Serikali inapokosolewa kwa Constructive Criticism, je, Ifuate Ushauri? Hongera Bunge letu tukufu kufuata ushauri na kutuondolea ubatili huu

OK tukubaliane na hilo

Hapa ndipo penye tatizo la viongozi wa nchi yetu. Kujiuzulu Spika ni suala lenye 'public interest'
Hivi JYN hakuwa na washauri wakati wa maamuzi magumu kama hayo?
Hivi CCM hakuna wanasheria au wajuvi wa kubaini kwamba press ya JYN ilikuwa fyongo?
Bunge ndilo lina tatizo kweli. Katika hali ya kawaida katibu wa Bunge angetoa taarifa ya maneno machache 'tumepokea barua''. Hili tu lingeondoa utata na mashaka na tungesahau hao wengine.

Mh Mbati alieleza nia ya kwenda Mahakamani, ilikuwaje ikafikia huko ikiwa Katibu wa Bunge alikuwa na barua na mandate ya kusema 'amepokea'? Kuna sheria gani inamzuia Katibu wa Bunge kuzungumza huku ikimpa katibu wa CCM mamlaka ya mhimili wa Bunge?
Utaona kuna tatizo na hata barua iliyotolewa mahakamani ina shaka kama ilifuata taratibu

Kutofuata taratibu hakumaanishi haramu, lakini uhalali unajengwa juu ya taratibu.

Mahakama imefanya kazi yake bila shaka. Mahakama imepokea barua iliyothibitika au copy iliyothibitishwa. Mahakama haina sababu zozote za kuingilia taratibu nyingine.
Mkuu Nguruvi3, asante tena, hapa ni kama umemaliza kila kitu, hii ndio a concluding remarks kwenye bandiko hili, whataver is done kwenye kujiuzulu Spika, the end justifies the means, Spika JYN amejiuzulu legally kwa mujibu wa katiba, Sheria, taratibu na kanuni.
Asanteni sana wote mliochangia bandiko hili, la Hypothetical situation. Ile makala yangu na bandiko hili ni msaada mkubwa kwa serikali yetu, vitu vidogo vidogo kama hivi, vinaepukika.
Asanteni sana
Paskali
 
Wanabodi,
Hii ni Nipashe ya Leo, 30.01.2022
View attachment 2100761

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huteremka na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" leo ni swali na pongezi. "Serikali inapokosolewa kwa constructive criticism, kama ushauri uliotolewa ni ushauri nzuri wenye maslahi kwa taifa, jee serikali ifuate ushauri huo, au iupuuzie kwa kushupaza shingo?. Hongera sana Bunge letu Tukufu kwa kufuata ushauri na kutuondolea ubatili katika Barua ya kujiuzulu Spika JYN

Declaration of Hypothetical.
Naomba kuanza bandiko hili kwa kutoa angalizo la kitu kinachoitwa a hypothetical situation, yaani dhana ya kufikirika, inaweza ikawa kweli au ndio, na inaweza ikawa sio kweli au sio.

Kukitokea ukame wa muda mrefu, halafu wewe Siku ya Jumamosi, ukajitokeza in public kuomba mvua na kusema Jumapili mvua itanyesha. Na kweli hiyo Jumapili mvua ikanyesha kweli. Kunyesha mvua huko kutachukuliwa kuwa ni sababu ya maombi yako ya kuomba mvua, lakini ni Hypothetical situation tuu ya a coincidence kuwa muda wa kunyesha mvua ulikuwa amefika, hata usingefanya maombi ya mvua, hiyo mvua ingenyesha tuu, lakini kwa vile uliomba mvua na tunaishi kwa imani, hivyo utapokea credits za kuomba mvua na ikanyesha.

Hivyo bandiko hili ni la dhana ya barua ya kujiuzulu Uspika ya Mhe. Job Ndugai. Job Ndugai alipojiuzulu uspika, aliandika barua ya kujiuzulu ambayo sio a public document, kisha anaandika a Press Release kwenye Order Paper ya Bunge, kuelezea kuwa amejiuzulu uspika na ameandika barua kwa Katibu Mkuu wa CCM, na copy kwa Katibu wa Bunge.

