Serikali inapoahidi kufanyia kazi kero na mapendekezo ya wananchi

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,458
956
Mara nyingi tumekuwa tukisikia serikali na tasisi zake, kadhalika hata watu binafsi kuahidi kufanyia kazi mambo mbalimbali.Hii hupelekea ama kusitisha mjadala au kuongeza kiu ya wananchi na kujenga matarajio kwa matokeo ambayo aghalabu ni nadra kuyaona.
Mifano michache ya ahadi hii kutoka serikalini ni kama ifuatavyo:-

1. Mh.Vita Kawawa aliuliza:Mheshimiwa Spika, Kwa kuwa katika Halmashauri ya Namtumbo Kaimu Mkurugenzi wetu alifariki kwa kuungua moto akiwa katika harakati za kupata mafuta ya generator ya ofisi kufanya kazi usiku. Sababu ya msingi ni kukosekana kwa umeme. Je, Serikali inaweza kuwahakikishia wananchi wa Namtumbo watapatiwa umeme katika kipindi hiki cha miaka mitano ya Awamu ya Nne?
Jibu -NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI:
Mheshimiwa Spika, Ningependa kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba harakati ya Serikali kuhakikisha kwamba vijiji vyote hapa nchini vinapatiwa umeme inafanyiwa kazi.....pale fedha zitakapopatikana vijiji hivyo vitapatiwa umeme.

2. Profesa Ndullu alibainisha kuwa anakabiliwa na changamoto katika kurudisha hadhi ya BoT na kutimiza matarajio ya Rais Kikwete.
Alitaja baadhi ya mikakati itakayoiwezesha BoT kurudisha hadhi yake kuwa ni kushirikiana na Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kuzifanyia kazi tuhuma zilizotolewa na wananchi vyama vya upinzani na taasisi nyinginezo.

"Ajira za wafanyakazi wote wa BoT inafanyiwa kazi kwa kuangalia mwenendo mzima wa kazi zilivyotangazwa, usaili, alama za wasailiwa na jinsi zilivyotolewa, ili kuangalia kama waliopitishwa walikuwa na sifa zote zilizotakiwa," alieleza Profesa Ndullu.

3.WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema ripoti ya timu maalumu iliyoundwa kupitia mapendekezo ya Bunge kuhusu ripoti ya Richmond, imeanza kufanyiwa kazi na kwamba kama ipo haja ya kuwasilishwa bungeni katika mkutano wa sasa wa 11 wa Bunge itafanywa hiyo.

4.Mbunge wa Same Mashariki kwa tiketi ya CCM, Anne Kilango aling'aka bungeni akitaka watuhumiwa waliohusika katika kujipatia fedha za EPA kinyume na sheria wawajibishwe hali ambayo ilileta mjadala mkubwa bungeni.Wapo baadhi yao walimuunga mkono wakiwemo viongozi wa upinzani huku wabunge wengine wa CCM wakiponda hoja hiyo kuwa isiendelee kujadiliwa kwa madai kuwa inafanyiwa kazi na isiendelee kujadiliwa.

Tunaposikia kauli kama hizo ni mawili - tutarajie matokeo au tukate tamaa na kuona kuwa mjadala umefungwa isivyo rasmi? Nini maoni yenu wana JF?
 
Kuna msemo maarufu sana hasa kwa wanasiasa na watendaji serikalini na taasisi za umma ....kuwa suala fulani linafanyiwa kazi/tutalifanyia kazi.Je una maana gani? Does it mean tutarajie matokeo au ni kufunga mjadala/maswali kistaarabu?
Chukulia mifano michache ifuatayo:
1.Tarehe 12 Nov 2007 naibu waziri wa fedha alijibu suali bungeni"Mheshimiwa Mwenyekiti, wazo la kuanzisha Benki ya Wakulima ni zuri lakini linahitaji mchakato na maandalizi mazuri.....Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunalikubali, tutalifanyia kazi na nataka kuwahakikishia kwamba tutakapokuja kwenye bajeti ya mwaka 2008/2009, nadhani maombi hayo yatakuwa yamekwishashughulikiwa na tutaweza kuliambia Bunge kwamba tumefikia wapi.( sina uhakika kama hili limefanyiwa kazi na jibu kuletwa kikao hiki cha bunge)
2.tarehe 18 July 2003, mbunge Faida Mohamed Bakar [ CCM ]Special Seat
aliuliza swali na akajibiwa kuhusu umeme kwa nyumba za askari na Waziri wa Mambo ya ndani Mapuri Omar Ramadhan "napenda kumuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, suala la kufikisha umeme tunalifanyia kazi na tunatarajia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2003/2004 litakamilika "
( lilifanyiwa kazi?)
Hii ni mifano miwili tu.... ipo mingi...
Hivi maana ya msemo huu ni nin waungwana?
 
