Serikali inafanya kazi kimyakimya juu ya waliohusika na Operesheni Tokomeza!

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
3,216
988
Kama kweli basi nawapongeza!

Nimeambiwa serikali imeanza kuwasimamisha kazi baadhi ya watendaji katika wizara ya maliasili. Na wanalenga kuwaondoa kabisa askari waliohusika na utesaji wa raia.

Katibu mkuu wa wizara ya mifugo pia inadaiwa amepumzishwa lakini yote haya ni kimyakimya.

Tunaomba wana JF mliopo katika maeneo hayo mtupatie mrejesho wa ukweli juu ya hayo
 
Nchi haitatawalika kauli hiyo. Mkaanza anataka kuleta vita, anavuruga nchi. Sasa m prove, umeme umepanda inamaana bado tunatafunwa na richimond ya Lowassa, Serikali inapomoka kila uchwao inaonekana hakuna anaefaa kabisa, makada wanaogopa kuvaa hata vitaa maana kila wakionekana huwa ni vigumu kuwatofautisha na vibaka. Tunaomba muondoke mtuachiachie nchi yetu period
 
Basi hii ni kimyakimya sana yaani mpaka PS wa wizara anapumzishwa bila taharifa kuvuja mitandaoni? labda!
 
Hii inanikumbusha story ya Mkurugenzi wa wanyamapori kipindi kile ya utoroshwaji wa Twiga wakamsimamisha kwa mbwembwe kisha baada tukasikia amerudishwa! Bongo ni Zaidi ya Holwood
 
Kababu, uongo huwa una mwisho wake. Kwani Mbowe na mkakati unaousema ndio umehusika pia na operesheni tokomeza iliyotesa wananchi?
 
Hii ni Serikali dhalimu nimelisema hilo siku nyingi sana, wanachokifanya ni danganya toto tu hakuna mkubwa yeyote wa vyombo vya dola atakayeondolewa kazini.

Itakuwa haina maana kama wakuu wa vyombo vya dola nao hawatasimamishwa.
 
Basi hii ni kimyakimya sana yaani mpaka PS wa wizara anapumzishwa bila taharifa kuvuja mitandaoni? labda!
Nimeuliza waandishi wa habari kadhaa wameniambia kweli PS mifugo hayupo ofisini
 
Presentation1.jpg Hawa maliasili wameonyesha hakuna waziri lakini wizara zingine bado zinaonyesha mawaziri walioshushwa, naona kuna tofauti ya utendaji tu. Wengine wanasema wengine labda kwa unafiki wao tu ndiyo hawasemi kujipendekeza kwa viongozi walioshushwa.
 
Back
Top Bottom