Serikali inasubiri tufe ndio ichukue tahadhari kwa uuzwaji wa gesi za kupikia holela mitaani?

ryan riz

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
423
682
Jamani hata nyie ni mashahidi, mitungi ya gesi tena yenye gesi ndani yake inauzwa kwenye maeneo hatari yenye mkusanyiko wa watu km vile vibanda vya chipsi, bar, migahawa karibu na majiko ya kupkia ya mkaa, maduka yanayouza sigara yaani wanapishana tu milango ya frame. Saa nyingine mbele ya haya maduka ndio kijiwe cha kupigia stori na kuvutia mifegi.

Hapo hakuna tangazo la onyo lolote wala tahadhari.. Mimi naona bora wale wanauzia vituo vya kujazia mafuta maana kule kaelimu cha nini wafanye raia wafikapo pale tunacho, ila huku watu wanaona barida tu.
 
Wabongo kwa lawama!
 
Last edited by a moderator:
Gesi ya miaka hii hailipuki.

Siyo ile stoo ya gesi kule haydom hosp iliyolipuka miaka ya sabini eeeh Mungu wangu. Watu walikufaje. Daaa hatari.
 
Mbona mnakaa chini ya nyaya na nguzo za tanesco na transformer hamjaomba serikali iondoe
 
Elimu Kidogo Upande Wangu
Nilisikia Gas Ya Sasa Ni Tofauti Na Ya Zamani Yaani Siyo Rahisi Kulipuka
 
Mh inabidi kuchunguza kwa kweli mi nimekwishasikia mara 2 mmoja kanda ya ziwa ililipuka na mtu kufariki. Aidha juzi tu hapa Buguruni kuna familia iliteketea na sababu kubwa mtungi wa gesi.
Mi naona mtoa mada ana point ni risk kwa mfano nyumba kadhaa zikiongozana na kufanya biashara ya gesi( km. tujuavyo wabongo kwa kuigana biashara). Ingewekwa umbali gani au maeneo gani yanaruhusiwa kufungua biashara ya kuuza gas. Kwa ujumla biashara hii ingedhibitiwa. Kwa wale wa zamani a.k.a 'wa miaka ya 47' ,takumbuka jinsi uangalifu uliokuwepo. Enzi hizo Unapiga simu, Agip wanakuletea mpaka nyumbani kwa vigari na fundi mahsusi na ni yeye ndio anakubadilishia na kukufiksia gas cylinder lingine. Siku hizi Dreva wa bodaboda anaaagizwa anakuja anakufiksia hata km hana ujuzi maana ataona aibu kusema hajui ndio akufiksie.
Kwa upande wangu nina jiko la gesi lakini nikikumbuka umakini wa zamani nasita kufunga gas cyllinder sasa sijui nitapataje ujasiri kwa sasa ukizingatia niko nje ya kwenye kitovu cha wajuaji yaani DSM.
 
Na viberiti visiuzwe ovyo ovyo mitaani, maana vinaweza kuwashwa na kuunguza vitu na watu!!
 
Ha

Umenikumbusha hadithi ya mwanaume mmoja aliyehukumiwa kwa kosa la kumiliki mtambo wa kutengeneza gongo, akaomba mahakama imhukumu pia kwa kosa la kumiliki mtambo wa kuwabakia wanawake.
 
Mbona sasa mitungi tunaenda kuitumia kwenye majiko yaliyo ndani ya nyumba kabisa?

Hapa bado sijaelewa au?
 
Mh inabidi kuchunguza kwa kweli mi nimekwishasikia mara 2 mmoja kanda ya ziwa ililipuka na mtu kufariki. Aidha juzi tu hapa Buguruni kuna familia iliteketea na sababu kubwa mtungi wa gesi.
Mi naona mtoa mada ana point ni risk kwa mfano nyumba kadhaa zikiongozana na kufanya biashara ya gesi( km. tujuavyo wabongo kwa kuigana biashara). Ingewekwa umbali gani au maeneo gani yanaruhusiwa kufungua biashara ya kuuza gas. Kwa ujumla biashara hii ingedhibitiwa. Kwa wale wa zamani a.k.a 'wa miaka ya 47' ,takumbuka jinsi uangalifu uliokuwepo. Enzi hizo Unapiga simu, Agip wanakuletea mpaka nyumbani kwa vigari na fundi mahsusi na ni yeye ndio anakubadilishia na kukufiksia gas cylinder lingine. Siku hizi Dreva wa bodaboda anaaagizwa anakuja anakufiksia hata km hana ujuzi maana ataona aibu kusema hajui ndio akufiksie.
Kwa upande wangu nina jiko la gesi lakini nikikumbuka umakini wa zamani nasita kufunga gas cyllinder sasa sijui nitapataje ujasiri kwa sasa ukizingatia niko nje ya kwenye kitovu cha wajuaji yaani DSM.
fanya utafiti kabla ya kukimbilia jf.
Gesi ya buguruni ililipuka baada ya moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme kusambaa mpaka kwenye mtungi.
Mitungi ya sasa ni vigumu sana kuvuja
 
Serikali imewek utaratibu wa namna ya kufanya biashara hiyo ya gesi ya kupikia. Kila duka utakuta lina mtungi wa kuzimia moto wa gesi, leseni, mizani nk.
Pia washindiliaji wa gesi kwenye mitungi wamewekewa masharti na serikali kwa ke-seal mitungi yote na kuweka label za kampuni husika n.k.
Mitungi midogo ya gesi ina majiko au stove zenye viberiti vya ndani ambavyo switch ikiwekwa on vinaliwasha automatically, hivyo hakutakuwa na mlipuko wa hatari. Majiko yote ya gesi siku hizi yana viberiti vya aina hiyo.
 
Naona hukunielewa maana yangu ni kuwa kama kila baada ya nyumba kuna gesi , risk ni kubwa kwani ile ya Buguruni kusingekuwa na gesi hata wale watu heunda wasingekufa. Sijui umenielewa Kabombe?
 
Serikali imewek utaratibu wa namna ya kufanya biashara hiyo ya gesi ya kupikia. Kila duka utakuta lina mtungi wa kuzimia moto wa gesi, leseni, mizani nk.
Pia washindiliaji wa gesi kwenye mitungi wamewekewa masharti na serikali kwa ke-seal mitungi yote na kuweka label za kampuni husika n.k.
Mitungi midogo ya gesi ina majiko au stove zenye viberiti vya ndani ambavyo switch ikiwekwa on vinaliwasha automatically, hivyo hakutakuwa na mlipuko wa hatari. Majiko yote ya gesi siku hizi yana viberiti vya aina hiyo.
Je huyo aliewekwa kuuza anao utaalamu wa kutumia hiyo fire extinguisher?
 
Sidhadhani kamwa hata wanajua namna ya kutoa lock na kuspray kwenye moto. Pia hata harufu ya gesi sidhani kama wanijua. Serikali inabidi ifanye serious teaching kwa wagu hawa na wapewe vyeti kama ilivyo kwenye ddriving licence.
 
Back
Top Bottom