Serikali inakosea kuwakamata Changudoa. Inasambaza maradhi kwa wengine hivi hivi.

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,355
2,736
Dokezo:- Ukamataji wa Makahaba sio wa nchi Nzima. Waliokamatwa Dar wamehamia Morogoro na Pwani, Wanaokamatwa Mwanza Wamekuja Geita, Sengerema na Chato, Wanaokamatwa bukoba Mjini wameenda Wilaya ya Missenyi huko Mutukula na wengine Karagwe. Wanaokamatwa katika miji mikubwa wanaenda pembezoni.

Siasa kuingilia mipango ya kitaalam:- Kutokana na kasi ya kiongozi wa juu, baadhi ya viongozi wa chini wanarekodi kila neno analolitaja Mkuu wa nchi mdomoni na kutaka walitekeleze ili wamridhishe wabaki Madarakani.

Hatari Iliyopo:- Wale woote waliokuwa wanapata huduma rafiki mfano dawa za ARV maeneo husika walipopazoea wamekimbia wengine bila kuwa na dawa za kutumia walikokimbilia. Ni ngumu kwenda sehemu mpaya na kuanza kupewa huduma rafiki hasa wakijua kuwa biashara yako ni ya kujiuza. Madaktari na wengineo wanajua umuhimu wa ARVs katika kupunguza viral road katika damu na hivyo kusaidia kupunguza maambukizi.

Wateja wa Wadadapoa ni akina nani?:-
  • Kwa ufupi wateja wa wadada poa ni sisi wenyewe wanaume Watanzania tunaoishi na wadada hawa mahali wanapoishi.
  • Ni sisi wenye wake na watoto,
  • Ni sisi walimu ambao huenda kusahihisha mitihani,
  • Ni sisi wanafunzi wa Vyuo, ambao ni wapenzi wa watoto wa vigogo wakiwemo wakuu wa polisi, wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri n.k
  • Ni sisi wakimbiza mwenge
  • Ni sisi vijana wa chama
Tunazungukana sisi kwa sisi!! Sasa hata hawa wenye maambukizi mkiwakimbiza na kuwakamata na matokeo yake tukutane nao pasipo wao kumeza dawa zao kwa usahihi tunafanya nini jamani serikali. Nimeona kabisa mtu aliyekimbia mjini kaenda kijijini watu wanajishindia jamani tena kwa hela kidogo.......tunafanya nini jamani nchi yangu.

Hivo serikali kwa mkono wake yenyewe imepeleka hatari tena kwa watu ambao uelewa wao ni mdogo hata wa kutumia kondomu, mahali ambapo CTC ni chache. Japokuwa nyaraka za serikali zinaonesha kutambua makundi hayo na kuweka Mipango ya Kuwasaidia, lakini katika nyaraka nitakazo weka hapa hakuna la kuwapeleka polisi na kuwafunga miezi 6 au kulipa faini.

Kwa mtu wa kawaida atanishangaa. Lakini naomba tujiulize, hawa machangudoa wanatengenezwa na nani? Machangudoa tunawatengeneza wenyewe na serikali ikiwemo. Hatuna mahali ambapo kuna mpango maalum wa serikali kuwasaidia yatima. Hakuna mpango wa kuwasaidia watoto wa mtaani, elimu inayotolewa kuanzia darasa la kwanza hadi form six haiwezi kuajiri mtu.

Watu wanamaliza vyuo vya ualimu wanasubiri mwaka mzima kupata ajira au kupangiwa shule za kufundisha. Achana na wale waliosoma fani nyingine mbali na ualimu ambao baadhi yao wanakaa hadi miaka mitano bila ajira.

Katika mpango wa kuzuia UKIMWI wa serikali wa mwaka mpaka 2018, kuna mikakati ya kupambana na kuzuia UKIMWI kwa kutoa huduma rafiki kwa makundi hatarishi kama Female Sex Workers, Male having sex with Males(Hawa wanapewa lubricants na condoms) na wale Wajidunga ambao inabidi wapewe elimu ya kuacha huku wale ambao tayari wameugua wapewe huduma ya matibabu kama ARVs na huduma za matibabu ya Magonjwa ya ngono.

Baadhi ya Ushahidi kutoka katika Nyaraka za Serikali.