Kwa kifupi wababaishaji ndio wenye majibu ya namna hiyo, kama unajua unachokifanya huwezi kamwe kuwa na majibu ya kisanii namna hiyo.
 
Imebidi nirudi kufikiria hii thread hasa baada ya kusikiliza hotuba ya jana. Yawezekana lugha inaficha mambo fulani.
 
Mara nyingi tumekuwa tukisikia serikali na tasisi zake, kadhalika hata watu binafsi kuahidi kufanyia kazi mambo mbalimbali.Hii hupelekea ama kusitisha mjadala au kuongeza kiu ya wananchi na kujenga matarajio kwa matokeo ambayo aghalabu ni nadra kuyaona.
Mifano michache ya ahadi hii kutoka serikalini ni kama ifuatavyo:-

1. Mh.Vita Kawawa aliuliza:Mheshimiwa Spika, Kwa kuwa katika Halmashauri ya Namtumbo Kaimu Mkurugenzi wetu alifariki kwa kuungua moto akiwa katika harakati za kupata mafuta ya generator ya ofisi kufanya kazi usiku. Sababu ya msingi ni kukosekana kwa umeme. Je, Serikali inaweza kuwahakikishia wananchi wa Namtumbo watapatiwa umeme katika kipindi hiki cha miaka mitano ya Awamu ya Nne?
Jibu -NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI:
Mheshimiwa Spika, Ningependa kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba harakati ya Serikali kuhakikisha kwamba vijiji vyote hapa nchini vinapatiwa umeme inafanyiwa kazi.....pale fedha zitakapopatikana vijiji hivyo vitapatiwa umeme.

2. Profesa Ndullu alibainisha kuwa anakabiliwa na changamoto katika kurudisha hadhi ya BoT na kutimiza matarajio ya Rais Kikwete.
Alitaja baadhi ya mikakati itakayoiwezesha BoT kurudisha hadhi yake kuwa ni kushirikiana na Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kuzifanyia kazi tuhuma zilizotolewa na wananchi vyama vya upinzani na taasisi nyinginezo.

"Ajira za wafanyakazi wote wa BoT inafanyiwa kazi kwa kuangalia mwenendo mzima wa kazi zilivyotangazwa, usaili, alama za wasailiwa na jinsi zilivyotolewa, ili kuangalia kama waliopitishwa walikuwa na sifa zote zilizotakiwa," alieleza Profesa Ndullu.

3.WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema ripoti ya timu maalumu iliyoundwa kupitia mapendekezo ya Bunge kuhusu ripoti ya Richmond, imeanza kufanyiwa kazi na kwamba kama ipo haja ya kuwasilishwa bungeni katika mkutano wa sasa wa 11 wa Bunge itafanywa hiyo.

4.Mbunge wa Same Mashariki kwa tiketi ya CCM, Anne Kilango aling'aka bungeni akitaka watuhumiwa waliohusika katika kujipatia fedha za EPA kinyume na sheria wawajibishwe hali ambayo ilileta mjadala mkubwa bungeni.Wapo baadhi yao walimuunga mkono wakiwemo viongozi wa upinzani huku wabunge wengine wa CCM wakiponda hoja hiyo kuwa isiendelee kujadiliwa kwa madai kuwa inafanyiwa kazi na isiendelee kujadiliwa.

Tunaposikia kauli kama hizo ni mawili - tutarajie matokeo au tukate tamaa na kuona kuwa mjadala umefungwa isivyo rasmi? Nini maoni yenu wana JF?

kwa kweli thread hii imenikumbusha mbali, nikiangalia hali ya uchumi unavyoenda,.. katika nyakati tofauti serikali imesema inafanyia kazi upatikanaji wa umeme wa uhakika. JE ni mpaka lini...
neno jingine ni tupo katika mchakato.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom