Serikali inapobipiwa kununuliwa ni nani aanze kusema hapana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inapobipiwa kununuliwa ni nani aanze kusema hapana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jun 15, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika siku za karibuni tumesikia walimu sehemu mbalimbali za Tanzania wakilalamikia kutolipwa posho zao kama malipo ya awali kwa mtumishi yeyote anayeanza kazi katika kituo kipya kwa mara ya kwanza katika utumishi. Lakini pia tumesikia mara nyingi kutoka kwa viongozi wa walimu kuwa walimu wanayo malimbikizo ya madai yao ya muda mrefu ambayo serikali haijawatekelezea.

  Sio kusudio langu kujadili suala hili kwa leo, lakini kupitia shida hizi za watumishi hawa walimu nataka nisema yafuatayo, natambua kitu kinachoitwa serikali hukiona na wala huwezi kushika na ukasema hii ndio serikali. Lakini kwa lugha isiyo ya kisomi serikali ni taratibu, kanuni, sheria na sera ambazo hutumika kusimamia uwajibikaji wa jamii husika ambayo hugharimiwa kwa njia ya kodi na majukumu yake hutekelezwa na watumishi ambao huitwa 'watumishi wa umma'.

  Kwa hiyo serikali ni kila mtu ambaye ameajiriwa na mfumo huu na kutakiwa atekeleza majukumu katika mfumo huo, watumishi wake wanaanzia chini kabisa kwa mhudumu hadi kwa kiongozi mkuu mwenyewe ambaye katika mfumo wetu ni Rais.

  Ili watumishi hawa watekeleza majukumu yao ipasavyo wana miiko yao na wanaagizwa na kusimamiwa kutii miiko hiyo, ipo miiko mingi sana lakini moja wapo ni ule wa kukatazwa kupokea zawadi kutoka kwa mtu asiye serikali akishukuru kwa kazi yoyote ambayo tuliifanya wakati wa utumishi wetu. Kusudio la katazo hili ni kufunga milango ya rushwa na kutumia zawadi zetu kuandaa mazingira ya upendeleo. Juzi juzi hapa tumeshuhudia Mbunge wa Singida mjini akiandaa mazingira ya kuiweka sehemu ya serikali katika halmashauri ya Singida Mjini mfukoni mwake. Hapa sio kusudio letu kuona jambo jema la Mbunge halitekelezwi lakini Mohamed amevuraga uchaguzi wa 2015 kwa sababu walimu hawa ndio wengi wao watasimamia uchaguzi kipindi hicho, ameinunua serikali kwa kisingizio cha kutoa shukrani. Mohamed amevunja sheria ya utumishi wa umma kwa kuitisha mkutano mkubwa wa watumishi wa umma bila kibali cha serikali yenyewe, kwa nini amewachagua walimu na si wakaazi wa Singida mjini kwa ujumla wao, kwa nini watumishi wa umma. Wanagapi kati ya walimu hao walisimamia vituo vya uchaguzi katika jimbo lake?

  Serikali inapaswa kukemea hili siku nyingine tutaona mwekezaji anawachukua watumishi wa wizara moja anawapeleka mbugani, siku nyingine tutaona mawaziri wanapewa complimentary za ajabu , huku ni kuanza kubip kuinunua serikali. Hii ni hatari katika uendeshaji wa shughhuli za kiserikali. Tuanze kukataa leo, tulikatae kwa nguvu zote, tumzomee Mbunge huyu na ikiwezekana apigwe stop asigombe ubunge singida au alipie gharama za uhamishi wa walimu hawa ambao ameisha wakoroga vichwa vyao atakuwa amepoteza ubunge huo kwa vitendo navyo fanya leo


  Let us learn the lessons of the past at a fearful cost and we shall profit from them
   
Loading...