Serikali inapoingia mikataba ya karne ya mahekta ya ardhi na wawekezaji ni pigo kubwa kwa kizazi kijacho

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,207
16,613
Wakuu

Kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja tangu Mama aingie madarakani utafiti unaonyesha kuwa mikataba mikubwa ya mahekta ya ardhi imesainiwa na wawekezaji wageni hapa nchini.

Mikataba hiyo iliyosainiwa inasoma miaka 99 Hadi 100!! Hii unaleta sintofahamu juu ya umiliki wa ardhi wa kizazi chetu kijacho!

Tujiulize haya yanayotokea ni juhudi za serikali kuifanya nchi yetu kuwa kama jamuhuri ya kenya ambapo mabepari wachache wanamiliki ardhi ya wengi Sana Hadi wazawa waliowengi hawana ardhi na kuwa watumwa katika nchi yao wenyewe.

Mamlaka husika TUNAWAOMBA mfuatilie hilo muokoe mstakabali wa TAIFA letu HUKO mbeleni!!

Asanteni KWA kusoma.
 
Na wewe kanunue ardhi kwaajili ya wajukuu wako.
Duniani ardhi haijawahi kuwa tatizo huko ulaya wanaishi miaka na miaka lakini bado kuna maeneo yako tupu kabisa.
 
Mkui
Nitafanya kazi ushauri wako
Lakini yangu itawatosha wangu tu je najua wajukuu na vitukuu vitakuta ardhi ya kutosha kama ina gawiwa KWA wageni KWA mahekta!!!?
 
Wasiwe wale wawekezaji wa brief case na $ 5,000 anachukua Ardhi ndiyo anayo enda kukopea. Baadaye wanatunanga ukienda kuwekeza Tanziania beba akili yako tu, capital utakita hukohuko.
 
Wakuu

Kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja tangu Mama aingie madarakani utafiti unaonyesha kuwa mikataba mikubwa ya mahekta ya ardhi imesainiwa na wawekezaji wageni hapa nchini.

Mikataba hiyo iliyosainiwa inasoma miaka 99 Hadi 100!! Hii unaleta sintofahamu juu ya umiliki wa ardhi wa kizazi chetu kijacho!

Tujiulize haya yanayotokea ni juhudi za serikali kuifanya nchi yetu kuwa kama jamuhuri ya kenya ambapo mabepari wachache wanamiliki ardhi ya wengi Sana Hadi wazawa waliowengi hawana ardhi na kuwa watumwa katika nchi yao wenyewe.

Mamlaka husika TUNAWAOMBA mfuatilie hilo muokoe mstakabali wa TAIFA letu HUKO mbeleni!!

Asanteni KWA kusoma.
Hii ni hatari

Kiembembuzi kumeshaisha sasa ni kuitapanya hovyohovyo bara
 
Utaratibu wetu upo wazi, ardhi ni ya serikali, hicho kipindi wajukuu wako wakiihitaji wawekezaji watalipwa fidia wataondolewa.

Ardhi ipo tupu imejaa hivi hamtaki watu waje wawekeze watoto wenu wapate ajira?
 
Umiliki wa ardhi kwa mwekezaji ambaye si raia ni kumkodisha kwa mkataba usiozidi miaka 30, haya ya miaka 99 yanatoka wapi?......acheni mchezo na rasilimali ardhi.
 
Akili za kimaskini ni hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu.

Utajikuta hapo unavieka vyako mia kadhaa unajio umemaliza na uzao wako. Usichojua hao wakezaji wakishachukua hayo namia elfu ya hekari ndio imekula kwa Ndg zako ambao leo hawana huo uwezo uliio nao wewe. Kesho wakiwa na uwezo watakuta ardhi imeshakuwa kama hapo Kenya. Familia moja inamiliki nusu ya ardhi ya nchi.
 
Hukunielewa maana yangu. Mimi ni mwananchi mnyonge tu na hapa nipo kwenye foleni ya kufatilia kazi ya sensa.
 
Wakuu

Kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja tangu Mama aingie madarakani utafiti unaonyesha kuwa mikataba mikubwa ya mahekta ya ardhi imesainiwa na wawekezaji wageni hapa nchini.

Mikataba hiyo iliyosainiwa inasoma miaka 99 Hadi 100!! Hii unaleta sintofahamu juu ya umiliki wa ardhi wa kizazi chetu kijacho!

Tujiulize haya yanayotokea ni juhudi za serikali kuifanya nchi yetu kuwa kama jamuhuri ya kenya ambapo mabepari wachache wanamiliki ardhi ya wengi Sana Hadi wazawa waliowengi hawana ardhi na kuwa watumwa katika nchi yao wenyewe.

Mamlaka husika TUNAWAOMBA mfuatilie hilo muokoe mstakabali wa TAIFA letu HUKO mbeleni!!

Asanteni KWA kusoma.

Eti mamlaka husika ! Mamlaka gani wakati huyu bibi kungwi Samia ndio anayeuza ?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom