Serikali inapochoka kuadhimisha kumbukumbu za kifo cha mwalimu nyerere..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inapochoka kuadhimisha kumbukumbu za kifo cha mwalimu nyerere..!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Aloysius, Oct 22, 2012.

 1. Aloysius

  Aloysius Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na Aloys Rugazia
  Jumapili asubuhi ya tarehe 14/10, ninaamka alfajiri na mapema nakujiweka sawa kwaajili yakuanza siku hii muhimu, ni baada yakuota ndoto za ajabu ajabu usiku kucha, ndoto zinazo changanya kuhusu nchi yangu, moja ya vipande vya ndoto hio ninavyo vikumbuka, ni ile yakumuona mwanamke mmoja nusu mtu nusu fisi, aking’ang’ana kubebena kipande kimoja cha mwamba mkubwa ambao umejichonga kama ramani ya nchi yetu hii, anataka anywe maji yote ya mwamba huo, anywe yeye peke yake na vitoto vyake, upande mwingine nikaona kama wananchi wa nchi yangu wote wanakwenda kwenye harusi ya mtu fulani aliyepata kuwa mashuhuri sana, lakini kilicho shangaza, wananchi hao wa nchi yangu walikuwa wamevaa matambara, tena machafu yaliyovunda, sio kwa umaridadi wa mtu aendaye tafrijani, mishipa yakichwa imewatoka, mama wenye watoto wao maziwa yakiwa yamewakauka kifuani, wananjaa, ukurutu na machacha miguuni! Ndipo nikageuza shingo niangalie mapambo ya ukumbi wa harusi hio kubwa, nikaona jua kali linawaka kama tanuru la moto, halafu kipande kidogo tu kimetiwa kivuli na kipande kingine kikubwa kimeachwa kichomwe jua kwaajili ya watu wale waliotokwa mishipa, weusi kama mkaa! Hata hivyo watu wa nchi yangu bado walionekana kumuheshimu sana yule mwenye kufanyiwa harusi, hawakujali wala hawakuoji kwanini wale waliokaa katika kivuli wamenenepeana na wao hawalipendi jua, halafu kwanini hawakukitanua kivuli kile kiwapate watu, kwanini kama shida ni pesa, hawakuchangishwa ada ya harusi ile ya mtu huyo mashuhuri ili maandalizi hayo yawajali pia, hawakuhoji hata kidogo, wamezoea, walijikalia kimya. Wakiwa njiani kwenda harusuni walisikia mlio mkubwa wa risasi, kuna mtu mmoja aliyelitumikia taifa ili kwa udi na uvumba, kwa damu na jasho, alikuwa ametunguliwa risasi ghafla kwasababu zisizo julikana, ni mkoa jirani tu, ila hawakujali sana kwakuwa wameanza kuzoea sauti za mitutu, damu zisizo na hatia kumwagika limeanza kua jambo la kawaida katika nchi yao. Mara na wao wakawa wanazisikia kwa mbali sauti za mwanamke yule nusu mtu nusu fisi, akihoji, kwanini Mlima Kilimanjaro hawaja gawa kati kwa kati na watu wa Nyayo? Kwanini kitenge cha ziwa Tanganyika hakijashona vazi kwaajili ya watu wote ambao kitenge hicho ni kama kinawahusu? Au mtu huyu anayekwenda kufanyiwa harusi aliwazidi akili? Huku wakiyasikia hayo kwa mbali, bado hawakujali, waliendelea kusonga mbele, mara nikaona mtu mmoja mwenye nywele nyeupe pe akimnyooshea mama yule upanga mkali ajabu, akamtolea maneno yalio mtisha mama yule mwenye kichwa cha fisi, “nakuambia ukiyanywa maji hayo yote kama unavyotaka tumbo lako nitalipasua kabla hujamaliza kunywa hata kikombe cha mia sita sitini na sita na maji hayo yote uliyo yanywa yatarudi tena katika mwamba huu mgumu”! Ndipo ndoto yangu ikazidi kutisha tena, huku nikirudisha macho yangu katika ukumbi wa harusi, mboni zangu zikakutana na tukio la ajabu, mshenga wa harusi ya yule mtu mashuhuri hakuwa ukumbini kumbe, alikua na kesi kubwa, kesi iliotikisa taifa, kulikuwa na watu wazee na wazima, wamejivika mavazi ya busara na wanalea tamaduni za watu