Mimi nikapandisha bandiko kuikosoa taarifa hiyo kwenye kuwekwa kwenye order paper ya Bunge badala ya headed paper, nikaonyesha ukiukwaji wa katiba kwenye barua ya kujiuzulu uspika na kutoa mapendekezo yangu ya nini kifanyike kurekebisha makosa hayo. Baada ya siku kadhaa, barua yenye marekebisho imewasilishwa mahakamani, hivyo I have the right to claim hypothetically ule ushauri wangu umefuatwa, ila in reality, it Could be ni just a coincidence tuu hata nisinge shauri, bado marekebisho yangefanyika tuu. Coincidences kama hizi zinaitwa an amaizing coincidence kama ile coincidence ya mwaka 2014 niliposema rais wa Tanzania kwa mwaka 2015 atakuwa John Pombe Magufuli, na kweli akawa Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, kisha mwaka 2017 nikasema rais wa Tanzania 2020 atakuwa ni Samia Suluhu Hassan, akawa Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020 na 2019 nikasema 2020 Spika wa Bunge atakuwa Dr. Tulia Akson na amekuwa Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini... hizo zote ni just amaizing coincidence hivyo hata huu ushauri wangu kwenye hili la kujiuzulu uspika Je, wajua haramu isipoharimishwa inageuka halali? Na batili isipobatilishwa inageuka halali. Je, tuhalalishe ubatili huu kwa mhimili wetu wa Bunge?

Kikawaida serikali kitu kinachoitwa being, yaani kipo tuu, ila sio physical being, ni Hypothesical being ambacho kina exist, hivyo serikali haiwezi kukosea jambo lolote, lakini serikali inaendeshwa na watu na inaongozwa na watu, human beings, watu hao wanaoongoza serikali ni binadamu na sio malaika, hivyo wanaweza kukosea, watu hao wanapokosea, inahesabika kuwa ni serikali ndio imekosea, hivyo serikali inapokosea au kwa kukosea yenyewe au kwa kukoseshwa, lazima ikubali kuwajibika kwa makosa hayo. Japo nimesema serikali kama serikali haiwezi kukosea, ila watendaji ndio wanaokosea na kuikosesha serikali.

Kila serikali inapofanya makosa, sometimes huwa kunatokea watu wenye jicho tunduizi, ambao wanaona makosa hayo na kuikosoa serikali kwa kutumia ukosoaji wa ujengaji (constructive criticism) ambao hufanyika kwa kuonyesha kosa lililofanyika na wakati huo huo kutoa mapendekezo ya jinsi ya kurekebisha makosa na kushauri a way forward kurekebisha makosa yaliyofanyika yasijirudie na maisha yaendelee. Naishauri serikali yetu tukufu, pale inapokosolewa kwa makosa ya wazi, kwanza isikasirike, pili ifuate ushauri na kurekebisha makosa na kujitahidi makosa kama hayo yasijirudie. Kitendo cha serikali kukubali kosa, not expressly but impliedly kwa kurekebisha kosa bila kukiri kosa, kwa kupokea ushauri, sio udhaifu ni uimara, na kuonyesha serikali yetu ni serikali sikivu.

Moja ya makala yangu ya nyuma, nilishauri, viongozi wa kisiasa na wa serikali, wanapofanya makosa ya wazi na kuifanya serikali ionekane imekosea, wanapaswa kwanza kukubali makosa, kuomba msamaha na kuwajibika. Hiki ndicho kilichofanyika kwa Spika aliyejiuzulu, Mhe. Job Ndugai, Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere? kwanza alikubali makosa, kisha akaomba msamaha, japo msamaha wenyewe ulikuwa ni msamaha batili Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu!
akidhani atasamehewa, na baada ya kuomba msamaha huo batili, sisi waona mbali tukashauri, Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away? na baada ya shinikizo, ndipo JYN akakubali kujiuzulu ila huku nako alikurupuka na kuandika barua batili, hatukukaa kimya, Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away?

Taarifa ya kujiuzulu uspika ya Spika Mhe. Job Ndugai kwa vyombo vya habari, iliyosambazwa na ofisi ya Bunge, ni hii
View attachment 2100870
Taarifa hii ya Ofisi ya Bunge kwa vyombo vya habari, illionyesha Spika Ndugai ameandika barua ya kujiuzulu na kuilekeza kwa Katibu Mkuu wa CCM na nakala ofisi ya Bunge. Msemaji wa Katibu Mkuu wa CCM akakiri kuipokea barua hiyo, na Ofisi ya Bunge ikakiri kupokea nakala ya barua hiyo kutoka CCM.

