pumper 2 pumper
Member
- Feb 13, 2017
- 69
- 42
Habari wandugu. Poleni na majukumu. Najua kupitia JF mambo mengi yanafikia walengwa hususani watoa maamuzi. Leo ningependa kupata mtazamo wa wadau humu ndani kuhusu mashirika ya kimataifa maarufu kama INGOS yanavyoedeshwa. Kwa uzoefu nilio nao mashirika haya yanategemea bajeti zao kutoka kwa wafadhili Sida Danida usaid nk na huwa wanaomba pesa kwa kuandika andiko mradi linalolenga kunisaidia serikali kutekeleza jukumu fulani. Na kwamba serikali ina bajeti finyu. Hiii ni nzuri. Tatizo ninatokea pale wanapoomba pesa nyingi kuliko uhalisia kwa ajili ya kulipa wafanyakazi wa mradi husika.mfano mfadhili anaambiwa project manager atalipwa Euro 10000 kwa mwezi wakati uhalisia ni mil 3 za Tza. Hapa serikali ingefaidika na kodi kama kilichoombwa ndio kimelipwa ila pia mfanyakazi angefaidika. Mashirika haya yanatumia pesa nyingi kwa ajili ya expatriate ambao kazi wanazozifanya hata hapa nchini kuna watu wenye uwezo nazo. Mfano kweli tunahitaji expatriate kwa ajili ya majiko banifu improved cooking stoves au choo cha kisasa improved toilet. ....jibu ni hapana
Naomba kuwasilisha.
Naomba kuwasilisha.