ambao wanaonekana kama wenye busara, kunaviashiria hivyo ambavyo siwezi nikavieleza vizuri, ni kama nimevisahau hivi, japo sina uhakika kama kweli bura yao inaridhisha au la, mimi sio Mungu, ama kweli walichokidai kilibarikiwa na mama mchwa! Watu hao niliwasikia wakisema, ni lazima tudeke, lazima tudeke, tusipokudekea wewe tutamdekea nani, wewe bwana... au tukulaani, watu hao walimweleza mshenga yule wa harusi ya mtu yule mashuhuri. Ajabu mtuhumiwa wa kesi ile alikuwa bado yuko tumboni, ni kichanga, haileweki kama atazaliwa au la, na akisha kuzaliwa atakuwa mungwana au la, kwakua bado yupo tumboni, ila watu wale waliokuwa wazee tu waliendelea kuimba sisi lazima tudeke... na huyo mtoto huko tumboni tupeni tukipasue kichwa chake kama karanga. Lo! Ilikua ni ndoto nzito kweli, sikuelewa kwanini watu wale walisema lazima wadeke... na kwanini watake kichanga yule afe kabla yakupewa haki yakuchagua kuwa raia mwema au mualifu, na kwanini mshenga wa mtu yule mashuhuri na watu wale wakae chini kumjadili mtu ambaye ubongo wake haujatengamaa.., nje ya mle ndani walipokuwa wamekaa, kulikua na wazee wengine wamebeba kitabu chekundu hivi, nyuma kimeandikwa jina la bwana mmoja, ambaye picha yake iliniijia akiwa amekaa katika ghorofa lake moja refu sana (plaza) mji mmoja wenye miamba mingi, mfukoni akiwa amejaza vijisenti, akiwa anawarushia vijisenti vingine watu weupe na vingine watu wanene kama yeye, kitabu hicho ni cha mwaka 1977, kimechakaa chakaa, na mlango wake wa 39 na 67 ulikua unamzomea yule bwana harusi mtu mashuhuri, pia wazee wale walikua na kitabu kingine kimeandikwa, Sheria ya Tanzania Sura Namba Kumi na Sita na nyingine inayohusu watoto, walikuwa wanagonga mlango kwa nguvu, na nguo zao nyekundu kama damu ziki waya waya, wanapaza sauti, ni kazi yetu hiyo! ni kazi yetu! lakini kama watu walioingiwa na jinamizi, sauti yao haikutoka, walipaza na kupaza sauti lakini sauti haikutoka. Pia kwenye tukio hilo kulikua na mambo mambo kama wizi kidogo hivi na uharibifu wa matunda yalioota katika miti iliopo chini ya msalaba mrefu uliogusa wingu, uharibifu uliofanya msalaba ule ulie machozi ya damu, mambo yaliyo nifanya ni hakiki, niangalie ramani ya nchi yangu upya, kuhakiki kama niko katika taifa langu au moja ya mataifa ya Mashariki ya mbali, au Afrika Kaskazini au katika pembe la bara, hata hivyo sikugundua mara moja, ni kapita pita mitaani kukagua bendera zinazo peperuka, sikuona popote bendera ya taifa zilizoonyesha nipo katika taifa langu, hata katika ofisi za serikali na mashuleni. Oops! Lazima liwe taifa ambalo uzalendo uko mkiani, ndipo nikabahatika kuona katika nyumba moja ambayo paa lake la makuti limeoza, bila shaka linavuja, nikaona bendera ya kijani, rangi ambayo wengine wanaihusisha na kupe, sijui kwa namna gani, na jirani kidogo bendera imechorwa vidole ambavyo wengine wanavihusisha na upepo mharibifu, hekalu la mashetani wekundu, na wengine kama jahazi la ukombozi, ndipo nikajua kwa uhakika, nipo taifani kwangu, lakini bendera ya taifa, sikuiona popote! Nikiwa nimetoka jasho la uoga wa ndoto ile yakutisha, nikarudisha macho yangu ukumbini, hapohapo nikamuona mshenga yule, nikajiuliza, wako wawili au amefika pale kwa kasi gani, nikakumbuka uchumi huko juu, yule ntu mweusi mpwa wa Mbeya ndivyo atapavyo, amebebwa na kunguru? Mara mawazo yangu yakachukuliwa na mateso waliyo yapata wananchi wale chini ya jua angavu lililofura, wakimsubiri bwana harusi kwa