hata ulinzi wa nkulu, basi huenda mambo yakawa sawa.....tusbiri tuone....
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,882
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Na bado.................... mtakosa usingizi mwaka huu, mkeshe macho usiku kucha
   
 7. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hao waliotuma huo ujumbe nawatakia kila la heri ktkt kuiteleza kazi yao maana tumeshindwa kuwatoa mafisadi kwa njia za kidiplomasia mpaka wamefikia stage ya kuwamaliza wapambanaji kwa njia ya sumu.ILa waifanye kazi yao kwa viongozi wachache tu ambao ndio wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya nchi hii.Mungu ibariki Tz.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,463
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Serikali itumie nguvu sisi wananchi tulizo wapa kwa mujibu wa katiba kuwashughulikia ipasavyo hawa wahaini. Hakuna excuse kwa kuwacha kila mpuuzi afanye atakalo.
   
 9. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mwendo huu wa serikali ya CCM kunyanyasa wananchi wake,pamoja na kauli wanazotoa wakina Nape za kusema hii nchi ni ya CCM,zitaleta madhara makubwa sana na wahenga walisema chazo cha moto ni moshi................
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 10,987
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Maneno mtupu hayauwi! Tusubirie kidogo kama jamaa wote hawajachukua uraia nchi zingine. We unafikiri kikosi cha 2,858 ni mtu chache siyo. Wataona TZ ndogo! Wapuuzi wakubwa hawa mafisadi!
   
 11. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,721
  Likes Received: 782
  Trophy Points: 280
  kama hakuna ukweli kwenye huo ujumbe kwa nini waogope?kwanza ikiwa kama walivyopanga hao wanajeshi tupo tayari kuwasaidia kwa lolote lile
   
 12. doup

  doup JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 773
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii Kitu imekaa vizuri sana!!!

  Siku zote inlikuwa najiuliza hivi hakuna hata mtu mmoja kati ya waliokula viopo kuilinda TZ, kutuanzishia mwanga kwa style kuwapoteza viongozi wezi na wengineo wate wanaishirikiana naokatika kuiangamiza nchi.

  hawa jamaa naona watakuwa wametokewa na mzimu wa Nyerere, labda wawe wanatania.

  28,58 tupo pamoja katika kazi.
   
 13. doup

  doup JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 773
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningeshauri waanze kudonoa palepale
   
 14. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,168
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  sawa, subiri uone kitakachowapata hao unaowaita serikali.......unadhani Kikosi cha watu 2,858 wanatania?
   
 15. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Poa sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 16. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,528
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  siku zimeanza kuhesabiwa lini na mwisho wake lini? Nalog off
   
 17. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,168
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ni toka walipotoa tangazo kwa mara ya kwanza....zimepita kama siku 10 hivi.
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  28
  58
  haya
   
 19. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,625
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kamati ya ulinzi na usalama ya kitaifa ilishaujadili waraka chini ya mabrigedia wa zone sita na kuona hauna ukweli wowote lakini kama ilivyo ada habari inabaki kuwa habari na hivyo haiwezi kupuiziwa hata kidogo.
  Kikosi cha watu maalumu kinafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wahusika wakuu wanatiwa mbaroni.
   
 20. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,168
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  2858 inawezekana ikawa ni code...inaweza ikamaanisha siku au anything...letswait and see...
   
Loading...