Serikali inajua wizi wa mafuta Msimbati, Mtwara?

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Ndugu wana JF, kuna taarifa kuwa katika mkoa wa Mtwara eneo la Msimbati yako mafuta yanachimbwa na wachimbaji wana helkopta tano na wanaishi Dar es Salaam na wanaenda Mtwara na kurudi. Mafuta yanayochimbwa hayawanufaishi watanzania hata kidogo. inasemekena kuwa wachimbaji husafirisha mafuta kwa njia haramu na si serikali wala wakazi wa maeneo hayo haifaidiki kwa njia yoyote. Pia wachimbaji wamekuwa wanazuia mtu yeyote kuingia sehemu ya uchimbaji na waliojaribu wamepoteza maisha.

sasa ni namna gani tunaweza kupata taarifa zaidi?
Viongozi gani wanahusika na uhalamia huu unaoifilisi nchi?
Kwa walioko mtwara, tunaweza kupata taarifa zaidi?

nawasilisha
 
mmh hii imekaa ki udaku udaku!manake mafuta tunavyoyajua sisi ili yaweze kutumika ni lazima yapitie refinery!sasa hiyo helikopta ina uwezo wa kubeba mapipa mangapi ili hiyo business ilipe?ngumu kumeza hii!hebu tusubiri wenye data wamwage
 
Unatuhabarisha au unatuuliza?
Maneno haya si kweli.Wataalamu wanakaa Mtwara na Helicopter inawachukua asubuhi kuwapeleka kwenye meli yao ya utafiti,huwarudisha mchana na jioni.
 
Muulize Marriale kama kweli serikali haijui kitu kuhusu huo wizi wa mchana sasa mwaka wa pili.
 
Kule inapotoka Gesi including SongoSongo kila mwaka kunapatikana mafuta kiasi toka kwenye visima vya gesi au ndio hayo?But mafuta ya kujaza meli ili yalete faida kwa helkopta no! Labda kuna madini mengine yanachimba ki haramu sawa lakini mafuta kwa helkopta apana
 
Ndugu wana JF, kuna taarifa kuwa katika mkoa wa Mtwara eneo la Msimbati yako mafuta yanachimbwa na wachimbaji wana helkopta tano na wanaishi Dar es Salaam na wanaenda Mtwara na kurudi. Mafuta yanayochimbwa hayawanufaishi watanzania hata kidogo. inasemekena kuwa wachimbaji husafirisha mafuta kwa njia haramu na si serikali wala wakazi wa maeneo hayo haifaidiki kwa njia yoyote. Pia wachimbaji wamekuwa wanazuia mtu yeyote kuingia sehemu ya uchimbaji na waliojaribu wamepoteza maisha.

sasa ni namna gani tunaweza kupata taarifa zaidi?
Viongozi gani wanahusika na uhalamia huu unaoifilisi nchi?
Kwa walioko mtwara, tunaweza kupata taarifa zaidi?

nawasilisha

Usirukie tu kitu bila kufanya utafiti. Mtwara sasa ni oil and gas exploration base, kuna exploration activities nyingi sasa ambazo zinaendela kule deep sea, Mtwara ndio base ya hiyo kazi. Hivyo helikopta hupeleka wataalamu kwenye drill ship ambako uchimbaji wa mafuta unafanyika na si vinginevyo.Hakuna mafuta yaliyogunduliwa hapa Tanzania---bado tuko kwenye utafutaji

Acha upotoshaji ndugu.
 
Haaaa ni kweri tarihizo zimesikika na wanacho safirisha ni lile tope lake na huwa wananweka kwenye makontena na pia vigogo wa serikali hii wanajua swara hili na pesa zinaingia mifukoni mwao tu na si nchiii.
 
Ndugu wana JF, kuna taarifa kuwa katika mkoa wa Mtwara eneo la Msimbati yako mafuta yanachimbwa na wachimbaji wana helkopta tano na wanaishi Dar es Salaam na wanaenda Mtwara na kurudi. Mafuta yanayochimbwa hayawanufaishi watanzania hata kidogo. inasemekena kuwa wachimbaji husafirisha mafuta kwa njia haramu na si serikali wala wakazi wa maeneo hayo haifaidiki kwa njia yoyote. Pia wachimbaji wamekuwa wanazuia mtu yeyote kuingia sehemu ya uchimbaji na waliojaribu wamepoteza maisha.

sasa ni namna gani tunaweza kupata taarifa zaidi?
Viongozi gani wanahusika na uhalamia huu unaoifilisi nchi?
Kwa walioko mtwara, tunaweza kupata taarifa zaidi?

nawasilisha
Miye nachukia Ufisadi lakini vile vile nachukia maneno haya "inasemekana" hakiki taarifa yako iwe na uhakika halafu post!!
 
kibiashara huwezi kusafirisha mafuta kwa helikopta.....haiwezi kulipa.. ..labda kama wanachukua malighafi nyingine...uchunguzi ufanyike
 
Back
Top Bottom