Serikali ina taarifa kuwa Mabenki yanapunguza na kufukuza wafanyakazi?

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
861
1,097
Waziri anayehusika na kazi anayo habari kuwa mamia ya wafanyakazi katika mabenki mbali mbali hapa nchini wamepoteza ajira kwa kufukuzwa?

Walianza Access, Finca na sasa Stanchart na mengine binafsi isipokuwa yanayomilikiwa na serikali. Kibaya zaidi wafanyakazi wanalipwa mafao duni na wengine kubambikiziwa makosa. Waziri wa kazi upo wapi?
 
Kwahiyo unazani ukifanya kazi benk ukasababisha hasara kwa uzembe wako usifukuzwe? Hapa waziri anahusikaje? Ukifukuzwa kwani hujui mahakamani? Siukafungue madai kama una haki? Unamuitiaje waziri wa kazi ujinga wako?
 
Wanafanya retrenchment at a low costs kosa kidogo tu mfanyakazi anafukuzwa kazi badala ya kutumia taratibu zinazotakiwa za retrenchment
 
Nafikiri techolojia nayo itasababisha benki wahitaji wafanyakazi wachache, nilipokuwa majuu kuna branch unakuta ina mtu mmoja tu kwa ajili ya shughuli za customer service. Ukitaka kutoa, kuweka pesa, kuhamisha, kufanya malipo wanatumia ATM machine au internet banking.

Sijajua kwa nini internet banking bado haijafika bongo, lakini akaunti yangu niliyokuwa natumia nje nilikuwa naweza kuingia, kutazama salio, kuhamisha pesa yaani sikuwahi kabisa kurudi ndani ya benki baada ya kufungua.

Kuna siku niliingia branch kuweka pesa wakanirudisha kwenye ATM wakanielekeza namna ya ku- deposit kwa kutumia ATM.
 
Unalalamika wafanyakazi kufukuzwa hujui wakati huu corona imepiga kila sekta ya biashara? Yaani wakuwache kazini wakati wao hawapati faida


Lunatic

Hilo nalo neno
Wakati dunia nzima wanalia
Hata Bank nyingi zinafunga high street kwa gharama wameamua kwa hasara wanazopata
Eti itakuwa sisi
 
Halafu malipo kwa cash yamepungua sana kwa wazungu na kuna wengine hawakubali kabisa kuchukua pesa, mimi nilikuwa hadi nitoe pesa kwenye ATM ndo nikanunue vitu, tunaelekea kwenye cash-less society ambapo maisha yote hutashika pesa mkononi.
 
Aisee Ila kuna kitu kila nikikiangalia kinanipa utata juu ya hatima ya elimu yetu. Mfano mafundi wengi wazuri wa magari mtaani hawajatoka VETA wala DIT na Tech nyingine bali wote ni 'darasa la 7' na wako vizuri sana.

Sasa wale wenye degrees na diploma za banking wengine hata kutoka nje ya nchi wakiwa wanajiandaa kulinga na mashati yao ya blue na meupe mara paap unakutana na mawakala ambao wanaserve bank zote kwa level ileile, tena cha zaidi wao wanakuwa wazi saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku tofauti na banki ambazo zinafunguliwa saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni. Uliza walisomea wapi sasa ndio utajua tulipo palivyo pagumu
 
Back
Top Bottom