Serikali inakiuka haki za Wakimbizi na wahamiaji binafsi kibinadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inakiuka haki za Wakimbizi na wahamiaji binafsi kibinadamu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Candid Scope, Aug 9, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Serikali inakiuka haki za Wakimbizi na wahamiaji binafsi kibinadamu
  Waziri Nchimbi ametetea watuhumiwa wahamiaji haramu nchini na Makongoro Mahanga amepingana na waziri mwenzake kuwa alishawafukuza watuhumiwa hao.

  Kuna jambo moja ambao watanzania na hata viongozi wanakiuka haki za binadamu katika idara ya uhamiaji, kwani kama mataifa mengi yangekuwa yanafanya hivyo wabeba mabox wengi huko majuu na kwingineko duniani wangesharudishwa makwao tukizingatia wengine walikuwa wazamiaji ambao hawakuingia na visa katika nchi husika. Hawa tunaowaongelea wameingia kwa visa halali, wamepitiliza muda na pengine hati zao za kazi kuisha muda wake au kuajiriwa kwa dirisha la nyuma ingawa kuna baadhi ambao wanaangukia kwenye jumba la walioingia bila visa kwa kutumia njia za panya.

  Jambo lingine ambalo limeibuka bungeni safari hii ni kauli ya kufukuzwa waadhirika wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kutoka nchi za Rwanda na Burundi, kwamba asiyeondoka atakuwa amevunja sheria ya nchi, lazima warudi kwao Watu hawa wengi wao wameishi Tanzania kwa miaka zaidi ya 10, 15, 20 nk, wana mashamba yao, na wengine wamejenga nyumba zao za kuishi na kushiriki maendeleo ya nchi. Si busara wala ubinadamu kufikia hatua hiyo badala ya kuwapa hiari ya kufanya hivyo.

  Mataifa mengine ya Ulaya na Marekani kaskazini Wakimbizi kwa kawaida wanapewa kipa umbele na uraia wa nchi wanazofikia ili kupooza machungu waliyopata, na baadhi ya mataifa hayapendi wakimbizi hao kurudia nchi walizokuwa ili kufuta saikolojia ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu na mauaji ya kinyama. Kwani wakimbizi wengi walishapotezana na ndugu zao, mali zao, nyumba na mengineyo, sasa kuwaambia warudi kwao ni sawa na kwenda kuwa wakimbizi katika nchi yao ya kuzaliwa kitu ambacho kwangu naona si utu na pengine kinyume cha haki za wakimbizi duniani na katu si ubinadamu.

  Tukirudi nyuma kwa wahamiaji wengine, mataifa mengi mhamiaji kama havunji sheria za nchi na anaendelea kuwa raia bora, suala la ajira kwa watu binafsi linabaki huru, ila serikalini na mashirika ya umma huwa vigumu. Haina maana serikali haijui uwepo wao, ila sababu kuu ya kuwaacha ni ubinadamu, kwani yaliyowapeleka huko ni matatizo ya kifamili, kijamii, kidini, kisiasa, kiuchumi nk. Kwa wanaovunja sheria hapo mkondo wa sheria huchukuliwa na hapo yatafumuliwa yote hata status ya ukazi wake katika nchi husika.

  Mataifa ya Ulaya na Marekani, utakuta biashara na makampuni binafsi, hoteli na nyumba nyingi za kulala wageni zinazomilikiwa na raia wa kigeni kama wahindi ambao ndio wanaoongoza, wafanyakazi wengi ni hao wahamiaji wasio na vibali vya kuishi wala kufanya kazi, lakini ni sekta binafsi haiingiliwi vinginevyo kuna uvunjaji wa sheria. Katika nchi hizo wapo wengi tu wafanyakazi ambao hawana hati za kuishia au hati zao ziliisha muda wake lakini bado wanaishi kwa kutegemea tu ajira kwa watu binafsi na serikali zinajua hilo.

  Kama ni tatizo la ajira ni la po pote duniani, huko nchi nyingine duniani ambako watanzania wapo wanakirimiwa kwa ajira hata wasioishi kihalali wapo wananchi wanaotaabika bila kupata ajira. Jambo hili lisifanywe kwa kukomoana bali kwa busara na ubinadamu.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sijafahamu sababu za kuwanyooshea sana vidole watu ambao wanasemekana wanaishi kinyume cha sheria nchini wakati wengi wao ni walipa kodi serikalini.
   
Loading...