Serikali inapoteza kodi kwa wafanyabiashara wanaofanya huduma ya delivery

hata madukani pia hali ni hiyohiyo..kuna siku nilienda k/koo nikachukua mzigo wa milioni 2 na usheee..sasa wkt wa kuandika risiti mwenye duka akaniandikia milioni 1 neti..nilimkomalia ikabd achane aandike ya bei halisi
 
Na wewe si walewale tuu
 
Mimi huwa sipendi unafiki. Vitu vingi navyomiliki nikienda kununua chakwanza nawaambia nipeni bei isiyo na lisiti.

Haiwezekani nilipe kodi alafu baada ya apo mseme barabara sijui maendeleo kaleta magufuli wakati anakula na kulala kwa kodi zetu na mshahara wake halipi kodi.
Wewe kama mimi
 
TRA amkeni kuna hela nyingi zinapotea kwa wanaofanya biashara kwa mtandao na kufanya delivery, watu hawa wanaongoza kwa kukwepa kodi.

Imeshanitokea mara mbili, mara ya kwanza niliagiza TV yenye thamani ya tshs 1, 300, 000/= jamaa alioileta rist iliandikwa laki nne nikamgomea nikamwambia sitaipokea hadi nimepate risiti iliyoandikwa kiwango nitakacholipia na mara ya mwisho juzi tu kwenye kampuni nyingine pia utaratibu ulikuwa uleule.

Kifaa nilichoagiza kina thamani ya tshs 94, 000/ safari hii rist iliandikwa 5, 000/= . Nikamwambia aondoke na mzigo wake siku ya pili alinipigia simu na kuniambia amepata risiti hivyo aniletee mzigo nikamwambia sihitaji tena.

Hii biashara ni ya hovyo sana.
We ni mjinga kumbe,tangu lini mtu akinunua kitu anapewa RIST?
 
Hauko sahihi kwa sabbu kabla kitu hakijatoka kiwandani au bandarini tayari imeshalipiwa kodi, direct tax,,
Na mtiririko wa vAT katika nzunguko wa biashara umekaaje?

Maana kila uchochoro wa mzunguko wa biashara, vat inatozwa, bila kujali huko ulikoinunulia hiyo bidhaa tayari umelambwa Vat, unapoiuza, Vat tena.

Sasa Vat ngapi kwa bidhaa moja!

Siyo kwamba raia tunakamuliwa bila weledi?
Hata nchi zilizoendelea wanafanya huo uovu kweli?
 
K
Kweli bidhaa hadi kumfikia mteja tunakuwa tumelipa kodi nyingi.
We fikiria import tax; VAT, sijui kodi ya jiji, mapato. Na mteja akinunua bado serikali inataka 18%. Alafu tukiuliza kodi zinaenda wapi mnatuambia barabara utadhani TZ ndyo nch pekee yenye barabara yani.

Mabara bara yenyewe ni viraka kila sehem.
Kodi zetu zinatumika kununulia wapinzani!Bora wakose tu
 
Kulipa kodi ni uzalendo, lakini nchi hii ukikwepa kodi binafsi nakupongeza sana. Kuna mlolongo wa makodi ya uonevu sana, ni kama vile waliona njia pekee ya kukusanya pesa ni kodi, ajabu hakuna tax exemption kwa wafanyabiashara wa kawaida hata mara moja kwa miaka mitano mfululizo!
 
TRA amkeni kuna hela nyingi zinapotea kwa wanaofanya biashara kwa mtandao na kufanya delivery, watu hawa wanaongoza kwa kukwepa kodi.

Imeshanitokea mara mbili, mara ya kwanza niliagiza TV yenye thamani ya tshs 1, 300, 000/= jamaa alioileta rist iliandikwa laki nne nikamgomea nikamwambia sitaipokea hadi nimepate risiti iliyoandikwa kiwango nitakacholipia na mara ya mwisho juzi tu kwenye kampuni nyingine pia utaratibu ulikuwa uleule.

Kifaa nilichoagiza kina thamani ya tshs 94, 000/ safari hii rist iliandikwa 5, 000/= . Nikamwambia aondoke na mzigo wake siku ya pili alinipigia simu na kuniambia amepata risiti hivyo aniletee mzigo nikamwambia sihitaji tena.

