Serikali inapoteza mapato uwanja wa taifa

Dazzle 2

Senior Member
Oct 9, 2015
125
71
Serikali inapoteza mapato ya mamilioni ya pesa pale uwanja wa taifa eneo la nje kwenye Parking. Kila mechi kuna vijana wamejigawia maeneo na kutoza parking ya sh 2000 kwa gari linalopaki nje. Kwa wastani mechi moja inaweza kuwa na magari kati ya 250-300 ukiachia mbali mechi kubwa za simba na yanga au azam ambazo watu huja kwa maelfu na zile za kimataifa. Najiuliza hizi pesa tunazotozwa za parking na wale vijana wa mtaani pale nje kwa nini serikali au manispaa wasiweke utaratibu wa kuweka vijana wao pale kila mechi ili wakusanye pesa hii iingie serikalini kuliko kutozwa na wale vijana wa mtaani bila kujua zinaenda wapi?

Meya wa Temeke au meya wa jiji chanzo hicho cha mapato.
 
Kwanza ilitakiwa iwe bure! Uongozi wa uwanja ulitakiwa ulinde magari ya waliolipa ticket na kuingia uwanjani! Kwa kulipiwa pes mara 2 si sawa!
 
Wao wanajua magari yanayoingia ndani ya uzio wa uwanja mimi naongelea yale yanayopaki nje kabisa ya uzio wa uwanja.kuna vijana pale kila mechi wamejimilikisha maeneo ukipaki gari unalipa 2000 na hizi ndio tunazoshauri ziwekewe utaratibu wa kulipia kwenye mamlaka sahihi kwani kuna ubaya gani kuleta watu wa parking pale kukusanya parking fee na kuziingiza kwenye mapato rasmi kuliko kulipa pesa bila kujua zinaenda wapi kwa shughuli ipi
 
Heri tuwap vijana wetu wa mitaani walio rasmi wakusanye hizo 2,000 wakale na ndugu zao! Hayo mapato ya parki system ungejua mikataba yao utalia wamekubalian kuilipa serikali 10m kw mwezi.....wakati hayo makusanyo ya siku 3 tu.........mikataba ile I ufisadi mkubwa sana! Acha tu! Pale Ubungo walikaa JKT siku 7....mapato yake hadi aibu sawa na Ferry pale walikaa JKT na PCCB aibu sana wakaogop kusema mapato halisi kwa wanan maana wangetumbuliw wengi sana!!!!

Ndio maana tunataka manispaa au jiji lilimamie.lenyewe.sasa hivi kuna mashine za EFD zinatumika kukusanya mapato kutoa pesa zikaliwa kiujanja ujanja wakati wake ulishaishaaa
 
Serikali hawakuhitaji hizo fedha. Kama wangezitaka wasingeweza kujenga uwanja wenye kuingiza watu 60,000 kisha wakaacha kujenga parking za magari. Hii nchi iache hivyo hivyo. Acha vijana wajipatie kipato chao halali kwani ndio wanaosaidia wenye magari kuhakikisha usalama wa magari yao wanapokuwa kwenye mechi.
 
Back
Top Bottom