Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama hujui nyamaza...Ila wabongo tunalalamika aiseeeeee.
Kwenye kila kitu. Kila kitu.
Nimesema suala hili kwa muda mrefu.mimi napendekeza kustaafu iwe hata 45yrs.tatizo litakwisha.Au iwe ajira za mkataba wa miaka 10-15tu.Suluhisho ni kupunguza muda kustaafu kutoka 60 hadi 50 serikalini.
Pia serikali kuweka mazingira rafiki ili makampuni binafsi yawe mengi, maana ndio wazalishaji wa ajira.
Bila kusahau mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ili raia wajiajiri kupitia biashara.
Cheka sana, furahi sana lakini omba yasikukute!BACHELOR DEGREE??? 🤣🤣😃😃😁😁
POLE SANA
Hadi 45Suluhisho ni kupunguza muda kustaafu kutoka 60 hadi 50 serikalini.
Pia serikali kuweka mazingira rafiki ili makampuni binafsi yawe mengi, maana ndio wazalishaji wa ajira.
Bila kusahau mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ili raia wajiajiri kupitia biashara.
Taratibu zakazi huwa haziangalii daraja ya masomo ya juu huwa unatangaza kuanzia hapa.Serikali mara kwa mara imekuwa ikiwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kufaulu lakini jambo la kusikitisha unapofika wakati wa ajira serikali hiyo hiyo inawabagua tena.
Tumeona kwenye ajira za polisi wanaotakiwa ni wale ambao hawakufanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne. Yaani waliopata divisheni Four ila waliofaulu vizuri kwa kupata divisheni one na Two hawatakiwi.
Sanjari na hilo, kuna ubaguzi mkubwa unafanywa na serikali kwenye utoaji wa ajira hasa kwa wahitimu wenye elimu ya juu i.e bachelor degree holders kulinganisha na level zingine za kielimu kama vile diploma na certificate.
Mfano mimi nimehitimu kidato cha nne mwaka 2011. Kwakuwa nilikuwa na ndoto ya kufika mbali kielimu kama serikali inavyosisitiza, nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita.
Sikuishia hapo, niliendelea kukazana kwa nguvu zote na maarifa yote na hatimaye nikafanikiwa kuendelea na elimu ya juu na sasa ni mhitimu wa moja ya chuo kikubwa hapa nchini
Lakini katika yote, wenzangu niliomaliza nao kidato cha nne wakapata ufaulu wa divisheni Four kisha kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti leo hii ni waajiriwa wa serikali wanakula keki ya Taifa.
Niliomaliza nao kidato cha sita wakakosa sifa (qualifications) za kujiunga chuo kikuu wakaenda kusomea ualimu ngazi ya diploma tayari wote wameajiriwa serikalini
Lakini mimi niliyefuata ushauri wa serikali wa kusoma kwa bidii na kufaulu kwa kufikia kiwango cha elimu ya juu leo naonekana sina thamani kwani serikali ile ile iliyonihamasisha kusoma kwa bidii ndio ile ile imeniweka mtaani kwa takribani miaka minne sasa. Kwa maana nyingine kiherehere changu cha kusoma kwa bidii na kufaulu leo hii ndio kinaniponza kwa sababu kama ningefeli kidato cha nne au sita leo ningekuwa ni miongoni mwa wanaofaidi keki ya Taifa.
Mwisho wa yote kama serikali haina mpango wa kuajiri wahitimu wenye bachelor degree tunaomba itamke hadharani ilikusudi vijana tujue moja kwani hata ajira zinapotangazwa wenye bachelor degree wanaoajiriwa ni wachache sana tena nafikiri ni katika jitihada za serikali kuficha dhambi ya ubaguzi wanayoifanya isijulikane kirahisi.
Hongera mungu azidi kukutanguliaNina division four yangu safi ya form four, sasa hivi nipo ofisi nyeti ya serikali napiga kazi😏
Hivi kama unamchukuwa kijana wa dv4 una mpa kaz anaifanya vizuri alafu una mchukia wa dv1 anafanya kama darasa la Saba wewe unge muajiri nani? Elimu imeimgiliwa mm naona sawa tu.Serikali mara kwa mara imekuwa ikiwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kufaulu lakini jambo la kusikitisha unapofika wakati wa ajira serikali hiyo hiyo inawabagua tena.