Serikali inashikilia ng,ombe 9,500 kutoka nchi jirani, watapigwa mnada wahusika wasipolipa faini

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Waziri wa ufugaji na uvuvi Luhaga Mpina katika mahojiano na Azam Tv amesema serikali inashikilia ng'ombe 9,500 kutoka nchi jirani katika mikoa ya Kagera na Kigoma, katika operesheni inayoendelea

Mifugo hao watapigwa mnada enapo wahausika hawatajitokeza kuwalipia faini
Amesema uhusiano na nchi jirani hautayumba kwa sababu kitendo cha kuingiza mifugo nchini ni kinyume na sheria na uhusiano wa nchi mbili hauvunjwi na wztu wasiofuata sheria

Chanzo: Azam Tv
 
Kuna double standard hapo. Vifaranga walichomwa moto hawa ng,ombe wanapigwa mnada na wote kosa lao kuingizwa nchini kinyume na sheria.
 
Tatizo la mwingiliano wa mipakani ni sugu na baya lakini busara na diplomasia vitumike kuliko nguvu na kukomoana
 
Kwa nini ng'ombe wanawapiga mnada wakati vifaranga waliwachoma moto.
 
Back
Top Bottom