tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,307
- 4,585
Uwanja wa Songwe Mbeya, ambao hauishi kujengwa, umekosa taa za njia ya kurukia na kutua kwa ndege mpaka sasa. Hizi taa (runway edge lights) hutumika kuonesha mwisho mwa pembe za barabara ya ndege wakati wa kiza na pale panapokuwa na shida ya kuona hususani kuwapo na mvua au ukungu.
Mwanzoni mwa mwaka huu Fastjet ilishindwa kutua katika uwanja huu na kurejea Dsm mara mbili (nilikuwa mmoja wa abiria katika safari moja, usipime)!!! Gazeti la Mwananchi liliandika habari hii (FastJet yashindwa tena kutua Uwanja wa Songwe)
Ikiwa serikali imeamua kujenga uwanja mkubwa kama ule, na kuufungua bila taa unategemea nini?
Wahusika wanasubiri siku moja kutokee maafa, ndipo taa zijengwe?