Hii biashara ni ya hovyo sana.
Acha zipotee tu hata zikilipwa zitaenda kununua wapinzani na kujenga chattle
 
Tanzania tusingehutaji msaada au mkopo kutoka nchi yoyote kama tungekusanya property tax inavyostahili.
Vile kodi nyumba za makazi na sehemu za biashara hapo pia serikali imelala sana. Unalipia kodi ya mwaka chumba na baraza Sinza kwa sh. 3,000,000/= kwa mwaka serikali haioni ndani hata senti tano. Dalali nae kala
250,000/= bila kodi. Hizo pesa za mikataba ya frame wenye nyumba wanapeta tu. Kweli sisi sio masikini ila tumeshindwa tu kujiongeza.
Ndio yale yale Rwanda inakusanya mapato makubwa kwenye makampuni simu kuliko Tanzania.
We can stand on our own ila tu tujiongeze.
 
Hauko sahihi kwa sabbu kabla kitu hakijatoka kiwandani au bandarini tayari imeshalipiwa kodi, direct tax,,
Hauko sahihi. Bidhaa moja yaweza kulipiwa Kodi hata mara kumi.

Unajua maana ya VAT? Unajua impact ya neno"ADDED" kwenye neno"VAT"?

Kama TV itanunuliwa kwa say 1,000,000/= from Importer to Dealer, VAT yake ni 180,000/= so Dealer atalipa 1,180,000/- kununua hiyo TV from Importer.

Dealer akiongeza Bei/thamani ya hiyo TV say iwe 1,300,000 VAT yake itakua 234,000= so ataiuza kwa 1,534,000/=.

Yaani kwenye TV atakua na faida ya 1,300,000 - 1,000,000 = 300,000/-. Na kwenye VAT atakua na ziada ya 234,000 - 180,000 = 54,000/=. Hii 54,000/- ndo hupaswa kuwasilishwa TRA.

Na labda alienunua kutoka kwa Dealer sio final user, tumuite Supplier nae ataongeza Bei akiiuza, na kiasi kilichoongezeka kwenye VAT atakayopokea atatakiwa kukiwasilisha TRA.

Mfano wangu unahusu TV moja, ila ki uhalisia VAT huwasilishwa kwa pamoja/ujumla kwa bidhaa zote zinazotakiwa kutozwa kodi kwa kipindi/mwezi husika hivyo anapotoa risiti ya bei ndogo means ana record kua kapata hasara.

Mimi kama mimi hua najali tu kama bidhaa nimeipenda na imenivutia na Bei yake ninaikubali, mambo ya Kodi na risiti watajuana wenyewe supplier na TRA. Ningekua nina utaratibu wa kukatia bima vifaa vyangu ndio ningejali sana kilichoandikwa kwenye Risiti.
 
TRA amkeni kuna hela nyingi zinapotea kwa wanaofanya biashara kwa mtandao na kufanya delivery, watu hawa wanaongoza kwa kukwepa kodi.

Imeshanitokea mara mbili, mara ya kwanza niliagiza TV yenye thamani ya tshs 1, 300, 000/= jamaa alioileta rist iliandikwa laki nne nikamgomea nikamwambia sitaipokea hadi nimepate risiti iliyoandikwa kiwango nitakacholipia na mara ya mwisho juzi tu kwenye kampuni nyingine pia utaratibu ulikuwa uleule.

Kifaa nilichoagiza kina thamani ya tshs 94, 000/ safari hii rist iliandikwa 5, 000/= . Nikamwambia aondoke na mzigo wake siku ya pili alinipigia simu na kuniambia amepata risiti hivyo aniletee mzigo nikamwambia sihitaji tena.

Hii biashara ni ya hovyo sana.
Acha roho ya uchawi ndugu yangu, huwezi jua sababu ya wewe kuuziwa TV ya milioni 2 kwa milioni 1.3m, hivyo kwa vyovyote huo unafuu ndio umekuvutia kuagizia mtandaoni.
 
Back
Top Bottom