Serikali inahaha kumtafuta alau mtu wa kuvaa koti jeupe anekane daktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inahaha kumtafuta alau mtu wa kuvaa koti jeupe anekane daktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mayoscissors, Jun 25, 2012.

 1. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha sana serikali yetu isiyo makini kiasi kwamba inawachukua medical students wapite mawodini ili public ijue hamna mgomo.Leo muhimbili kazi hamna na wananchi wenyewe watasema hata kama vyombo vya habari vimekatazwa kutangaza habari za mgomo.Naishauri serikali itoe pamba masikioni amasivyo itangoka na wazalendo kuendesha nchi.
   
 2. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Udhaifu ndio huo!kwenye mgomo w walimu sijui watatafuta fimbo na chaki?dhaifu bhana,ni dhaifu tu.
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  huu mgomo kweli upo au tishia nyau kama kawa!!
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Haya bhana,,,,,,
  ukweli ni uhuru
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,814
  Likes Received: 36,902
  Trophy Points: 280
  Wauza bucha si wanavaa makoti meupe?

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 6. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wanawapa kamati ya katiba Tsh 450,000 kwa siku kila mjumbe. Hii ni haki kweli-hatuvai mjoho mpaka kieleweke
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Na wakilegea safari hii,basi madaktari wajihesabie kuishia mortuary
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wabunge wakilalamika posho wanaongezewa...madaktari walimu wakilalamika wanakaa kimya...juzi nilipita kituo cha polisi cha oysterbay nikaona zile nyumba za polisi pale kiliniuma sana kuona binadamu ambao wanatakiwa watulinde sisi na mali zetu wanaishi sehemu zile. Ndio maana mapolisi wengine wanaamua kuchukua rushwa au kuwa majambazi maana hali ni ngumu.

  Nawapeni mfano, angalia ofisi mpya za serikali zinavyojengwa, angalia nyumba za mawaziri kule oysterbay/masaki. Je kweli serikali inashindwa kuwajengea polisi nyumba zenye hali nzuri wakaishi na familia zao kama binadamu wengine wa kawaida?
   
 9. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,931
  Trophy Points: 280
  Mkuu Daudi,mbona hututakii mema? wewe unajua wazi serikali yetu ilivyo dhaifu,usije acha ikachukua ushauri wako tukakutana na wauza bucha Muhimbili bure!
   
 10. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Serikale haibabaishwi ba vidaktari uchwara hamna lolooote hata mgome mwaka wagonjwa watapona tUuu mlieee nyieeee
   
 11. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ni kweli kabisa!serikali hamjali mwananchi au mtetezi wake.
  hivi kwa nini serikali ilikurupuka kwenda mahakamani?
   
 12. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu Jackbauer, Mopaozi anatibiwa nje ya nchi! hajui watu wengine wanatibiwaje, anasema hivyo kutetea watawala ili waendelee kutibiwa nje ya nchi!!
   
 13. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tuna rais dhaifu sana, asiyejua ni yapi majukumu yake, amekaa pale ikulu kama zuzu tu, rais mnafiki na asiyekuwa na uchungu na Taifa lake. Inashangaza sana, juzi kwenye mauaji ya raia wa Denmark kule mbugani Serengeti JK alikuwa very fast kutoa executive directives kwa mawaziri wake (Kagasheki na Nchmbi), lakini kwa swala la msingi na muhimu kama hili la madaktari JK amekaa kimya, as if hakuna kinachotokea. JK hatufai kabisa watanzania, hafai kuendelea kututumikia sisi wananchi, mbaya zaidi, sisi wananchi tunaendelea kumuacha akifanya madudu yake tu. Tubadilike jamani, tuandamane tukamtoe pale ikulu, hawezi kutupiga risasi raia wote, afterall akileta mzaha ICC itakuya yake...
   
 14. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,398
  Likes Received: 6,587
  Trophy Points: 280
  Tuwe wakweli waungwana..katika sekta inayonisikitisha hapa nchini ni ya afya..nenda hospitali za serikali..utakoma ubishi..kwanza wodi ni chafu na zinanuka( naomba radhi kam anitakua nimekosea) hakuna vipimo, hakuna madawa, hakuna wataalam wa kutosha..ukienda hospitali..hata ukiumwa ugonjwa gani...lazima wakupime malaria kwanza....hali ni mbaya sana..inanishangaza watu kukaa bungeni na kujadili bajeti ya matrilioni huku wakiisahau sekta ya afya...unataka kutawala wafu?? hamuoni kuwa kiongozi anakua bora kama akiwa na wananchi wenye afya?? vipi taifa litaendelea bila kuwa na watu wenye afya??? Kuna zaidi ya UHAI???? Hii nini kama si UUAJI??? siku moja nilikwenda mwananyamala , nikakuta foleni kubwa balaa unapima leo unaambiwa majibu kesho...haya kwenye dawa sasa..unakuta vilio vya watu..hawana pesa za kununulia dawa..unakuta mama kabeba mwanae amelala mgongoni...hoi..analia hana hata buku ya kununua dawa!!!! Hapo huko bungeni..watu wanadai oo sijui sekta ya afya sijui nini..porojo tu...hatuna viongozi..ni wauaji tu...Kazi kwenda ulaya kila siku na kupost trip zao wakiwa washington dc, uk wapi huko...Huyo mnaemsifia sijui zito sijui nani??? Ushawahi mwona akitembelea hata wodi moja ya wagonjwa??? kuangalia jinsi sekta ya afya ilivyoteketea??? watu wanakufa kwa kukosa matuibabu sahihi kila siku kwa mamia..asilimia kubwa ya magonjwa ya watanzania...inatokana na lishe duni pamoja na kuishi maisha hatarishi...kisa?? hali ngumu ya maisha...imesababishwa na nani??? Viongozi wote....si serikali wala wapinzani..wote wapenda anasa tu..hakuna afadhali...WAUAJI WAKUBWA NYIE!!!
   
 15. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mimi ndo nasema hivi, kama hii tabia ya sisi kwa sisi kutokujipenda itaendelea! ipo siku moja tutaanza kugawana kile wenzetu tunaoishi nao hapa hapa nchini bila kuangalia kazipata vipi. Haiwezekani binadamu mwenzako anakosa dawa ya elfu moja wewe unaitumia hiyo elfu moja pengine kwa kununulia chungwa moja au vyovyote harafu unashindwa hata kutengeneza mazingira mazuri ya huyo mtu basi afanye kazi aweze kugharamia huduma mhimu. Its nonesense!!
   
 16. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hivi mnaopinga mnaenda kutibiwa kwenye hizo hospitali au mwaenda kwenye hizo za private? Jaribuni kuangalia hizo hospitali zinazoitwa za serikali kama mtakuta kitu au mjionee wenyewe vifo vya kizembe jamani pengine hamtakuja kutetea utumbo hapa.
   
Loading...