MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Maneno yangu ni kiduchu tu!
Mh Tundu Lissu alishasimama kidete muda mrefu kupigania mikataba mibovu ya madini nchini, aliitwa mchochezi na kisha akafungiliwa kesi mahakamani.
Hivi sasa wengi hawajui anachomaanisha Mh LISSU, anaelewa fika kitakachoenda kutukuta na ndio maana amesema anapinga hili jambo hadharini kokote.Kwa ninavyomuelewa LISSU sio mtu wa kuhongwa na hahongeki labda asingiziwe tu, yatakayotukuta tutasema tena kua "Tundu LISSU aliyesema haya". Hapa ndipo tutakapomkumbuka na kulitaja jina lake muda wote na mwisho wa siku ataonekana kama shujaa na. mzalendo namba moja wa taifa hili.
Zaidi amemaanisha kua ni kwanini tuhamishie nguvu kubwa kwenye mchanga ulipo bandarini ambapo sisi mali yetu ni persent ndogo sana pale kuliko mali ya mzungu ambayo ni halali yake kwa mujibu wa sheria za mikataba iliyopo? Gharama tunayotumia kuhangaika na ule mchanga ni kubwa mno kuliko kipato chetu kilichpo mle, ni kubwa na bado kuna hasara ya fidia tutakayolipa hao wazungu wakiamua kutufungulia kesi.
Hivi tunaelewa kua mali kubwa na nyingi ni ile iliyoko mgodini kuliko iliyoko kwenye huu mchanga wa bandarini? Tunaelewa kua tunaibiwa kwa kiasi kikubwa kule Buzwagi kuliko kwenye mchanga uliko bandarini? Hivi tunaelewa kua sheria iliyopo inawaruhusu hawa jamaa kufanya watakacho kule migodini? Hivi tunaelewa kua kama hawa jamaa walikua wakituibia na wanajua kua wanaweza kula hasara muda wowote? kwanini wasiongeze kasi ya kutuibia kule migodini wakati sisi tunakomaa makanikia kule bandarini?
Kuna ugumu gani wa kufanya mazungumzo na hawa wawekezaji tukafanya "REVIEW" ya mikataba yote tulioingia nayo ili kuona nasi tunanufaikaje? Kwanini tunakomalia kuwaita wezi ilihali mali tuliwapa sisi tena kisheria? Kwanini wale waliowapa mali yetu wasiwe wezi?
IPO SIKU WASIOMUELEWA MH LISSU WATAMJUA TU.
LISSU AMEWAZA MBALI TOFAUTI NA TUNAVYOMTUHUMU KUTOKANA NA KUTOLIFAMU VYEMA JAMBO HILI.