Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,552
- Thread starter
- #81
Mkuu Nguruvi3, asante tena, hapa ni kama umemaliza kila kitu, hii ndio a concluding remarks kwenye bandiko hili, whataver is done kwenye kujiuzulu Spika, the end justifies the means, Spika JYN amejiuzulu legally kwa mujibu wa katiba, Sheria, taratibu na kanuni.OK tukubaliane na hilo
Hapa ndipo penye tatizo la viongozi wa nchi yetu. Kujiuzulu Spika ni suala lenye 'public interest'
Hivi JYN hakuwa na washauri wakati wa maamuzi magumu kama hayo?
Hivi CCM hakuna wanasheria au wajuvi wa kubaini kwamba press ya JYN ilikuwa fyongo?
Bunge ndilo lina tatizo kweli. Katika hali ya kawaida katibu wa Bunge angetoa taarifa ya maneno machache 'tumepokea barua''. Hili tu lingeondoa utata na mashaka na tungesahau hao wengine.
Mh Mbati alieleza nia ya kwenda Mahakamani, ilikuwaje ikafikia huko ikiwa Katibu wa Bunge alikuwa na barua na mandate ya kusema 'amepokea'? Kuna sheria gani inamzuia Katibu wa Bunge kuzungumza huku ikimpa katibu wa CCM mamlaka ya mhimili wa Bunge?
Utaona kuna tatizo na hata barua iliyotolewa mahakamani ina shaka kama ilifuata taratibu
Kutofuata taratibu hakumaanishi haramu, lakini uhalali unajengwa juu ya taratibu.
Mahakama imefanya kazi yake bila shaka. Mahakama imepokea barua iliyothibitika au copy iliyothibitishwa. Mahakama haina sababu zozote za kuingilia taratibu nyingine.
Asanteni sana wote mliochangia bandiko hili, la Hypothetical situation. Ile makala yangu na bandiko hili ni msaada mkubwa kwa serikali yetu, vitu vidogo vidogo kama hivi, vinaepukika.
Asanteni sana
Paskali