Serikali inaihujumu NSSF?

J4MAYOKA

Senior Member
Jul 16, 2011
147
84
NSSF ilikuwa wainunue Kiwira kwa shilingi 1 toka serikalini ..waziri wa Usiku aka NGELEJA akaamua kuwapa wa China

NSSF waliandaa business plan ya kupanua pipeline mpya ya gesi toka Songosongo...leo tunasoma kuwa waziri wa usiku kaamua wapewe waChina

sasa inaonekana NSSF kazi yao kuandika business plans kisha waziri wa usiku anatuma watu kwenda pale kwa akina Kidula na kisha wanazipeleka huko Uchina

naona hii ni nchi pekee duniani isiyotaka wazalendo wafanye kazi yoyote ile

Tenda za constrction zote sasa hizi serikali inawapa wa China kuanzia barabara mpaka majengo...ma contractor wazalendo wanafunga makampuni

I wouldnt be surprised kuskia leseni za uvuvi zote zinapewa exclusively wachina
 
Kabla ya kuilaumu serikali, tujiangalie na sisi wenyewe ambao ni vinara wa kuilaumu serikali!!! Nakumbuka hata Mwanakijiji, kama sio humu JF basi makala kwenye gazeti alishawahi kupinga suala la NSSF kujiingiza kwenye suala la uzalishaji wa umeme kupitia hiyo hiyo kiwira!!!
 
Kazi za miradi mikubwa ya nishati na miundo mbinu ni za serekali. Nssf wanatakiwa kufikiria kuwekeza kwenye miradi ambayo itawasadia wanachama wake moja kwa moja, kama makazi ya bei nafuu, vile vile wafikirie kuboresha mafao ya wanachama.
Kukimbilia kwenye hiyo miradi wanachama tuna mashaka na uadilifu wenu nssf kwenye hiyo miradi.
 
Tatizo ni kuwa watu wanataka kuifanya NSSF kuwa badala ya serikali. Kila serikali inaposhindwa inakimbilia kutumia fedha za wanachama wa mifuko hii. Matokeo yake ni kuwa serikali itaacha kufanya majukumu yake na kuyadefer kwa NSSF, PPF n.k Binafsi ningependa kuona mifuko hii inaboresha zaidi mafao ya wanachama wake. Leo hii kujitamba kuwa mtu analipwa mafao ya 80,000 kwa mwezi ambayo hayafikii hata kima cha chini halafu kutaka kwenda kutumia bilioni 1 kwa ajili ya umeme ni kutowatendea haki wanachama.
 
Kwanza hao NSSF ndiyo wanaopiga dana dana ya daraja la kigamboni. Kwanza kwa sifa ya ufisadi katika miradi mingi ya NSSF bora wasipewe kabisa hiyo miradi maana utasikia kapewa u-agent Manji na bei itakuwa inflated.
 
nssf kuwalipa wanachama wake mafao yao ni bonge la mbinde utafikiri hiyo ela unawaomba mkopo kumbe walikuwekea na riba yenyewe wanayotoa ni ndogo sana wakati mwanachama aliwapa mtaji wazalishe , kuna uzembe usio na mfano katika utendaji wao wa kazi Je wataweza hiyo miradi mikubwa kama sio nao wanatamaa ya kifisadi??? waboreshe kwanza walicho nacho kabla ya kukimbilia vitu vikubwa zaidi
 
Halafu miradi hii isiyo na tija inayofahamika ni kutaka kuzamisha hela za wananchi.
 
Nssf bora wamenyimwa hizo kazi! Nani asiyejua hizo ni mishemishe za watu? Kazi ya million ishirini huwa wanaifanya kwa million themanini. Kama noma na iwe noma, booora wamezibeba wachina
 
NSSF ilikuwa wainunue Kiwira kwa shilingi 1 toka serikalini ..waziri wa Usiku aka NGELEJA akaamua kuwapa wa China

NSSF waliandaa business plan ya kupanua pipeline mpya ya gesi toka Songosongo...leo tunasoma kuwa waziri wa usiku kaamua wapewe waChina

sasa inaonekana NSSF kazi yao kuandika business plans kisha waziri wa usiku anatuma watu kwenda pale kwa akina Kidula na kisha wanazipeleka huko Uchina

naona hii ni nchi pekee duniani isiyotaka wazalendo wafanye kazi yoyote ile

Tenda za constrction zote sasa hizi serikali inawapa wa China kuanzia barabara mpaka majengo...ma contractor wazalendo wanafunga makampuni

I wouldnt be surprised kuskia leseni za uvuvi zote zinapewa exclusively wachina

Kwa hili namuunga mkono waziri wa usiku. Badala ya NSSF kujikita kwenye kuboresha mafao ya wastaafu wao wamekuwa wakiingia kwenye miradi ya kisiasa ili kupata sifa toka kwa wanasiasa.
 