Taarifa hiyo ya kujiuzulu ilisababisha mjadala mkubwa wa kwanini ipelekwe CCM badala ya ofisi ya Bunge kama katiba inavyoelekeza. Mjadala huo ulihitimishwa na taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa alichokifanya Spika Ndugai kuandika barua CCM badala ya Bungeni ni sawa tuu. Mimi nami nikaweka ukosoaji wangu ila ukosoaji wangu ulikuwa ni a constructive criticism kwa kukosoa na kushauri kitu sahihi cha kufanyika. Je, wajua haramu isipoharimishwa inageuka halali? Na batili isipobatilishwa inageuka halali. Je, tuhalalishe ubatili huu kwa mhimili wetu wa Bunge?

Mimi nilisema jambo fulani likielekezwa na katiba namna ya kufanyika, hakuna tena mjadala lifanyikeje, ni lazima lifanyike kwa jinsi ile ile katiba ilivyoelekeza, likifanyika kinyume, linakuwa ni batili au batilifu. Hivyo nilionyesha kifungu cha katiba kinachoekeza Spika akijiuzulu barua yake ya kujiuzulu inaandikwa kwa nani.

Ibara hii ya 149 1 (c) ya Katiba imeelekeza Spika akijiuzulu, ataandika barua kuliarifu Bunge. Kitu kikiishwa elekezwa na katiba namna ya kufanyika, kikifanyika kwa namna nyingine yoyote kinyume cha katiba, kitu hicho ni batili. Kujiuzulu halali ni kuandika barua kwa mamlaka yako ya uteuzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Spika kwa vyombo, imearifu ameandika barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na copy kwa Katibu wa Bunge. Katiba imeelekeza barua ya kujiuzulu Spika, itatumwa kwa Bunge. Kitendo cha Spika kuandika barua na kuituma kwa CCM kabla ya Bungeni, kumeifanya Barua ya Spika kuwa Batilifu, Bila huo ubatilifu kuondolewa, then barua hiyo imekuwa ni barua barua batili!. Katibu Mkuu wa CCM ametoa taarifa ya kupokea barua ya kujiuzulu Spika na tayari ameliarifu Bunge kuhusu kujiuzulu huko, na Bunge limeipokea taarifa hiyo b
atilifu hivyo hivyo ubatili wake na kuikubali. Huu ni ubatili!. Kama Bunge ndio mhimili wa kutunga sheria, Bunge lisipofuata katiba kwa kuukubali ubatili, nani atafuata katiba?.

Haki ya CCM Kupokea barua ya kujiuzulu, ni kama Mhe Spika JYN angejiuzulu uanachama wa CCM, hivyo kupoteza ubunge wake na uspika, ndipo CCM ingeliarifu Bunge.

Jee tuliruhusu Bunge letu tukufu kukumbatia ubatili katika madogo, jee ubatili huu ukihamia katika makubwa, nani atakuwa na jeuri ya kulihoji Bunge?
Hivyo nilitoa ushauri ufuatao
  1. Japo Spika Mhe. JYN tayari ameisha jiuzulu uspika, kujiuzulu huko, japo ni kujiuzulu batilifu, kufuatia taarifa kupelekwa mahali kusikohusika, lakini kujiuzulu ni kujiuzulu tuu, yaani Spika Ndugai ameishajiuzulu, lakini kwa kuheshimu katiba, lazima ubatili katika barua yake ya kujiuzulu uondolewe kwa kuandikwa barua rasmi kwa mujibu wa katiba.
  2. Kwa vile tayari CCM imeisha kiri kuipokea barua ile batilifu, Bunge nalo limekiri kuipokea barua kutoka CCM, marekebisho ya kuondoa ubatili huu, yafanyike kimya kimya. Spika mstaafu aelekezwe kuandika barua nyingine na Bunge lipokee kimya kimya barua mpya ya kujiuzulu kwa Spika iliyoandikwa kwa mujibu wa katiba, for filing kisha Bunge ndio litoe copy kwa CCM.
Kufuatia ubatili huu, Kiongozi wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, amefungua shauri Mahakama Kuu kuupinga ubatili huu, serikali ikaleta mahakamani barua rasmi ya Spika Ngugai kujiuzulu Uspika, ambayo imeonyesha Spika Ndugai, amejiuzulu kwa mujibu wa katiba, ni hii
View attachment 2100876
Barua hii ni utekelezaji wa ule ushauri wangu wa iandikwe barua nyingine kimya kimya na kuireplece ile barua batili. Barua yenyewe rasmi sasa ndio hii, na ndiyo iliyopelekea shauri la Mbatia kutupwa!. Japo ile taarifa ya kujiuzulu batili imeoishaondolewa kwenye website ya Bunge, lakini taarifa za CCM kuipokea barua batili ile ziliishatolewa na Bunge kuipokea barua batili ile ziliisha tolewa, ila ukienda kwenye files, hukuti tena barua batili, sasa utakutana na barua halali.