Ushahidi kutoka :
MKAKATI WA TATU WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA
(2013/14 – 2017/18)


3.1.7. Ushamiri wa Maambukizi ya VVU miongoni mwa Makundi Maalumu
3.1.8. Watu Wanaojidunga Sindano ya Dawa za Kulevya
3.1.9. Makahaba
3.1.10. Wanaume Wanaofanya Ngono na Wanaume Wenzao

Maelezo ya Serikali kuhusu Makundi hayo:-

Kutoka :

Serikali ikieleza kufahamu:

HIV/AIDS services for Key Populations (KPs): KPs are populations that are at higher risk of being infected or affected by HIV, who play a key role in how HIV spreads, and whose involvement is vital for an effective and sustainable response to HIV. In Tanzania mainland, groups which have been documented to be at a higher risk of HIV infection include Men who have Sex with fellow Men (MSMs), Female Sex Workers (FSWs), and People Who Inject Drugs (PWID), prisoners and other mobile population groups including among others, fishermen, miners, plantation labourers and trackers.


Serikali ikieleza jinsi ya kusaidia :

Stigma and discrimination experienced by PLHIV, as well as by population groups perceived to be most at risk for infection are major obstacles to the provision of accessible services for both prevention and treatment. The HSHSP III calls for the integration of health services for KPs aimed at fostering non-judgmental, inclusive, and responsive health services for all. Comprehensive services for KPs will also be made available in targeted health facilities.

Kwa nia hii ya Serikali baadhi ya miji imeanzishwa miradi ya kuongea karibu na makundi haya mfano makahaba ili wanapougua iwe ni magonjwa ya ngono, au HIV waende hospitali watibiwe wapewe elimu ya kujikinga na kuwakinga wengine na miradi hii ya KP (Key Populations) ilishaanza kufanya kazi vizuri mfano Mwanza Mjini, sasa Serikali inafanya nini pale inapofanya kinyume na mipango yake?

Nimeweka mpango mzima wa serikali, msome mpango mzima kisha mniambie hii kamata imetoka wapi.
 

Attachments

  • NACP Operational Plan Final - 25 March 2014 PDF.pdf
    870.8 KB · Views: 189
Hawa watu wangeboreshewa mazingira yao ya kazi Na serikali ikachukua kodi, bahati mbaya serikali CCM haina ubunifu wa kutengeneza pesa isipokuwa inaubunifu wa kutumia tu
 
Biashara ya madada poa inalipa sana najaribu kuitafakari taratibu

Kaka iangalie kimapambano.............ugonjwa upo na kuna shida, mfano wahudumu wa afya baadhi wanatoa lugha chafu ikiwa Mjidunga au kahaba ataenda hospital kuomba huduma. Baadhi watasema unanuka, wengine watasema we malaya....yaani aiseee
 
Kiongozi tunaangalia juu juu tuu, kuna shida..........
Iko kubwa sana lkn tutafanyaje sasa maana serikali imekuwa chanzo cha matatizo, kuna msichana mmoja alikuwa kapanga na akisomesha mtoto wake Na mdogo wake kupitia hiyo biashara, sasa ajiandaa kurudi songea
 
Kaka iangalie kimapambano.............ugonjwa upo na kuna shida, mfano wahudumu wa afya baadhi wanatoa lugha chafu ikiwa Mjidunga au kahaba ataenda hospital kuomba huduma. Baadhi watasema unanuka, wengine watasema we malaya....yaani aiseee

Inasikitisha sana, ninadhani kuna umuhimu wa wizara ya afya kuanzisha semina za Ethics in Health Care System kwa wafanyakazi wake wote.
 
Kaka iangalie kimapambano.............ugonjwa upo na kuna shida, mfano wahudumu wa afya baadhi wanatoa lugha chafu ikiwa Mjidunga au kahaba ataenda hospital kuomba huduma. Baadhi watasema unanuka, wengine watasema we malaya....yaani aiseee
Mkuu kuna kautafiti nilishawahi kufanya huko nyuma kwenye hispital za serikal kwa sababu zangu najua mengi sana, muda ukifika dunia itajua
 
Kodi ya madada poa inapotea bure, wangeachwa tu halafu wakasajiliwa. Si serekali haina dini nani anasema dhambi? Dhambi we mwenyew unazo kibao unaiba mali za umma.
 
Hawa watu wangeboreshewa mazingira yao ya kazi Na serikali ikachukua kodi, bahati mbaya serikali CCM haina ubunifu wa kutengeneza pesa isipokuwa inaubunifu wa kutumia tu
mkuu unamaanisha wapewe kabisa na EFD na sisi wateja tuhimizwe kudai risiti?!
 
Mkuu jaribu kufikiri mbali zaidi!
Kufikiri mbali zaidi kunathibitishwa kwa kipimo gani? Wewe unadhani kwanini kuna watu wako tayari kuitwa mabikra bila kujali umri wao lakini hawako tayari kujihusisha na ngono za mitaani kama sio kuogopa kuambukizwa HIV?
 
Back
Top Bottom