WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,459
- 952
Mara nyingi tumekuwa tukisikia serikali na tasisi zake, kadhalika hata watu binafsi kuahidi kufanyia kazi mambo mbalimbali.Hii hupelekea ama kusitisha mjadala au kuongeza kiu ya wananchi na kujenga matarajio kwa matokeo ambayo aghalabu ni nadra kuyaona.
Mifano michache ya ahadi hii kutoka serikalini ni kama ifuatavyo:-
1. Mh.Vita Kawawa aliuliza:Mheshimiwa Spika, Kwa kuwa katika Halmashauri ya Namtumbo Kaimu Mkurugenzi wetu alifariki kwa kuungua moto akiwa katika harakati za kupata mafuta ya generator ya ofisi kufanya kazi usiku. Sababu ya msingi ni kukosekana kwa umeme. Je, Serikali inaweza kuwahakikishia wananchi wa Namtumbo watapatiwa umeme katika kipindi hiki cha miaka mitano ya Awamu ya Nne?
Jibu -NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI:
Mheshimiwa Spika, Ningependa kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba harakati ya Serikali kuhakikisha kwamba vijiji vyote hapa nchini vinapatiwa umeme inafanyiwa kazi.....pale fedha zitakapopatikana vijiji hivyo vitapatiwa umeme.
2. Profesa Ndullu alibainisha kuwa anakabiliwa na changamoto katika kurudisha hadhi ya BoT na kutimiza matarajio ya Rais Kikwete.
Alitaja baadhi ya mikakati itakayoiwezesha BoT kurudisha hadhi yake kuwa ni kushirikiana na Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kuzifanyia kazi tuhuma zilizotolewa na wananchi vyama vya upinzani na taasisi nyinginezo.
"Ajira za wafanyakazi wote wa BoT inafanyiwa kazi kwa kuangalia mwenendo mzima wa kazi zilivyotangazwa, usaili, alama za wasailiwa na jinsi zilivyotolewa, ili kuangalia kama waliopitishwa walikuwa na sifa zote zilizotakiwa," alieleza Profesa Ndullu.
3.WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema ripoti ya timu maalumu iliyoundwa kupitia mapendekezo ya Bunge kuhusu ripoti ya Richmond, imeanza kufanyiwa kazi na kwamba kama ipo haja ya kuwasilishwa bungeni katika mkutano wa sasa wa 11 wa Bunge itafanywa hiyo.
4.Mbunge wa Same Mashariki kwa tiketi ya CCM, Anne Kilango aling'aka bungeni akitaka watuhumiwa waliohusika katika kujipatia fedha za EPA kinyume na sheria wawajibishwe hali ambayo ilileta mjadala mkubwa bungeni.Wapo baadhi yao walimuunga mkono wakiwemo viongozi wa upinzani huku wabunge wengine wa CCM wakiponda hoja hiyo kuwa isiendelee kujadiliwa kwa madai kuwa inafanyiwa kazi na isiendelee kujadiliwa.
Tunaposikia kauli kama hizo ni mawili - tutarajie matokeo au tukate tamaa na kuona kuwa mjadala umefungwa isivyo rasmi? Nini maoni yenu wana JF?