Natoa wito wa dhati kwa Serikali yangu, kukosea makosa madogo madogo is not a sin, to err is a human nature, kunapotokea makosa madogo madogo kama haya, na serikali kukosolewa, ni vitu vido tuu vya kurekebisha makosa na maisha yakaendelea. Serikali yetu ingekuwa inakubali makosa na kufuata ushauri, hii sintofahamu yote hadi kufikishana mahakamani, tusingefika huku kote. Hili jambo lilikuwa ni jambo dogo tuu, baada ya Bunge kutoa taarifa ya kujiuzulu kwa Spika Ndugai ikionyesha ameandika barua CCM, badala ya Ofisi ya Bunge, Bunge lingetoa taarifa ya pili kuonyeshea kulifanyika kosa dogo kwa barua kuelekezwa CCM, badla ya Ofisi ya Bungena kuonyesha kuwa Barua imeandikwa kwa Katibu wa Bunge na copy ndio kupalekwa CCM.

Unapokosoa kwa kuandika na kushauri, kitu cha kufanyika, halafu ukaona ushauri wako umefuatwa kama ulivyo, na makosa yamerekebishwa kama ulivyoshauri, huna budi kuandika tena na kutoa pongezi kwa serikali yetu kuwa ni serikali sikivu na kuuondoa ubatili ule, hivyo hapa nalipongeza Bunge letu Tukufu kwa kuondoa ubatili wa Barua ya Kujiuzulu kwa Spika Ndugai sasa imefuata katiba. Hongera sana kwa hili.

Sasa kumebakia ubatili mmoja tuu wa Naibu Spika, ajiuzulu kwanza nafasi ya unaibu Spika kabla ya kugombea Uspika na akiisha jiuzulu uNaibu Spika, ndipo angombee Uspika.

Nawatakia Jumapili Njema.
Wasalaam

Paskali
Update 1. Mchango muhimu toka kwa mchangiaji mmoja.
...

Mchango muhimu toka kwa mchangiaji mwingine

Concluding Remarks toka kwa one of our own GT wa ukweli humu jf.

Mkuu Nguruvi3, asante tena, hapa ni kama umemaliza kila kitu, hii ndio a concluding remarks kwenye bandiko hili, whataver is done kwenye kujiuzulu Spika, the end justifies the means, Spika JYN amejiuzulu legally kwa mujibu wa katiba, Sheria, taratibu na kanuni.
Asanteni sana wote mliochangia bandiko hili, la Hypothetical situation. Ile makala yangu na bandiko hili ni msaada mkubwa kwa serikali yetu, vitu vidogo vidogo kama hivi, vinaepukika.
Asanteni sana
Paskali
😂😂😂 Iliandikwa barua kimyakimya.
 
Mkuu Nguruvi3, asante tena, hapa ni kama umemaliza kila kitu, hii ndio a concluding remarks kwenye bandiko hili, whataver is done kwenye kujiuzulu Spika, the end justifies the means, Spika JYN amejiuzulu legally kwa mujibu wa katiba, Sheria, taratibu na kanuni.
Asanteni sana wote mliochangia bandiko hili, la Hypothetical situation. Ile makala yangu na bandiko hili ni msaada mkubwa kwa serikali yetu, vitu vidogo vidogo kama hivi, vinaepukika.
Asanteni sana
Paskali
Vinaepukika kwa kukiuka katiba ya JMT?
 
wanajua ww inapokuja swala hela ama madaraka akili yako henda likizo na humsifia hata shetani ni bora kuliko malaika
Hoja yako hii ni kweli, hakuna ubishi kuhusu shetani na malaika, shetani is more powerful kuliko malaika kwasababu shetani hufanya mwenyewe na malaika ni kiumbe wa kutumwa tuu!.
Pia shetani has a role, malaika hana role, kwasababu tangu uumbaji wa dunia hii, ni shetani ndie aliuchomeka ule 'mti' na lile 'tunda', bila 'mti' kutumika, 'kumega' lile 'tunda', tusingezaliwa!.