hamu, ajabu, mshehereshaji (MC) na wote walio simama walimsifia mshenga yule kama vile yeye ndio anaoa siku hiyo, walimpamba nakumpaisha,, kwa kadri ya macho yangu, mpaka dakika za mwisho ajabu kupita yote, bwana harusi hakutokea, japo bibi harusi nilimuona ukumbuni aking’aa ng’aa macho kumsubiri bwana harusi. Mara waka kata tamaa watu wale waliovaa matambara nakuanza kutoka nje ya ukumbi kwa masikitiko, aidha wakiwa njiani walimtafakari bibi harusi yule mashuhuri, waka hisi anaongozana nao, mwisho wakatabasamu, nakufuta jasho liliowatoka machoni. Baadae kidogo kule ukumbini ukaletwa moto hivi, mbele ya yule bibi harusi na mshenga, ukashangiliwa na kupigiwa makofi na wale waliokua wamekaa kivulini, moto mkubwa ambao siku uelewa, na hapo nikashtuka ikawa kumesha kucha! Nimeona nisimulie ndoto hio mnisaidie kuilewa kwakua ni baada ya ndoto hii yakuamkia jumapili, ndipo nilipo pata wazo lakuandika makala hii, baada yakurukia remote, nakuiangalia televisheni tunayo ilipia kodi, hata nisione maadhimisho yoyote yanayo muhusu Kiongozi wetu Shupavu Hayati Mwl. Julius K. Nyerere. Kwanini yasinge fanyikia Butiama?! Kwanini yasinge fanyikia Butiama?! Nilihoji kwa hasira, Hivyo kwa kifupi kabisa napenda kusema jambo kuhusu maadhimisho ya baba wa taifa hili, Mwalimu Nyerere, maaandilizi hayaku ridhisha, na nikama maadhimisho hayajafanyika kitaifa, kilichoonekana kwa upande wa serikali kwa maoni yangu nikama kilichofanyika ni kuhitimisha mbio za mwenge tu ambazo hata Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga alionekana kusoma viongozi kama haja jiandaa kiasi cha kuto kuzingatia hata itifaki. Naamini kuwa mwenge sio swala la moto, au la kukimbia tu, ile ni ishara, kama ilivyo, alama ni ishara ya jambo fulani, na alama haiwezi kuwa muhimu kuliko jambo linalo ashiriwa, hio ni kwa mawazo yangu. Kama ni hivyo, naamini mbio za Mwenge ni moja ya futuko za uzalendo na uzalendo ni pamoja na kuwaenzi ipasavyo waliowahi kuwa wazalendo wakweli wa nchi hii nakuona namna yakuiga na kujifunza toka kwao, pia kutambua mchango wao katika taifa letu. Sitasema mengi kwakua kila mtu ameona maadhimisho ya Mwalimu yalikua hafifu, kwa makusudi au kwa bahati mbaya yamechanganywa na vitu vingi ambavyo vimemeza (distract) usikivu wa watu juu ya siku hio muhimu licha ya juhudi za runinga mbalimbali zilizojitolea ambazo zinastahili pongenzi kubwa sana. Nina waachia wengine waeleze ni kwanini imekua hivyo, lakini mimi niseme tu, naamini kuwa kwa nafasi aliokuwa nayo Mwalimu nchini, barani na duniani kuna haja ya sisi kua wabunifu wa namna yakuiadhimisha siku yake hiyo kitaifa, watu toka pembe zote za dunia haina shaka kuwa watakuwa tayari kuja kujadili nasi fikra zake, nakuzidi kuijua Tanzania kama taifa ambalo liliwahi kuzaa binadamu mwenye uwezo na uadilifu wa ajabu ambao kizazi hichi kinawakosa, tufanye hivyo bila uoga wakupungukiwa umaarufu au kusutwa, tufanye hivyo kwaajili ya taifa letu! Imenishangaza kua siku hiyo mama Nyerere alikokotwa kuja Shinyanga badala yakuachwa Butiama atafakari kifo cha mume wake, kupokea wageni, pamoja nakuweka walau ua kaburini kwa waridi wake Mwl. Nyerere. Mimi nina miaka ishirini na nne tu, labda sijui sana, ndio maana nakataa kukubali kuwa kuadhiminisha maana yake ni kuacha kwenda shuleni na kazini! Kwa kweli kilicho fanyika katika sikukuu hizi ni kama Serikali imechoka kuadhimisha siku hii ya Nyerere! www.twitter.com/Aloysrugazia Phone: 0764323268
   
