Serikali inapoteza mapato kwa masaa 4 kila mwezi.; Mtwara

wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
3,984
4,131
Ni hali inayoshangaza sana, leo majira ya 2 asubuhi nikitaka kufanya harakati za manunuzi hapa jiji la gesi, Mtwara kuchele kwa wana Ndanda Fc nimeshangaa kukuta maduka yote yamefungwa.

Sababu eti ni juma mosi ya mwisho wa mwezi,hivyo huwa ni siku ya usafi ambapo maduka hufunguliwa kuanzia saa 4 asubuhi.

Nimewaza ni kiasi gani ujazo wa mauzo hukosekana kwa muda huo wote.

Faida kiasi gani inakosekana kuzalishwa kwa wafanyabiashara.

Mahitaji muhimu kwa wananchi ni kiasi gani hucheleweshwa.?

Namfaham Comrade Gelasius Byakanwa,sitaki kuamini kama hili ni agizo lake kwa wakazi wa mtwara.

Usafi ni muhimu na ni jambo endelevu halihitaji siku maalum. Watu wazidi kuelimishwa ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi mara kwa mara kama sehemu ya kuwa kumbusha wajibu zao.

Naangalia namna ya kumfikia huyu mkuu wa mkoa,ili kama ndiye aliyeagiza basi walau atengue agizo lake na watu wachape kazi.

Leo ktk harakati za chama hapa nangwanda stadium,bila shaka atakuwepo.

Nimefurahishwa sana na hii kampeni yake ya kuifanya mtwara ya kijani.

"Wikendi njema".
 
Back
Top Bottom