Kwanza sii wengi wanaofahamu kuwa shetani hapo mwanzo alikuwa malaika mkuu, the 2i/c to God!, who can do everything God can do ecept creation, yaani God ndiye The Only Creator, hivyo Lucifer alipoasi na kutupwa duniani, alitupwa na nguvu zake, hivyo ana powers kuliko malaika wote!.
Hili la shetani na malaika niliwahi kuliendeshea darasa humu


Moja ya sifa kuu ya shetani ambayo haifundishwi sana kwenye dini zetu ni uwezo wa shetani kujigeuza, disguises as anything, anyone!.

Kule kwenye bustani ya Eden, baada ya kujigeuza nyoka akapenya bustanini, kule ndani akajigeuza mtu, a handsome boy ndio akamtokea Eva, akamuonyesha 'mti', akamuuliza eva hilo 'tunda' ni la nini?, Eva akasema "Mungu ametukataza kula tunda hili". Shetani akamtempt kwa kumwambia Mungu ni mchoyo, hataki mfaidi utamu, kati ya matunda yote Duniani, 'tunda' lile ndio tunda tamu zaidi kuliko matunda yote, na 'likimegwa' 'tunda' hilo linawapa uwezo wa KiMungu wa kuumba viumbe wengine, yaani to create, creation!.
Shetani akamuonyesha Eva jinsi 'tunda' linavyo megwa kwa practical ya kumega 'tunda' and in fact shetani ndie wa kwanza 'kumega' 'tunda' na Eva, na kweli Eva akauona utamu wa 'tunda' akamfuata Adam na kumlazimisha na yeye 'amege' 'tunda' na kutokana na utamu wa tunda, baada ya Adam na Eva 'kula' 'tunda' kwa kumegeana, wakaishia usingizini, na hiyo zambi ya 'kumega' tunda, au 'kula' 'tunda' ndio dhambi ya asili, the original sin!. Ili binaadamu yoyote azaliwe, lazima hiyo dhambi itendeke!. Sisi Wakristu baada ya kuzaliwa na dhambi ya asili, dhambi hiyo huondolewa kwa kubatizwa.

Bwana wetu Yesu Kristo ndiye pekee aliyezaliwa bila dhambi ya asili, kwa Mama yake, Bikira Maria, kukingiwa dhambi ya asili, kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huku akiwa bikira, bila 'tunda' lake 'kumegwa'.

Na ndio maana viongozi wetu wa dini sisi Wakatoliki wanakula kiapo cha calibacy , Mapadri hakuna 'kumega', Masista hakuna kutoa 'tunda' 'kumegwa'.
Hivyo shetani yupo very tricky na most of the time he disguises as God!. Kuna watu wanamwabudu shetani wakiaamini ni Mungu!.
Hivyo be very careful!.
Paskali.
 
Mkuu Mwami Ntale, kwa vile Tanzania hatuna upinzani wowote wa maana, tulitaka Spika Bora wa kulibadili Bunge kuisimamia serikali na sio Bunge la kujipendekeza kwa serikali. Hivyo Dr. Tulia, akitulia anaweza!.
P
Paschal,ni ndoto ya kila mpenda haki kuona tuna bunge lenye uwezo wa kuisimamia serikali.Lakini amini kuwa as long as ccm iko madarakani hatuwezi kuwa na bunge la namna hiyo.Ni utaratibu wa ccm kuwa kila Rais na chama lazima viwe juu ya kila taasisi,hata kama katiba inasema vinginevyo.Kama rais angekuwa anaheshimu na kijali Uhuru wa mihimili mingine wala tusingekuwa na uchaguzi wa spika.
 
Unajilipaje nguvu yote hiyo unayotumia

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafanya kwa mapenzi tuu, ni kazi bure, ila situmii nguvu yoyote, kwasababu nafanya uandishi during my spare time. Nina shughuli nyingine inayoniingizia kipato cha kuendesha maisha yangu na familia yangu, hivyo uandishi wa habari naufanya bure kwa kujitolea tuu na sio kuingiza kipato.
P
 
Nafanya kwa mapenzi tuu, ni kazi bure, ila situmii nguvu yoyote, kwasababu nafanya uandishi during my spare time. Nina shughuli nyingine inayoniingizia kipato cha kuendesha familia yangu, hivyo uandishi wa habari naufanya bure kwa kujitolea tuu na sio kuingiza kipato.
P
Ok uzidi kubarikiwa Mungu huyu wa mbinguni tunaemwamini atakuzidishia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom