Serikali inahitaji trilioni 5 Kukamilisha Barabara zote kuu Tanzania

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,289
2,000
Barabara kuu ni zile zinazo unganisha mikoa na baadhi ya wilaya (Trunk Road). Hadi sasa kati ya KM 12000 paved ni km 7000 .. kwa hiyo km 4000-5000 bado zinavumbi, hapa nazungumzia kama barabara ya kutoka dar hadi kigoma kupitia tabora..

Kwa maana hiyo kila mwaka serikali inahitaji kuweka lami km 1000 sawa na tr 1 kwa bei ya bil 1/km kwa mwaka ambayo ni sawa na kutumia makusanyo ya kodi ya mwezi mmoja, kama itaweka lengo LA kumaliza km 5000 ndani ya miaka 5.

Hapo barabara za mikoa hazihusiki ..
FB_IMG_1479924181357.jpg
 
Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,337
2,000
Vipaumbele viko shaghala baghala. Usisahau kuna Chartor International Airport (CIA) na ndege nne zaidi ambazo zimeanza kulipiwa advances! Hebu tuone mkusanyaji kodi ambaye ndo mlipaji na muidhinishaji; huyo ambaye yeye ndo mambo yote kwenye procurement (aliye juu ya sheria zote ikiwemo ile ya PPRA); hebu tuone anafanyaje!
 
kinacho sikitisha ni kwamba toka Uhuru hatujaweza kumaliza km 12000 ambazo zinaunganisha mikoa na nchi za nje, mfano hadi Leo huwezi fika kigoma bila kula vumbi, karne ya 21 ..
 
Manstone

JF-Expert Member
May 12, 2013
481
500
Mbona Kigoma Mnalalamika Sana Hamieni Kwetu Musoma, Maana Mpaka Sasa Lami Ya Zamani Tumebomoa Tumeweka Mpya.
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,289
2,000
Mbona Kigoma Mnalalamika Sana Hamieni Kwetu Musoma, Maana Mpaka Sasa Lami Ya Zamani Tumebomoa Tumeweka Mpya.
huko musoma hamjaunganishwa na arusha hadi Leo, hakuna barabara ya lami toka arusha hadi Mara. Hapa tunazungumzia barabara kuu..
 
ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,636
2,000
Vipaumbele viko shaghala baghala. Usisahau kuna Chartor International Airport (CIA) na ndege nne zaidi ambazo zimeanza kulipiwa advances! Hebu tuone mkusanyaji kodi ambaye ndo mlipaji na muidhinishaji; huyo ambaye yeye ndo mambo yote kwenye procurement (aliye juu ya sheria zote ikiwemo ile ya PPRA); hebu tuone anafanyaje!
Ununuzi wa ndege cash kuna Madalali wanachukua 10% zao pindi cash ikilipwa ndiyo maana ununuzi wa cash umesimamiwa na Lipumba ambaye ni mshauri mkuu wa Uchumi pia tenda za kujenga uwanja wa ndege Chato Lipumba ana mkono wake.
 
ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,636
2,000
kinacho sikitisha ni kwamba toka Uhuru hatujaweza kumaliza km 12000 ambazo zinaunganisha mikoa na nchi za nje, mfano hadi Leo huwezi fika kigoma bila kula vumbi, karne ya 21 ..
Pesa zote anakula Lipumba kwa ajili ya kudhoofisha upinzani ni vigumu kigoma wajengewe barabara.
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Anajiamulia tu, hafuati bajeti ya bunge, anafanya mambo kwa kutumia akili yake kama vile yeye ni malaika hafuati katiba, yaani nchi inaendeshwa kama Shamba la mtu na vibarua wake
 
mshumbue-soi

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
1,846
2,000
Ununuzi wa ndege cash kuna Madalali wanachukua 10% zao pindi cash ikilipwa ndiyo maana ununuzi wa cash umesimamiwa na Lipumba ambaye ni mshauri mkuu wa Uchumi pia tenda za kujenga uwanja wa ndege Chato Lipumba ana mkono wake.
Ina maana Lipumba yuko kazini kimya kimya kama wale wanajeshi wa gwaride la kimya kimya?
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
10,906
2,000
Mwacheni awatumikie wananchi walimpa kura, yeye na mama Samia ndio walizunguka nchi nzima kuomba kura na sio nyie!
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
49,347
2,000
Hata hyo trillion 5 ikipatikana bado utambiwa inahitajika tena trillion 3 kumalizia kbsa

Ova
 
Watu

JF-Expert Member
May 12, 2008
3,230
2,000
Barabara kuu ni zile zinazo unganisha mikoa na baadhi ya wilaya (Trunk Road). Hadi sasa kati ya KM 12000 paved ni km 7000 .. kwa hiyo km 4000-5000 bado zinavumbi, hapa nazungumzia kama barabara ya kutoka dar hadi kigoma kupitia tabora..

Kwa maana hiyo kila mwaka serikali inahitaji kuweka lami km 1000 sawa na tr 1 kwa bei ya bil 1/km kwa mwaka ambayo ni sawa na kutumia makusanyo ya kodi ya mwezi mmoja, kama itaweka lengo LA kumaliza km 5000 ndani ya miaka 5.

Hapo barabara za mikoa hazihusiki ..
View attachment 451469
Umetembea na Kuzunguka Tanzania? au kwenu ni kigoma? nenada pale Ubungo? utakosa direct bus ya kwenda pande ipi ya tanzania hii?

Kwa barabara Tanzania tunajitahidi sana? hata hizo za vumbi nyingi zinapitika all season hakuna road ilikuwa chafu kama pale muhoro kwenda kusini? lakini imewekwa sawa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom