Serikali Ina Wajibu wa Kuhakikisha Raia Wake Hawadhulumiwi Maisha au Mali Zao

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,794
Moja ya majukumu makubwa kabisa ya serikali ni kuwalinda watu wake dhidi ya changamoto zote za kiusalama na kuwahakikishia amani na utulivu.

Jukumu la Serikali si tu kulinda watu wake kutokana na mashambulizi ya nje, lakini pia kuwalinda dhidi ya changamoto zote za kiusalama zinazoweza kujitokeza ndani ya nchi na miongoni mwa wananchi husika. Serikali inapaswa kuhakikisha sheria na taratibu za nchi zinafuatwa na amani pamoja na utulivu vinadumishwa kupitia vyombo vyake vya usalama.

Serikali inapaswa kulinda maisha na mali za watu binafsi na serikali kwani uwepo wa serikali unategemea ulinzi wa maisha ya watu na mali. Ulinzi wa maisha na mali unahusisha raia kuwa na uhuru wa kufanya shughuli zao na kuishi bila woga wa kuvamiwa au kutishwa. Na hii ndiyo sababu kuu ya kuwa na vyombo vya usalama.

Vyombo hivi ambavyo vinaendeshwa kwa fedha zinazotokana na wananchi havipaswi kuweka kipaumbele kwa viongozi na matajiri tu – kila mmoja anapaswa kunufaika navyo.

Kushindwa kwa serikali kudumisha usalama ni ukiukaji mkubwa wa majukumu yake kwa wananchi pamoja na ukikaji wa haki za binadamu. Kuishi, kuwa uhuru na kumiliki mali ni haki ambazo kila mmoja anapaswa kuzipata. Serikali ina jukumu la kuzilinda.

Serikali lazima ichukue hatua mahususi ili kulinda kikamilifu na kutimiza haki ya kuishi kwa kila mtu, bila kujali mazingira yao au hadhi zao. Sehemu muhimu ya wajibu wa serikali ni kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayedhulumiwa maisha yake kiholela.

Serikali ni chombo ambacho mamlaka yote ya nchi yamekabidhiwa kweke. Kwa hiyo, katika suala hili, serikali ina majukumu mbalimbali ambayo inapaswa kuyatimiza kwa wananchi wake. Baadhi ya majukumu hayo yanaitaka serikali kushirikiana na jamii kwa ajili ya utekelezaji ipasavyo, huku majukumu mengine yakitekelezwa na serikali pekee.

Hata hivyo, yote ni muhimu kwa usawa, hasa katika kuhakikisha kuwa jamii inapiga hatua kisiasa, kijamii na kiuchumi. Kwa hiyo ni wajibu wa serikali kuhakikisha kwamba majukumu yake yote yametekelezwa, lakini si kutekelezwa tu, bali kutekelezwa kwa njia bora zaidi.
 
Eti kuna 'vijikundi' vya wahuni vinawashinda nguvu wanausalama wenye mafunzo, waliotumia mabilioni ya walipakodi kupata mafunzo, ambao pia bado wanatumia jasho letu kutunza familia zao. Ajabu!
Tena wenye zana na vifaa na teknolojia juu.

Ingekuwa ni vijana wachadema wanaofanya mikutan8 tu, tena ya amani wangejua mkono wa dola😅😅
 
Back
Top Bottom