Alipewa mtoto wa King**** barabara ya Tabata-Kimanga /Mawenzi (Dar) aweke level ya lami lakini ikawa mavumbi na mashimo matupu. Kwa ueledi na ufisadi huu kweli wa tz tuna aminika tupewe miradi mikubwa?
 
Daraja la kigamboni , michoro, tathmmini, na garama zooote tayari , nssf wanasubiri kauli ya serikali toka mwaka jana, na gharama sasa zinazidi kuongezeka serikali iko kimyaaaaaaaaaaaa. Usije shangaa wanasmpa rostam
 
Tatizo ni kuwa watu wanataka kuifanya NSSF kuwa badala ya serikali. Kila serikali inaposhindwa inakimbilia kutumia fedha za wanachama wa mifuko hii. Matokeo yake ni kuwa serikali itaacha kufanya majukumu yake na kuyadefer kwa NSSF, PPF n.k Binafsi ningependa kuona mifuko hii inaboresha zaidi mafao ya wanachama wake. Leo hii kujitamba kuwa mtu analipwa mafao ya 80,000 kwa mwezi ambayo hayafikii hata kima cha chini halafu kutaka kwenda kutumia bilioni 1 kwa ajili ya umeme ni kutowatendea haki wanachama.

Mzee Mwanakijiji nakubaliana na wewe 100% NSSF badala ya Kujikita kutoa Mafao bora kwa wanachama imegeuka kuwa kampuni ya Uwekezaji!
Pamoja na kwamba ndio mfuko mkubwa ila ndio Unaotoa mafao kiduchu kwa wanachama wake na Serkali Inaangalia!
Mathalan,Fedha ya Mkupuo anayopewa mtu(Mwanachama) anayestaafu wa NSSF ni Kiduchu sana ukifananisha na Mifuko ya LAPF na PSPF!
Kuna kisa Kimoja cha nesi wa Peramiho Hospital kulalama kulipwa mafao ya mkupuo mkia wa mbuzi na NSSF ukilinganisha na nesi mwenzake Waliostaafu pamoja Ambae kapata mkupuo wa zaidi ya 60M kutoka mfuko mwingine wakati yeye wa NSSF kaambulia chini ya 30M!
Kitu kingine cha Shangaza,NSSF kujishebedua na Huduma za Afya kwa wanachama na ninyi watu wa Ughaibini wakati Tayari Taifa lina BIMA ya Afya!Hakuna haja ya mashirika ya Umma kuhangaikia kazi moja,ni bora wakaa pamoja ili swala la matibabu liratibiwa na chombo kimoja Kitaifa kwa ajili ya Ufanisi!Nanyie ndg zetu wa Ughaibuni nasika mmeingia mtego wa NSSF eti mtibiwe na ndugu zenu wa huku!NSSF Ni BIMA tangu lini kama tayari kuna NHIF ni bora nguvu za Afya zikapelekwa huko!
 
something really NASTY is being played tena jina la JK linatumika na mbaya zaidi looks like NSSF washapigwa bao.
 
Kama wana pesa nyingi waende serikali waongeze mafao kwa wazee wote (universal benefits) wa Tanzania
 
Kwanza hao NSSF ndiyo wanaopiga dana dana ya daraja la kigamboni. Kwanza kwa sifa ya ufisadi katika miradi mingi ya NSSF bora wasipewe kabisa hiyo miradi maana utasikia kapewa u-agent Manji na bei itakuwa inflated.

Nssf inajihujumu yenyewe
 
NSSF wamejipanga vizuri sana yahitaji tuwape moyo, nafikiri hayo makosa ni madogo sana ulinganisha na juhudi kubwa walizofanya katika ujenzi wa jamii.
 
Nssf hawana lolote mkitaka kuthibitisha someni gazeti la leo la business times,mitambo waliokuwa wameahidi kuipatia tanesco ili kukabiliana na tatizo la umeme wameshindwa aibu tubu
 
Kama wana pesa nyingi waende serikali waongeze mafao kwa wazee wote (universal benefits) wa Tanzania

Mkuu huu ni ukweli kabisa NSSF wao ni kudandia miradi ili kuthibitisha ninachosema watuonyeshe mradi wowote ambao wamebuni hata jengo la Benjamini Mkapa walipewa kutoka TPDC
 
Back
Top Bottom