 2. D

  Dr.Who Senior Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ye ndio amekufa peke yake?? kuna mashujaa wakweli Nyerere nae aliwasahau na kuwadhalilisha, What goes round comes round.

  Aliifilisi nchi. akae salama
   
 3. mgashi

  mgashi JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 304
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mkuu siongezi wala siponguzi neno, tatizo kiongozi wetu mkuu wa nchi akionekana anajishugulisha sana na mwalim wale wa iman yake watamkasilikia na yy hataki kuwauzi. Hivi hukusikilza radio imani? Mwalim alitukanwa na kuchwa mweupe kama mbulula fulani hiv. Je? Ulisikia lolote kuhusu hatua yoyote dhidi ya radio?
   
 4. O

  Oikos Senior Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kumbe hamjuiiiiii? Agenda ni kumrudisha mwarabu nchini ili kueneza uislamu. Chochote cha imani nyingine kinapigwa teke kitaalamu.. Nyerere ametukanwa kwenye DVDS chungu nzima za waislamu. Umesikia serikali imesema chochote? Wanajifanya kama hawaoni wala hawasikii... kitaeleweka tu
   
 5. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Unaumwa wewe! Waulize wenzako akina fulani walivyomuua st Thomas london ili wachukue madaraka wakati yeye aliwakataa.
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  tatizo wanajua kusherehekea siku ya mwalimu nyerere ni kuanza kusikiliza speech zake ambazo ni kama vile zinalenga viongozi wote wa serikali na chama wa sasa...na mkianza kuongea mambo nyerere aliyotufundisha kama uadilifu, mkweli, mchapa kazi, na mengine mengi watakua wanaona aibu kuongelea hivi vitu ambavyo sasa hivi hakipo hata kimoja
   
 7. D

  Dr.Who Senior Member

  #7
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwa nini hamja mpatia utakatifu hadi leo, mnaogopa nini kama si wanafiki? Mlifaidika na huu kiongozi mdini sasa mnatapatapa, nendeni kuhiji kaburini .

  Your honeymoon is over! wajinga nyie
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,734
  Trophy Points: 280
  Kweli mganga hajigangi! Kweli umeshindwa kujitibu pamoja na kujiita Dr? Hata kumeza pills umeshindwa?

   
 9. D

  Dr.Who Senior Member

  #9
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Huyu ndo mwanzilishi wa udini
  Kula kwa kaya
  Wasomi kukimbia nchi
  Wanasiasa kukimbia nchi
  Kutupeleka vitani
  Majirani wetu walikuwa maadui
  ..
  ..
  Wajinga nyie mlikuwa wapi???
   
 10. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mnamwonea Kikwete. Kwa uchafu huu anamoogelea unataka aadhimishe nini juu ya Nyerere wakati anambomoa? Kwake Kanumba ni bora kuliko Nyerere. Kwa alivyo na visa na kulipiza visasi unadhani anampenda Nyerere aliyemzuia kuukwaa wakati ule kwa vile alimjua kuwa angekuwa balaa kwa taifa kama alivyo sasa? Tumwache jamaa ale ni wakati wake ingawa huko tuendako anaweza kumalizia miaka yake lupango kama watanzania wataamua kuchagua haki. Kwa taarifa yenu ni kwamba wote waliomfuatia Nyerere hakuna anayeweza kumuenzi kwa vile wote wako pale kujaza mitumbo yao na watu wao kitu ambacho Nyerere hakufanya.
   
 11. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kweli wewe ni kilaza kama walivyo vilaza wenzako huko masjidi,ndio maana nchi inayumba kwa dhambi mliyofanya ya kuua kiumbe kisicho na hatia.
   
 12. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Madokta wapo wengi siku hizo..wengine wanaongeza makalio na wengine akina maji mafupi...so msishangae kwa majibu yatakayokuja
   
Loading...